Hivi kwanini Maboga na mbegu zake mijini ni chakula bora, adhimu na cha gharama, lakini vijijini ni chakula cha mifugo tu?

Hivi kwanini Maboga na mbegu zake mijini ni chakula bora, adhimu na cha gharama, lakini vijijini ni chakula cha mifugo tu?

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
51,453
Reaction score
41,274
Ni nini hasa kinafanya na kupelekea maboga na mbegu zake, yasiwe na thamani wala umuhimu sana vijijini na yawe na thamani sana mijini?

Na vijijini,
ni watu wachache sana hutumia maboga kama chakula, na mbegu za maboga kama miongoni mwa mboga za kula na ugali, mathalani unaweza kuandaliwa ugali, mlenda, mbegu za maboga na maziwa kama chakula cha mchana na kinashuka vizuri sana, sijui huko kwenu.

Una maoni gani kuhusu hili? Ni zipi fursa na faida za mabogo kiuchumi na kiafya?🐒


Mungu Ibariki Tanzania
 

Attachments

  • IMG_20260817_161236.jpg
    IMG_20260817_161236.jpg
    1.4 MB · Views: 8
Mbegu za maboga kwa sasa mijini ni ghali, kamfuko kama cha karanga ni buku, debe ndio usiseme kabisa. Kina mama wanauza kwa wanaume wakisema ni busta. Hapo kale bibi zetu vijijini walitukaangia tule kama kiburudisho na zingine walituanga kupata unga wenye mafuta kuungia mboga na makande
 
Kuna mashine zipo za kukamua mbegu za maboga kupata mafuta, ni mashine za kukamua alizeti. Si maboga tu hadi mbegu za vibuyu na jamii zake matetere na mamung'unya, mbegu jamii za matikiti / mamamari yale matikiti yasiyo na sukari meupe makubwa/magigini mbegu zake nazo hutumika kama mbegu za maboga tu
 
Kwa sasa mbegu za maboga huuzwa sambamba na karanga, kuna mpaka alizeti zilizofungashwa kama karanga. Mteja anachagua atafune nini, karanga, alizeti, korosho au mbegu za maboga
 
Mbegu za maboga zinaongeza sana uzito wa manii kwa wanaume na wingi ndio maana zinaliwa sana maana baada ya kazi nzito za siku nzima mwanaume hutaka apate mahali amwage ubongo wote
Akirejea akanyimwa na ameshakula mbegu za maboga ndio hapo utasikia "amuua mpenzi wake kwa kumnyiga kwa wivu wa mapenzi"
 
Nyumbani wakipiga maboga utasikia leo chakula adimu.
huko town sio?
yaani aise kijijini eti unakuta kifusi cha maboga wameyapasua wametoa mbegu, halafu boga yenyewe wameyatupa wanakula punda wazuriraji au nguruwe wanafugwa for free kabisa 🐒
 
Mbegu za maboga zinasaidia kuusimamisha mnara na kuifanya network ipatikane vizuri sana na kwa urahisi.
Are you sure?
au ni mind and perceptional game tu saikolojikali ili kuwapa matumaini wenye changamoto hizo?

binafsi siwezi kutafuna mbegu za maboga ispokua mamung'unya.

za maboga hua narudisha chenchi kuna kashombo fulani hua sikaelewagi pamoja na kwamba zimekaangwa 🐒
 
Back
Top Bottom