Hivi kwanini klabu ya Yanga inashindwa kuheshimu logo za klabu nyingine?

Hivi kwanini klabu ya Yanga inashindwa kuheshimu logo za klabu nyingine?

Nimeweka fact wewe huna fact unaleta taarabu.
1.Nilianza kwa kukuonesha kuwa man u sasa kwenye logo yaoya 2019/2020 wana rangi nyeusi isiyokolezwa na inatambulikana international.Hukunijibu.
2.nikakuletea mfano wa hapo azam tv ambao pia logo ni ileile lakin wanabadili rangi.Hujanijibu.kwa sababu unajua ila unaweka ubishi usio na manaana kwa sababu yanga wamefanya unataka kuonesha Yanga imefanya kosa.
3.Hivi kwenye ile logo ya nike ikiwekwa rangi nyeusi haitakuwa logo ya nike(mpaka hapo iwekwe nyeupe?

Ukinijibu kwa fact utaweza kunielewa ila kama unakaza kichwa napo sawa.


Unadhani kuandika gazetini ndo utaeleweka, angalia leo kwenye page ya Yanga kuelekea game ya leo ndo tunachomaanisha..hiyo taarabu peleka kwenu[emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yanga rangi zinazokubalika ni njano, kijani na nyeusi, hizo nyingine marufuku, hizo logo za timu nyingine wabadilishe rangi kuendana na matakwa ya yanga.
 
Hivi mambo ya viongozi wa mpira Tanzania kuwa ni watu wa Simba mbona umeshikilia bango hivi? Kama ingekuwa hivyo ungekuwa hapo ulipo kwenye msimamo wa VPL?

Acha kujitoa fahamu mkuu, wewe tunajadili mambo ya soka toka kitambo hapa, huyo anakushika sikio bado hajaelewa mada yetu hapo ubaoni, ana akili finyu

Narudia tena, kwa mfano bendera ya China, nchi ya Tanzania wanaweza kuinakishi kwa rangi ya Kijani, na China wakaridhia? naomba unijibu, tufunge mjadala.
Let us agree not to agree.

Kawapa mfano wa logo ya Azam jinsi inavyoweza kutoka na rangi tofauti tena wakiwa wameitoa Azam wenyewe. Sidhani kama kuna mfano au maelezo bora kuliko hayo.

Kama hili suala ni big deal, bila shaka litaingia kwenye kanuni za kuendesha ligi.

Si mara ya kwanza Vodacom kukubali Yanga ibadili rangi lakini sio logo yenyewe. Tuseme Vodacom hawajitambui? Narudia japo hulipendi kwamba viongozi wa mpira Tanzania ni watu wa Simba. Kama ni tatizo najua watalitolea maamuzi as "usual"

Kiongozi, tuachane na issues za logo. Tuendelee na masuala muhimu ya mpira. Timu au Kampuni itayoathirika kibiashara itaidai Yanga fidia na suala litaishia hapo. Huko Duniani kuna kesi kibao za matumizi ya logo.
 
Tumia akili kufikiri, kisha jenga hoja zenye mantiki, hapajasemwa jezi za Yanga zikae doa jekundu, suala ni logo za timu pinzani zinavyoboreshwa na picha tumeweka hapo

Mnakwama wapi mbona mada ipo wazi?
Hatutaki na kama mnaweza na nyie wekeni logo za wapinzani kwenye ma cover mekundu. Kama hamuwezi kausheni
 
Vile hauelewi mambo ya logo anayosemea mleta mada, hivi ulishawahi kuona chelsea amecheza na Man u[emoji22][emoji22] halafu logo ya man u , ikachalazwa blue tuu
Sisi Yanga siyo Chelsea wala Man U. Kwani ushaona Man U au Chelsea ni mbumbumbu?
 
Mkuu hatuzungumzii kubadilika kwa matokeo ya mechi, tunazungumzia kubadilisha nembo au logo ya timu zingine.
Wao wacheze mpira waifunge Yanga hayo malogo yao yakibadilika hayana madhara sana mana uhalisia wake unajulikana. Hata hivyo ukiondoa Yanga,Azam na mbumbumbu FC timu zingine hazijiendeshi kibiashara. Wacha tu tuchezee logo zao
 
Mimi ni shabiki wa MBEYA City (timu ya nyumbani) na ndio maana nikaweka kiambatanisho hapo juu. Nembo ya timu yetu ninayoijua haina rangi hiyo pichani. Na Nadhani huu ndio msingi wa hoja iliyopo mezani. Je, hili (kuweka nembo timu katika rangi isiyostahiki) lina uhusiano gani na GSM au Vodacom mkuu kama ulivyotuhumu hapo juu ?
Hako katimu kako hakajui masuala ya biashara kupitia nembo yake wewe umetoa wapi hayo mawazo!? Mikia a.k.a mbu×3 bwana!!
 
Sawa, hata kama ni utaratibu ambao umekuwapo kwa miaka na miaka (kwa mujibu wa madai yako) ila ni utaratibu mbovu.
Nimekuambatanishia hapa chini logo sahihi za timu ya Simba, Alliance na Iringa United na zilipostiwa kwenye official instagram page ya hiyo hiyo Yanga. Sijui ni kipi kiliharibika.
View attachment 1358066View attachment 1358065View attachment 1358067
Kwani kipi kiliharibika baada ya hayo mabadiliko? Hata viongozi wa timu hizo hawakulalamika!
 
Kuna wakati lazima tusimame kama wadau wa kandanda nchini, tukiachia mbali ushabiki, ndo maana tulitoa mifano ya rangi ya logo ya Mbeya City na Ruvu Shooting.

Mkuu acha mahaba yasiokuwa na maana, hivi leo Simba SC awe mwenyeji wa mchezo halafu waweke rangi nyekundu logo ya Yanga ni sahihi?
Ungeanza kusimama kukemea tff na marefa kuibeba simba kwanza ndo uongee hili. Siyo rangi Bali mkithubutu kuweka hata doa jekundu tu kwenye logo yetu tutawameza.
 
Hata kama jambo ujui uliza kwanza kuliko kuleta ujinga katikati ya waelewa.
Kwenye Logo kila kitu kinatafsiriwa Kwenye katiba sasa wewe unasemaje rangi hazina maana. Kwa nini msingekua mnaweka rangi nyekundu Kwenye Logo ya Yanga ka rangi hazina maana?
Logo ndo identity ya taasisi. Ndo mana hata mchezaji hua anabusu logo sio jezi

Sent using Jamii Forums mobile app
Anabusu nembo siyo hayo marangi yako
 
Sikiliza kaka.Rangi sio logo.Tafuta matangazo mengi kama 10 hivi ya kampuni tofauti tofauti tofauti.Kisha angalia logo zinafanana kwa kila kitu hasahasa rangi.Jibu ni HAPANA. Nakupa mfano mdogo tu.Logo halisi ya azam tv anayeonesha VPL ni maneno azam ni mekundu kisha neno TV ni rangi blue kisha kuna ile naweza kusema alama ya Tik iliyokama paa la maneno Azam tV ni rangi ya blue pia.

Sasa ukija kwenye baadhi ya situation utaona azam wanatumia logo hii(AZAM TV) ikiwa meupe yote)angalia picha hapa chini.Lakin official logo ni ile yenye maandishi nyekundu na blue.lakin baadhi ya situation utaona logo yote nyeupe.si ajabu pia kuona logo hii ya azam Tv ni nyeusi yote.
Lakin ukweli unabaki kuwa logo ya azam haijabadilika inabaki ileile. Sasa kama kuna kitu bado sijaelewa basi nielimishe kakaView attachment 1358203View attachment 1358204

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbumbumbu asipoelewa hapa basi mwache na umbumbu wake!
 
Pengine mtaelewa
Screenshot_20200215-151853.jpg
 
Katika kueleweshana tu.Bila ushabiki wala mihemuko.

1. Sehemu kuu za logo ni tatu ambazo ni Maneno, alama na rangi, rangi sio ya muhimu zaidi kuliko hivo vingine viwili
2. Si vyema kubadilibadili logo ya kampuni au taasisi (ikiwepo na rangi).
3. Logo itabadilika rangi kutegemeana na background colour ya Tangazo ili logo ionekane vizuri.
4. Ni vema(si lazima) kila kampuni ikawa na logo au nembo katika mwonekano wa rangi tofauti ili kukidhi baadhi ya situation.
5. Ni marufuku kubadili mfumo wa maandishi(Fonts) kwenye logo.Rangi tu inaweza kubadilika(ikiwa kuna ulazima).
6. Ni marufuku kubadili au kuondoa alama yoyote kwenye nembo kwani ndiyo inayotambulisha kampuni au taasisi husika.
Kitu ambacho tunaweza kujiuliza ni kuwa je,designer wa Yanga ana ulazima(kwa mtazamo wake)kubadili rangi za Nembo za wenzake?
Je, Kama rangi ya njano haiivani vizuri na baadhi ya rangi zilizoko kwenye nembo za wengine kwa nini asijaribu rangi zingine kama vile kinani n.k?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je,logo ile iliyoko kwenye jezi ya mbeya city ndo logo ya vodacom,Mbona ni nyeupe?

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu mbona unahamisha magoli, naomba tujikite kwenye logo za timu, hiyo ya mdhamini tuiache kwanza (japokua logo ni logo).
Anyways nakutakia kila la heri kwenye mechi yako ya leo dhidi ya Tanzania Prisons (japokua wanaMbeya tumewatuma vijana warudi na Pointi tatu muhimu).
 
Yanga Ina viongozi wabovu Sana na Simba Ina mashabiki wapumbavu dunia nzima.
 
Back
Top Bottom