Hivi kwanini mwendokasi huduma zinakuwa mbovu na wao ni monopoly?

Hivi kwanini mwendokasi huduma zinakuwa mbovu na wao ni monopoly?

Kwa maoni yangu, kwa kuwa pesa iliyojenga hizo barabara ni ya umma ilitakiwa kuwe na walau kampuni 2 au 3, za binafsi na zenye viwango, zinazofanya kazi kwa wakati mmoja kwa sababu uwezo wa hizo barabara kuzibeba zote upoo. Hapo kampuni zembe ingejifia yenyewe na kubaki kampuni makini. Kukiwa na kampuni zaidi ya moja ni rahisi hata kuwa na ubunifu mfano kuwa na usafiri express au luxury ili kama mtu anaumwa au hataki kubanana analipa 1000 au 2000 anaenda kwa raha zake. Kuiacha hiyo kampuni moja itambe njia zote hizo matokeo yake ndo hayo ya uzembe na kukera watu kwa sababu wanajua mtapanda tuu.

Tabu yote ya nini hiyo mkuu...

Mamlaka tu ya udhibiti ingeweka masharti magumu na muendeshaji akikiuka anapokwa kazi...
 
Hata wewe ukiwekwa hapo uwezi kusimamia mtu mweusi asome asomavio zaidi ataabulia kuongea kingereza na kuvaa suti kwa me na kwa ke ataabulia kuvaa kimini na mawigi kichwani kubandika kucha za bandia tu habari ya usimamizi tuwaachie weupe
Msile sana
 
[emoji3591] Nitajie mradi mmoja tu wa serikali ambao unaendeshwa kwa weledi na kwenda kama unavyotakiwa.

[emoji3591] Nitajie kitu ambacho sisi Wabongo tulishawahi kuanzisha na kikaenda vizuri.

[emoji3591] Nitajie taasisi au shirika lo lote la serikali ambalo linafanya kazi inavyopaswa. Labda NIDA! [emoji16][emoji16][emoji16]

Nipo nimekaa paleee [emoji117][emoji117][emoji117]

Hakuna…..Na hawana ushindani kwenye kuendesha mradi basi anayeteseka ni mwananchi
 
Inachokera ni ile hali ya mtu kusimama kuanzia saa 10 hadi saa 12 uko foleni gari haziji na njia haina foleni. Wakati kulikuwa na uwezekano after every 10 minutes gari inatoka.
Kati ya vitu vinakera ni kusimama foleni kama tunaomba misaada Kwa wahindi pindi tunasubiria gari
 
mleta uzi nadhani kwa kiasi kikubwa yuko sahihi ingawa sometimes hesabu zinaweza kuwa kazidisha kidogo ila ukweli ni kwamba mradi unaingiza hela na demand ni kubwa wameshindwa kuwa wabunifu kutumia kadi na kuongeza idadi ya mabasi thats it , vinginevyo Bongo ingekua kama mbele tu. Kwa jinsi yanavyojaza na watu kubambiana huwezi kuwa na akili timamu ukaacha gari yako home upande mwendo kasi BIG NO
 
Systematic corruption and colluding to steal are the main challenge of the organisations and others alike.
 
Basi moja inabeba watu si chini ya 350 during rush hours. Nauli ndogo ni 750. Per trip ni 262,500 hio ya kuishia Kimara tu. Chukulia basi kumi zifanye mzunguko huo mara 6 kuanzia saa 10 jioni hadi saa 3 usiku.

Roughly 262,500x10x6=15,750,000 hio ni Gerezani - Kimara one way hujahesabia kurudi. Ukiweka nenda rudi manaake unazungumzia 25M.

Kivukoni-Kimara nako upate 15,750,000 one way. Ukiweka nenda rudi maanake unazungumzia 30M kwa traffic ya ferry.

Hapo sijagusa ya mbezi mwisho ambayo ni 400x350=140,000
Ukiweka mabasi 10 yaende 6 trip kila moja ni 140,000x10x6 =8,400,000 hio ni one way Kimara-Mbezi tu during rush hours. Ukiweka 2 way maana yake inaweza gonga 12M.

Sijazungumzia less profitable routes kama Moroco, Muhimbili na Mwenge. Tuchukulie zote combined two ways zilete 23M tu during rush hours.

Twende kwenye hesabu ya jumla sasa.
Kwa masaa 5 tu ya jioni kuanzia saa 10.

Kimara-Gerezani: 25M
Kivukoni-Kimara: 30M
Kimara-Mbezi: 12M
Muhimbili-Morroco-Mwenge: 23M
SUB Totals================90M

Routes asubuhi: 70M
Routes jioni: 90M
TOTAL================160M

EXPENSES
FUEL. 20M
MISC. 5M (25)

NET==================135M

Humo una justify vipi kwamba umeshindwa nunua basi? Hio ni hesabu ya siku tu. Fanya kwa mwezi mzima utagundua kuwa hizo basi zinaweza generate 4.05B ukitoa mishahara ya kulipa staff wote, maintanance na vipuri utagundua the company makes around 2.5 Billions each month on average.

Basi moja la kichina sidhani kama linazidi 300M na hununui kila siku. Kwanini wanashindwa kununua gari hawa jamaa? Hivi wabongo ni nini tunaweza kusimamia wenyewe kikaenda bila ngendembwe? Ni aibu tupu!
Boss kwenye watu 350 per bus per trip nadhan hesabu haziko sawa hapa. Yale mabasi ni makubwa ndio lakin sidhan kama watafika abiria hao 350.

Kwengine sijaendelea
 
ni kipi ambacho Watanzania tumeweza kukiendesha kwa mafanikio kikawa mfano kwa wengine?..

ukipata jibu la hili swali basi utajua kwanini mwendokasi imetushinda
 
Hizo hesabu ni exaggeration
Kweli too much exaggeration. Haiwezekani ikawa rush hour kutoka Kimara to Gerezani/Ferry at the same time iwe rush hour kutoka Gerezani/Ferry to Kimara.
 
Tabu yote ya nini hiyo mkuu...

Mamlaka tu ya udhibiti ingeweka masharti magumu na muendeshaji akikiuka anapokwa kazi...
Kwa uzoefu wa jinsi tunavyofanya mambo yetu hiyo naona itachukuwa muda sanaa, angalia TTCL Vs makampuni mengine ya simu yanavyokimbiza...
 
Back
Top Bottom