Hivi kwanini mwendokasi huduma zinakuwa mbovu na wao ni monopoly?

Hivi kwanini mwendokasi huduma zinakuwa mbovu na wao ni monopoly?

Extrovert

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2016
Posts
70,785
Reaction score
186,690
Basi moja inabeba watu si chini ya 350 during rush hours. Nauli ndogo ni 750. Per trip ni 262,500 hio ya kuishia Kimara tu. Chukulia basi kumi zifanye mzunguko huo mara 6 kuanzia saa 10 jioni hadi saa 3 usiku.

Roughly 262,500x10x6=15,750,000 hio ni Gerezani - Kimara one way hujahesabia kurudi. Ukiweka nenda rudi manaake unazungumzia 25M.

Kivukoni-Kimara nako upate 15,750,000 one way. Ukiweka nenda rudi maanake unazungumzia 30M kwa traffic ya ferry.

Hapo sijagusa ya mbezi mwisho ambayo ni 400x350=140,000
Ukiweka mabasi 10 yaende 6 trip kila moja ni 140,000x10x6 =8,400,000 hio ni one way Kimara-Mbezi tu during rush hours. Ukiweka 2 way maana yake inaweza gonga 12M.

Sijazungumzia less profitable routes kama Moroco, Muhimbili na Mwenge. Tuchukulie zote combined two ways zilete 23M tu during rush hours.

Twende kwenye hesabu ya jumla sasa.
Kwa masaa 5 tu ya jioni kuanzia saa 10.

Kimara-Gerezani: 25M
Kivukoni-Kimara: 30M
Kimara-Mbezi: 12M
Muhimbili-Morroco-Mwenge: 23M
SUB Totals================90M

Routes asubuhi: 70M
Routes jioni: 90M
TOTAL================160M

EXPENSES
FUEL. 20M
MISC. 5M (25)

NET==================135M

Humo una justify vipi kwamba umeshindwa nunua basi? Hio ni hesabu ya siku tu. Fanya kwa mwezi mzima utagundua kuwa hizo basi zinaweza generate 4.05B ukitoa mishahara ya kulipa staff wote, maintanance na vipuri utagundua the company makes around 2.5 Billions each month on average.

Basi moja la kichina sidhani kama linazidi 300M na hununui kila siku. Kwanini wanashindwa kununua gari hawa jamaa? Hivi wabongo ni nini tunaweza kusimamia wenyewe kikaenda bila ngendembwe? Ni aibu tupu!
 
Mwendokasi kwa sasa umekua usafiri wa mateso ukilinganisha wakati unaanzishwa na madhumuni yake kiujumla.

Umekokotoa vyema na umeshauri vizuri.

Yafuatayo ni ya kuzingatia;
1. Waongeze idadi ya magari
2. Wafanye matengenezo ya magari yao
3. Madereva wao na viongozi wa vituo, wanachotakiwa kufahamu ni kwamba wapo pale kuhudumia wananchi.
4. Uongozi wa juu ubadilishwe(kama hakuna mipango endelevu)
 
Shalom mkuu, kinachokera ni wizi wa kijinga. Huo mpunga unakuta kuna vigogo wanagawana tu na kuua shirika.
Ni kitu gani kinapelekea Huduma za serikali kuwa mbovu
Kuanzia shule, hosptali , usafiri n.k ? Ukiachana na wizi pia angalia na Huduma zao Kuna siku nimependa mwendo Kasi nimefanyiwa unyanyasaji wa kisaikolojia na muhudumu .
 
Halafu zinajaza sana kiasi ambacho mpaka zinatoa utu wetu. Sisi ni binadamu eti lakini ukiwa kwenye mwendokasi utadhani ng'ombe zinasafirishwa. Anyway namshukuru Mungu sipandi tena public transport nalinga na kaIST kangu mjini tena uzuri kana namna E[emoji39]
Ebu elezea vizuri Kuna hoja hapo naiona.
 
Mwendokasi kwa sasa umekua usafiri wa mateso ukilinganisha wakati unaanzishwa na madhumuni yake kiujumla.

Umekokotoa vyema na umeshauri vizuri.

Yafuatayo ni ya kuzingatia;
1. Waongeze idadi ya magari
2. Wafanye matengenezo ya magari yao
3. Madereva wao na viongozi wa vituo, wanachotakiwa kufahamu ni kwamba wapo pale kuhudumia wananchi.
4. Uongozi wa juu ubadilishwe(kama hakuna mipango endelevu)
Inachokera ni ile hali ya mtu kusimama kuanzia saa 10 hadi saa 12 uko foleni gari haziji na njia haina foleni. Wakati kulikuwa na uwezekano after every 10 minutes gari inatoka.
 
Mule wanakula wengi si ajabu kipata halisi kinachowafikia wahusika ni negative.

Vijan wengi wanaokatisha tickets pale ni wapigaji mbwa..wanakuwa na tickets zao binafsi pia..na ni mtandao mkubwa.

We uliona wapi mradi unakabidhiwa unahadi scan machine ila mnaacha kuzitumia mnatumia manual hapo ni chizi tu ndio mnaweza mdanganya kuwa hakuna wizi.
 
Mule wanakula wengi si ajabu kipata halisi kinachowafikia wahusika ni negative.

Vijan wengi wanaokatisha tickets pale ni wapigaji mbwa..wanakuwa na tickets zao binafsi pia..na ni mtandao mkubwa.

We uliona wapi mradi unakabidhiwa unahadi scan machine ila mnaacha kuzitumia mnatumia manual hapo ni chizi tu ndio hatajua kinachoendelea.
Hahahah nilipoona tu wame ditch mfumo wa kadi nikajua tu ilikuwa itafutwa mbinu ya upigaji😀😀😀 kupitia mradi ule kuna vijana watajenga kupitia kukatisha tiketi tu pale 🤣🤣🤣
 
Halafu zinajaza sana kiasi ambacho mpaka zinatoa utu wetu. Sisi ni binadamu eti lakini ukiwa kwenye mwendokasi utadhani ng'ombe zinasafirishwa. Anyway namshukuru Mungu sipandi tena public transport nalinga na kaIST kangu mjini tena uzuri kana namna E[emoji39]
Inatweza utu wetu kabisa wanyonge 🤣
 
Back
Top Bottom