Hivi kwanini mvua isinyeshe kuelekea juu..Badala yake inanyesha kushuka chini?

Nelson nely

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2014
Posts
4,251
Reaction score
2,869
Kwa sababu ninavyofahamu kwa elimu ya shule ya msingi,Mawingu pale yalipo ni mvuke ulioganda,ambao ukijisikia unatoa mvua,tunalima na tunavuna.Sasa je,kwanini mvua ikitaka kunyesha hainyeshi kwenda juu na badala yake inanyesha kuja chini?
 
Ni kwasababu ya kani mvuto kuelekea uso wa dunia (gravitational force) ndio maana kila kitu juu ya uso wa dunia kinavutwa kuelekea uso wa dunia.
Kila kinacho anguka huelekea uso wa dunia. Ni kama nguvu flani ya sumaku inavuta vitu vyote kuja kwenye uso wa dunia.
Ukienda anga ya mbali sana (outer space) ambako hakuna kabisa nguvu hii au ni dhaifu kuliko nguvu ya mvuto kuelekea sayari nyingine basi ukiweka mabarafu au maji kama ya mvua hayatakuja duniani kwenye uso wa dunia.
maji(mvua/mawingu) yatabaki yana elea au yatavutwa kwenda sayari yenye nguvu kubwa zaidi ya mvuto kwenye eneo husika.
 
Mfano mzuri huu hapa. Huko angani kwenye space stations. Hata kuoga ni shughuli pevu. Maji hayatoki kwenye ndoo wala bakuli. Inabidi watumie vitu ambavyo vina suction effect.

Cheki kuanzia dk ya 3:00
 
Ufafanuzi zaidi:
Unajua maji yanapokuwa juu zaidi ya uso wa dunia ambako joto ni dogo sana basi huanza kuganda na kufanya density yake kuwa ndogo kuliko ya hewa iliyopo kwenye uso wa dunia. Maji hayo yakiganda huitwa mawingu ya mvua.
Sasa kwa nmna hiyo kitu chenye density ndogo huelea juu ya kitu chenye density kubwa.

Hali ya hewa inapobadilika na joto kuongezeka yana yeyuka na kuyafanya kuwa kimiminika yaani haya maji unayo yajua ambayo yana density kubwa kuliko hewa ndio yenyewe hushuka chini na hewa kwenda juu yake.

Sasa hiyo density ni uwiano wa tungamo(mass) na volume (ujazo). Hiyo tungamo(au mass) huusiana moja kwa moja na nguvu kani ya mvuto kuelekea kwenye uso wa dunia. na ndio maana pale ambapo nguvu kani hii ni dhaifu au haipo vitu vyote huonekana vyepesi havina uzito(weightless) na huwa vina elea tu haviendi juu wala chini.

Ni ngumu kuelezea sayansi ktk lugha yatu ya kiswahili. natumaini umenielewa kidogo.

UPDATE:
Hewa ikipata joto hutanuka na kuwa na density ndogo hiyo pia huchangia mabarafu yanayo yeyuka kushuka chini na hewa kwenda juu kama vile mvuke wa maji yanayo chemka.
 
Ni kwasababu ya kani mvuto kuelekea uso wa dunia (gravitational force) ndio maana kila kitu juu ya uso wa dunia kinavutwa kuelekea uso wa dunia.
Kila kinacho anguka huelekea uso wa dunia. Ni kama nguvu flani ya sumaku inavuta vitu vyote kuja kwenye uso wa dunia.
Ukienda anga ya mbali sana (outer space) ambako hakuna kabisa nguvu hii au ni dhaifu kuliko nguvu ya mvuto kuelekea sayari nyingine basi ukiweka mabarafu au maji kama ya mvua hayatakuja duniani kwenye uso wa dunia.
maji(mvua/mawingu) yatabaki yana elea au yatavutwa kwenda sayari yenye nguvu kubwa zaidi ya mvuto kwenye eneo husika.
Sasa kwanini mawingu yasivutwe mazima mazima na kani kuja ardhini?mbona yameganda tu pale?
 
Ufafanuzi zaidi:
Unajua maji yanapokuwa juu zaidi ya uso wa dunia ambako joto ni dogo sana basi huanza kuganda na kufanya density yake kuwa ndogo kuliko ya hewa iliyopo kwenye uso wa dunia. Maji hayo yakiganda huitwa mawingu ya mvua.
Sasa kwa nmna hiyo kitu chenye density ndogo huelea juu ya kitu chenye density kubwa.

hali ya hewa inapobadilika na joto kuongezeka yana yeyuka na kuyafanya kuwa kimiminika yaani haya maji unayo yajua ambayo yana density kubwa kuliko hewa ndio yenyewe hushuka chini na hewa kwenda juu yake.

Sasa ni uwiano wa tungamo(mass) na volume (ujazo). Hiyo tungamo(au mass) huusiana moja kwa moja na nguvu kani ya mvuto kuelekea kwenye uso wa dunia. na ndio maana pale ambapo nguvu kani hii ni dhaifu au haipo vitu vyote huonekana vyepesi havina uzito(weightless) na huwa vina elea tu haviendi juu wala chini.

Ni ngumu kuelezea sayansi ktk lugha yatu ya kiswahili. natumaini umenielewa kidogo.
Nimekupata vizuri sana mkuu,shukran.
 
Nimekupata vizuri sana mkuu,shukran.
Nadhani ufafanuzi zaidi umesha jibu swali lako kiasi flani na kilichobakia naendelea hapa chini.
Sasa kwanini mawingu yasivutwe mazima mazima na kani kuja ardhini?mbona yameganda tu pale?
Nimesema sababu density yake ni ndogo na joto linapo ongezeka kule juu basi mawingu (mabarafu) huyeyuka na kuwa na density kubwa kuliko hewa hivyo lazima hewa ilyopo chini yake ipande juu na yenyewe yaende chini.

Hii ndio sababu mvua hainyeshi miezi ambayo joto ni dogo ktk anga au juu ya uso wa dunia. Ukifuatilia mizunguko ya dunia ambayo ni miwili. Dunia kulizunguka jua na dunia kuzunguka yenyewe kwenye muhimili wake. Huo mzunguko wa kwanza ndio huleta majira ya mwaka na kubadilika kwa joto kwenye uso wa dunia.

Hivyo miezi ambayo joto huongezeka (zingatia hii sio jua kuwa kali) ni miezi ambayo mvua hunyesha sababu ndio mawingu huyeyuka.

Daah natamani ningekuwa mwalimu wa fizikia au jiografia lakini ndio hivyo tena sikusoma kabisa jiografia ktk elimu yangu ya upili.
 
Back
Top Bottom