Hivi kwanini lugha ya kingereza haitiliwi mkazo nchini mwetu?

mtundu27

Member
Joined
Jul 17, 2018
Posts
78
Reaction score
123
Natumai wakristo wanasherekea dominika nyingine katika calender ya shajara huku waislamu nao wakipumzika kusubiria wiki ianze tupambane kutafuta ugali wa familia.
Kuna jambo linasikitisha sana nchi mwetu, na viongozi wetu kwa kujua watanzania wana mawazo duni wanazidi kuwaangamiza kielimu na kiexposure.
Lugha ya kwanza ya kimataifa nchini mwetu haitiliwi mkazo kabisa na awamu hii ndio inaamua kuwapumbaza watu kwa kukazania kiswahili as if tuna mambo ya msingi tunayoyafanya kama nchi.
Shule za awali na msingi, lugha ya kufundishia ni kiswahili lakini unaposogea sekondari hadi vyuo ni 'ngeli', hii inashangaza sana.
Watoto wa viongozi wote wanasoma shule za ukweli na wengi wako nje ya nchi ambapo wanapata exposure ya kutosha, ila huku ndio wanapumbaza watu tu wakomae na kiswahili.
Inafika mahali, hata kuwa na uwezo katika nyanja za kimataifa watz wengi hawawezo kucompete, alafu mijitu bado inashangalia tu 'uzalendo uzalendo'.
Kujua lugha ngeni kunakuexpose na mambo mengi, especially kujua wenzako wanafanya nini, na kunakusaidia kupevuka mawazo na kuwa more creative.
Ila cha kushangaza zaidi, wakitangaza kazi utasikia competency in written and verbal english is a must, sasa kazi wanaziandaa kwa nani?
Mfano mmoja wapo, ni uchaguzi wa ubunge wa afrika mashariki, watu waliokuwa hawajui kingereza vizuri hadi wabunge wanawacheka ila waliokuwa vizuri mfano wa mtoto wa maghembe aliyesoma nje na kufanya kazi huko kwa miaka mingi, alikuwa anateleza tu na kupigiwa makofi kibao kuwa anajua mengi na yuko vizuri.
Sasa kwa mantiki hii, haya mambo ya ccm kudumaza akili za watu na kushangiliwa kwa upuuzi ni kwa manufaa ya nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanangu alisomea English medium akapata matokeo mazuri la 7 serikali wakamchagua secondary ya kata siku alipoanza class wale waliotoka shule za serikali majority hawakujua kuhesabu 1-100 in English! Mwanangu alishangaa sana, akawa darasani anaulizwa sana na wenzake mwalimu ameongelea nini?
Bila jitihada za kumwamisha shule angedumazwa pale kwanza uhaba ni mkubwa sana.
Kiujumla hali ya Elimu nchini ni mbeya sana hususan walimu na mitaala, hivi kwanini shule zote zisiwe kwenye kiwango cha English medium?
Kwa style tuliyo nayo tutaendelea kuajiri na kusimamiwa na wakenya kwa miongo mingi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini tusisome tu kiswahili mpaka mwisho? Kiingereza hakina faida yoyote ile, wanaijeria wanaongea kiingereza, Ghana wanaongea kiingereza lakini kati yao hakuna hata aliepiga hatua ya maana kimaendeleo, kinachosaidia kwenye elimu ni yaliyomo( content) sio lugha inayotumika. Swala la Bunge la afrika mashariki kusaili watu kwa kiingereza wacha wafanye tu. Bunge lile lipo kwa ajili ya diplomasia ni kama balozi wa Tanzania nchi nyingine. Halina athari yoyote kimaamuzi kwa watanzania, kwahiyo wale wanaojua kiingereza waende tu. Ila hapa kwetu mtu asitukanwe kwa kutojua kiingereza, wala asisailiwe kwa kiingereza. Kujua kiingereza hakusaidii uchumi, zaidi kimasaidia diplomasia na mazungumzo ya hapa na pale.
Tukomae tuwe na content nzuri kwenye elimu yetu sio lugha.
 
Sababu Tanzania ni nchi huru kama nchi ya China, Ufaransa, Ujerumani, Sweden nk..
 
Kwanini tusisome tu kiswahili mpaka mwisho? Kiingereza hakina faida yoyote ile, wanaijeria wanaongea kiingereza, Ghana wanaongea kiingereza lakini kati yao hakuna hata aliepiga hatua ya maana kimaendeleo, kinachosaidia kwenye elimu ni yaliyomo( content) sio lugha inayotumika. Swala la Bunge la afrika mashariki kusaili watu kwa kiingereza wacha wafanye tu. Bunge lile lipo kwa ajili ya diplomasia ni kama balozi wa Tanzania nchi nyingine. Halina athari yoyote kimaamuzi kwa watanzania, kwahiyo wale wanaojua kiingereza waende tu. Ila hapa kwetu mtu asitukanwe kwa kutojua kiingereza, wala asisailiwe kwa kiingereza. Kujua kiingereza hakusaidii uchumi, zaidi kimasaidia diplomasia na mazungumzo ya hapa na pale.
Tukomae tuwe na content nzuri kwenye elimu yetu sio lugha.
English ni muhimu na ni silaha kubwa sana kuelekea Mafanikio! Ya mtu kwa dunia hii, mara Ya kwanza kusafiri nje ilikuwa 80's tuliondoka watu 7 ni wawili tu tulioelewa lugha wale wenzangu walinisumbua sana tukifika transit airport, kwenye desk zote za Uhamiaji na kutafuta geti kwa ajili ya flight boarding.. Ilibidi niwafanyie hadi kazi ya kuwaelekeza vilipo vyoo na kuuliza bei za bidhaa! Ilikua shiida
Halafu leo unasema lugha hii haina umuhimu!

Itafsiri hiyo hali uliokutana nayo kama ungekua ni muingereza umekuja Tanzania na wewe tu ndo unajua kiswahili wenzio hawajui Ila wanajua kiingereza, ukifanya hivyo utagundua umuhimu wa kiingereza ni mawasiliano tu kwenye hiyo hadithi yako. Ni kama kiswahili tu. Wewe kimekisaidia nini kiingereza mpaka leo?
 
Kwanini tusisome tu kiswahili mpaka mwisho? Kiingereza hakina faida yoyote ile, wanaijeria wanaongea kiingereza, Ghana wanaongea kiingereza lakini kati yao hakuna hata aliepiga hatua ya maana kimaendeleo, kinachosaidia kwenye elimu ni yaliyomo( content) sio lugha inayotumika. Swala la Bunge la afrika mashariki kusaili watu kwa kiingereza wacha wafanye tu. Bunge lile lipo kwa ajili ya diplomasia ni kama balozi wa Tanzania nchi nyingine. Halina athari yoyote kimaamuzi kwa watanzania, kwahiyo wale wanaojua kiingereza waende tu. Ila hapa kwetu mtu asitukanwe kwa kutojua kiingereza, wala asisailiwe kwa kiingereza. Kujua kiingereza hakusaidii uchumi, zaidi kimasaidia diplomasia na mazungumzo ya hapa na pale.
Tukomae tuwe na content nzuri kwenye elimu yetu sio lugha.
Unaweza ukafuta kauli kwa usalama wako? Unajua kuwa Nigeria ni nchi ya kwanza kiuchumi Africa?
 
Kila raia wa nigeria akishika sh 1 jumla unapata million 190. Wana GDP kubwa kwasababu wapo wengi ila hamna wanachozalisha, we unajua bidhaa ngapi za kinaijeria? Elimu ya kiingereza ingekua inawasaidia tungekua na magari, treni au piki piki za kinaijeria lakini hakuna. Wahindi wanaleta bajaji na kiingereza hawajui. Wanaijeria wapo wengi ndomana GDP yao kubwa.
 
  • Thanks
Reactions: pri
Content ya elimu ndo jambo la msingi, sio lugha. Swali la kujiuliza tulianzaje kusoma kwa kiingereza na tunawezaje kusoma kwa kiswahili?
 
English ni muhimu na ni silaha kubwa sana kuelekea Mafanikio! Ya mtu kwa dunia hii

Kuna kasi kubwa ya watu kujifunza kichina hata kwa nchi za ulaya kwa sasa je tutashika lipi na kuliacha lipi
 
Kila raia wa nigeria akishika sh 1 jumla unapata million 190. Wana GDP kubwa kwasababu wapo wengi ila hamna wanachozalisha, we unajua bidhaa ngapi za kinaijeria? Elimu ya kiingereza ingekua inawasaidia tungekua na magari, treni au piki piki za kinaijeria lakini hakuna. Wahindi wanaleta bajaji na kiingereza hawajui. Wanaijeria wapo wengi ndomana GDP yao kubwa.
Duh!!!!
 
Back
Top Bottom