Hivi kwanini klabu ya Yanga inashindwa kuheshimu logo za klabu nyingine?

Hilo ni tangazo tu la burudani.Sio official kiivyo ndo maana hata wenye timu hawalalamiki.Hilo Tangazo liko kiburudani zaidi.Kwa hiyo rangi zisikusumbue wala kukuchanganya sana.
Sema huenda wao Yanga waliwasiliana na wenye timu kuwauliza kama wafanye hivyo ndo maana wakakubaliwa. Lakini kama kungekuwa na shida ungeona Wenye timu zao wakilalamika au hata wachambuzi wa mpira wanaojua mpira kuliko sisi wangeshaonyesha wasiwasi.Lakin kama wako kimya ujue everything is on right track.Japo sio vizuri kubadili logo hata rangi kama hujamtaarifu mwenyw logo lakin kwa burudani aaah!hiyo kawaida tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kama jambo ujui uliza kwanza kuliko kuleta ujinga katikati ya waelewa.
Kwenye Logo kila kitu kinatafsiriwa Kwenye katiba sasa wewe unasemaje rangi hazina maana. Kwa nini msingekua mnaweka rangi nyekundu Kwenye Logo ya Yanga ka rangi hazina maana?
Logo ndo identity ya taasisi. Ndo mana hata mchezaji hua anabusu logo sio jezi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikiliza kaka.Rangi sio logo.Tafuta matangazo mengi kama 10 hivi ya kampuni tofauti tofauti tofauti.Kisha angalia logo zinafanana kwa kila kitu hasahasa rangi.Jibu ni HAPANA. Nakupa mfano mdogo tu.Logo halisi ya azam tv anayeonesha VPL ni maneno azam ni mekundu kisha neno TV ni rangi blue kisha kuna ile naweza kusema alama ya Tik iliyokama paa la maneno Azam tV ni rangi ya blue pia.

Sasa ukija kwenye baadhi ya situation utaona azam wanatumia logo hii(AZAM TV) ikiwa meupe yote)angalia picha hapa chini.Lakin official logo ni ile yenye maandishi nyekundu na blue.lakin baadhi ya situation utaona logo yote nyeupe.si ajabu pia kuona logo hii ya azam Tv ni nyeusi yote.
Lakin ukweli unabaki kuwa logo ya azam haijabadilika inabaki ileile. Sasa kama kuna kitu bado sijaelewa basi nielimishe kaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Attachments

  • Screenshot_2020-02-15-10-14-07.jpeg
    33.8 KB · Views: 1
  • Screenshot_2020-02-15-10-07-38.jpeg
    41.6 KB · Views: 1
  • Screenshot_2020-02-15-10-14-07.jpeg
    33.8 KB · Views: 2

Jambo baya ni baya tu hata kama kila mtu analifanya au hata kama hakuna wa kulikemea. Huo ukimya wa wachambuzi sio kigezo kabisa cha kwamba kinachofanyika ni sahihi.

Na hoja yako kwamba inafanyika ''kiburudani'' kwahivo hakuna shida ya kuzingatia rangi halisi za klabu zingine binafsi sikubaliani nayo.

Leo hii Coastal Union akicheza na Yanga nayeye aweke logo ya Yanga ikiwa na rangi nyekundu au nyeupe ?
Ndanda aweke blue, Lipuli aweke 'damu ya Mzee' (maroon)
Au hii kiburudani inaishia wapi ?
Nini maana ya logo ya timu kuwa na rangi rasmi kama kila mtu atakua anaweza kuburudika na rangi anazojisikia ?

Kwa muktadha wa uweledi (professionalism) hilo ni kosa kubwa, ila kwa sababu mmeamua kuburudika, ngoja tuwaache.
 
Shukurani Kiongozi. Umejitahidi kuwaelimisha lakini mbumbumbu hawana tiba. Watabaki kama walivyo.
Mpira wote wa Tanzania unaongozwa na watu wa Simba. Ndiyo kiburi cha Haji kwamba ni zamu yao. Hawajaona hilo au wamejua ni upuuzi tu.
Kwa nini wasilalamike Prisons kwa mfano?
 
Waziri Yupo
BMT Wapo
TFF Wapo
Msemaji Wa Wizara Yupo

Natoa Wiki Moja Hatua Zichukuliwe Haraka
Wewe ni nani? Wcha ujuha na umbumbumbu wako! Nendeni makanunue marefa mpate ubingwa achaneni na mambo ya Jirani mapunguani nyie

-
 
Je kununua mechi na marefa hakuwaibishi?

-
 
Sasa ndo umejibu hapo nilivyokuuliza? Maneno mengi kumbe kichwani mweupe... Punguani Waheed
 
Unadhani kuandika gazetini ndo utaeleweka, angalia leo kwenye page ya Yanga kuelekea game ya leo ndo tunachomaanisha..hiyo taarabu peleka kwenu[emoji23]
 
Mkuu asikupasue kichwa huyo mjinga, hajui maana ya Brand wala Tredmark...

Anadhani kila kitu kinawekwa tu bila ya kuwa na sababu maalum, hivi leo Kenya bendera ya Tanzania wanaweza kuitia rangi nyekundu? Halafu Tanzania waseme aaah poa

Sasa baada ya kujibu yeye analeta gazeti ambalo hakuna cha maana alichoandika.
 
Mkuu unajua hapa kuna ambao wanaongea wasichokijua, nimetaka klabu yeyote duniani kwenye page Official ambayo wanafanya hivyo wameshindwa kuleta

Halafu anatokea Nyumbu mmoja anajifanya hili halina neno, ila wale waliochagua logo ya rangi yao ni Wajinga

Hiki ndo sahihi kwa wenye akili..
 
Hivi mambo ya viongozi wa mpira Tanzania kuwa ni watu wa Simba mbona umeshikilia bango hivi? Kama ingekuwa hivyo ungekuwa hapo ulipo kwenye msimamo wa VPL?

Acha kujitoa fahamu mkuu, wewe tunajadili mambo ya soka toka kitambo hapa, huyo anakushika sikio bado hajaelewa mada yetu hapo ubaoni, ana akili finyu

Narudia tena, kwa mfano bendera ya China, nchi ya Tanzania wanaweza kuinakishi kwa rangi ya Kijani, na China wakaridhia? naomba unijibu, tufunge mjadala.
 
Soka letu lina safari ndefu sana kuelekea waliko wenzetu kwa hizi mentality. Haya ni mambo ya kienyeji mno.
 
Sasa ninyi mlipigwa kamoja na Polisi mkataka kufukuza kocha.Sisi tulipigwa tatu bila na bado hatukuwaza yote hayo.Nani anapresha kati yenu na sisi?
Nishakuona wewe ni mweupe kichwani , sitapoteza muda kujibishana na wewe
Ukweli wa mambo unaujua ila hapa unataka kuleta ushabiki maandazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wabadilike,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…