Mandi ni aina ya wali unaopikwa na viungo kama biryani ama pilau.
Tuseme ni biryani la kiarabu.
Mie nilijifunza kwa mama mzazi jinsi ya kulipika.
Japo nalo lina namna tofauti tofauti ya upikaji.
-viungo;
Pilipili manga/pilipili mtama,vitunguu maji,vitunguu saumu,zafarani,tangawizi,manjano,karoti,majani yalokauka ya bei,haltiti,mchele na kitoweo chochote eidha kuku,bata,nyama ya kondoo,mbuzi ama ng'ombe.
-Maandalizi menya na uponde vitunguu saumu,menya vitunguu maji kesha kata na karoti na uandae mchele.
Pia kitoweo ulichokipata kioshe kiweke viungo kwa kukichemsha supu kwa kukisagia tangawizi na kukipaka pilipili manga/mtama na kukikatia karoti na kukiwekea majani ya bei/bay,kesha kichemshe supu.Katika uwekaji tangawizi kuna namna ya kuimenya na kuikata tangawizi ikayeyukia katika supu.
Sio kwa kuisagia mpaka kamba zake zikaonekana katika supu,maana supu ndio utapikia huo wali.
-Upishi ukishamaliza kuchemsha supu ya kitoweo ulichopata tafuta sufuria nzuri inayoendana na kilo unazotaka kupika kaanga vitunguu maji,vitungu saumu na karoti, vitunguu maji visiwive kwenda rangi ya brown viishie kwenye rangi ya gold,kesha utose mchele ukaange na hivyo viungo mpaka viingie kwa dakika zisizozidi 5,kesha umwagie haltiti,zafarani,manjano na pilipili manga/mtama ukaange kwa dakika 2-3.Kesha chukua supu na kitoweo chako mwagia kwenye ule mchele pamoja na kitoweo vimix/vichanganye kwa mwiko kesha funika vichemkie.
Una maamuzi eidha supu ikaukie ama isikaukie wali utoke na supu yake,maana kwa wahajemi Mandi huchukulia kuwa ni (rice soup).
Ila kwa wewe waweza ukausubiri ukauke kabisa.
Wakati supu inakaukia waweza weka kwa juu ya wali majani ya bei yanyonywe harufu na wali.
Hivi ndivyo ambavyo mimi hupikaga kwa kuona mama mzazi akipika hivi.