Safi kabisa, swali limejibu swali.Na kwanini wakati wa Kampeni Polisi huwa wala hawaonekani kwa uwingi wao ila Siku ya Uchaguzi na katika Ngome za Wapinzani huwa ni wengi?
Ccm itajuria maisha yote kitendo cha kuondowa siku ya kupiga kura jumapili na kuifanya kuwa jumatano, mtajuta sana.Hivi kwa nini mikutano ya kampeni watu hufurika mno hasa vijana lakini ukienda vituo vya kupiga kura huwaoni.
Yaani huo umati unaouona kwenye kampeni kama wote wangekuwa wanaenda kupiga kura vituo vya kura vingezidiwa.
Lakini hakuna ukienda vituoni unashangaa kukuta wengi ni watu wazima na vituo vingine unakuta saa sita tu mchana hamna watu wameshaisha.
Hiyo mikutano ya kampeni huwa wanafuata nini wakati Siku ya kupiga kura hawaendi.
Natoa uzoefu wangu kama mpiga kura.Na tarehe 28 october na wewe utakuwa shahidi wa haya niliyoandika,Tanzania upande wa vijana kuna matatizo huwa hawaendi kupiga kura wengiUnaharaka gani si usubiri tarehe 28 October ndipo useme hiyo hoja.