Wao wacheze mpira waifunge Yanga hayo malogo yao yakibadilika hayana madhara sana mana uhalisia wake unajulikana. Hata hivyo ukiondoa Yanga,Azam na mbumbumbu FC timu zingine hazijiendeshi kibiashara. Wacha tu tuchezee logo zao
Hako katimu kako hakajui masuala ya biashara kupitia nembo yake wewe umetoa wapi hayo mawazo!? Mikia a.k.a mbu×3 bwana!!
Kwani kipi kiliharibika baada ya hayo mabadiliko? Hata viongozi wa timu hizo hawakulalamika!
unaongea ujinga wa hali ya juu mbele ya magraphic humu jukwaani hakuna kubadili logo husika kwa kitu chochote mvuto wa nini kama unedisign poa jwa nini ikataeKatika kueleweshana tu.Bila ushabiki wala mihemuko.
1. Sehemu kuu za logo ni tatu ambazo ni Maneno,alama na rangi.rangi sio ya muhimu zaidi kuliko hivo vingine viwili
2. Si vyema kubadilibadili logo ya kampuni au taasisi (ikiwepo na rangi).
3. Logo itabadilika rangi kutegemeana na background colour ya Tangazo ili logo ionekane vizuri.
4. Ni vema(si lazima) kila kampuni ikawa na logo au nembo katika mwonekano wa rangi tofauti ili kukidhi baadhi ya situation.
5. Ni marufuku kubadili mfumo wa maandishi(Fonts) kwenye logo.Rangi tu inaweza kubadilika(ikiwa kuna ulazima).
6. Ni marufuku kubadili au kuondoa alama yoyote kwenye nembo kwani ndiyo inayotambulisha kampuni au taasisi husika.
Kitu ambacho tunaweza kujiuliza ni kuwa je,designer wa Yanga ana ulazima(kwa mtazamo wake)kubadili rangi za Nembo za wenzake?
Je, Kama rangi ya njano haiivani vizuri na baadhi ya rangi zilizoko kwenye nembo za wengine kwa nini asijaribu rangi zingine kama vile kinani n.k?
Sent using Jamii Forums mobile app
unaongea ujinga wa hali ya juu mbele ya magraphic humu jukwaani hakuna kubadili logo husika kwa kitu chochote mvuto wa nini kama unedisign poa jwa nini ikatae
Mkuu mbona unahamisha magoli, naomba tujikite kwenye logo za timu, hiyo ya mdhamini tuiache kwanza (japokua logo ni logo).
Anyways nakutakia kila la heri kwenye mechi yako ya leo dhidi ya Tanzania Prisons (japokua wanaMbeya tumewatuma vijana warudi na Pointi tatu muhimu).
Mkuu utaumiza kichwa buree kubishana na yanga timu ambayo haina hata mpiga picha,
Wanasubili azam wapige picha waziweke mtandaoni wao wazichukue waanze kuzicrop na kuzifanyia edit picha za wenzao
Hawana mpiga picha, nenda kaangalie picha za mazoezi wanayofanya moshi wamepiga kwa simu cameraman wao akiwa kindoki [emoji124][emoji124]
Ndio maana nasema yanga wote ni sawa na kenge na nina ushahidi,bisha nije na ushahidiYanga inafuata katiba yake iliyokuwepo toka enzi za mkoloni? unajua kwa nini yanga ilipiga marufuku g rangi nyekundu? sababu ni kwamba enzi za mkoloni wakati yanga inashiriki kwenye harakati za kupigania uhuru, klabu ya simba ikiitwa sunderland walikuwa mstar wa mbele kushirikiana na mkoloni kuwapinga waafrika waliokuwa wanapigania uhuru, simba walikuwa wasaliti na ndio sabab ya rangi nyekundu kupigwa marufuku.
View attachment 1356345
Hii ni nyingine hapa ya Mbeya City FC. Hili kwa kweli halipendezi hata kidogo.
Pengine ni uzembe tu wa ''vijana wao'' wa idara ya habari na mawasiliano hasa wale wanao handle social media accounts zao.
Nmecheka kuona povu linawatoka Yanga Yanga Yanga. Kuna wapuuzi wameenda mbali zaidi eti siipendi Yanga sasa usipoipenda ww mjinga nn kinapungua?
Jitu jinga lipuuzi tu eti siipendi Yanga kwan wao wanakupenda? Achen ushamba wa kujiona ww bora kwa kisichokuhusu
Sent using Jamii Forums mobile app
Naamini Yanga ina viongozi weledi tena wasomi kwa hili walirekebishe mapema maana kama hawataki rangi nyekundu basi wasiwe wanatumia kabisa noti ya elfu kumi (10,000) ambayo ina rangi myekundu inayotumiwa na timu ya Simba.
Kuna watu wanalichukulia suala la logo kama kitu kidogo. Kiukweli logo ni utambulisho wa tasisi fulani na kila taasisi inakuwa imechagua rangi kwa sababu maalum. Kwa hiyo unapobadilisha rangi (corporate colour) kwenye logo ya taasisi husika bila ridhaa yao unakuwa haujaitendea haki hiyo taasisi.
Hebu tuweke ushabiki pembeni kwenye mambo ya msingi, hivi kweli siku ambayo Simba watacheza na Yanga uwanja wa taifa na Simba akawa mwenyeji halafu kwenye matangazo akaweka Simba VS Yanga halafu logo ya Yanga ikawa ipo kwenye rangi nyekundu je Yanga watakubali? Je nchi itakalika? Vipi Yanga wakienda Mbeya kucheza na Mbeya City halafu kwenye matangazo Mbeya City wakaiweka logo ya Yanga kwa rangi nyekundu je Yanga watakaa kimya au watakimbilia TFF? Usichopenda kutendewa usimtendee mwingine maana siku akikutendea utaona unaonewa.
Viongozi wa Yanga hili lipo chini ya uwezo wenu limalizeni mara moja maisha yaendelee kwani watu wanawatazama nyinyi na wala hawatizamwa hawa mashabiki wanaoliunga mkono hapa jamvini.