Hivi kwanini Nahreel na Aika hawapati sapoti ya kutosha Bongo ili hali wako na sound ya tofauti kuzidi wasanii wengi wa kwenye A list

Hivi kwanini Nahreel na Aika hawapati sapoti ya kutosha Bongo ili hali wako na sound ya tofauti kuzidi wasanii wengi wa kwenye A list

Nadhani masikio ya watu wengi yanafurahia vitu virahisi, mfano nyimbo za Zuchu na boss wake. Zimekaa kama nursery rhymes na zinahit na kuchuja ndani ya wiki 2. Kusema kweli binafsi zimenishinda kusikiliza lakini za hawa jamaa navy kenzo, unasikia kabisa yaliyomo yamo. Hamna tofauti kubwa na akina Patoranking
Yeah, umeongea vyema mkuu, na wale huwa wanaandika vile makusudi kwasababu wanajua watzedi kwa asilimia kubwa huwa hawapendi vitu vigumu.😅
 
Kwani kwenye A list nani na nani wapo ? Nakumbuka kuna jamaa mmoja alikuwa anamhoji Tunechi akamwambia kuna list ya rapper bora imetoka akasema Jay is on number one, Wayne akasema okay, alafu akasema Drake is on number 3, Wayne akasema that's cool si unajua tena Drizzy is from YMCMB, hakuisema namba mbili sababu alimaanisha Wayne yuko namba 2, sasa ikifika wakati Wayne akauliza, who else is on the list ? Mtangazaji akasema Gucci, Wayne akauliza Eminem ? Mtangazaji akasema Eminem is not on the List, Wayne akacheka alafu akasema "Gucci is on the list and Em is not on the List? Shout out to my nigga Gucci"...
 
Tukiongea ule ukweli kabisa hawana uwezo wanafanya mziki kitajiri , kiufupi hata wanachoimba hakisikiki . Mfumo wa mziki wanaoimba ni nchi kama Jamaica ila jamaa hawana mashairi mazuri labda wakaimbie matajiri na watalii .

Unataka kusema nyimbo gani wameimba hata kiitikio kikabamba ? Kiufupi wanachanganya lugha kama sio watanzania , sikiliza ile nyimbo yao kamatia chini 😀...John makini anapiga hizo za Jamaica sana ila anaelekewa sauti inatoka kabisa ila hao wenzetu hata kiswahili hakieleweki.

Uwezo mdogo , angalia beat aliyoipiga Nahrel kwenye nyimba ya weusi ''gere'' ila bado weusi wameimba wakasikika ndani ya beat yenye nguvu ila wao binafsi na mkewe beat ikiwa juu wanatafuna maneno : Mfano kwenye kamatia chini na ile walioimba na Diamond.
 
Na inaonekana wameridhika na walipo kwa maana wanafanya muziki kama hobby na wala si kama biashara... Inabidi media zianze kuwasema waache hii tabia ili waisaidie nchi kwenye upande huo😅😅😅
Yeah media ziungane hususan kina Baba levo na Mwijaku wawaseme mpaka wajute
 
Mimi huwa niko na kawaida ya kutengeneza playlist tofauti tofauti na kuzisikiliza wakati naendelea na kazi zangu (huwa napata utulivu wa kubaki kwenye jambo moja kwa wakati huo, kwasababu kichwa changu huwa kina shida ya kufungua mafile mengi kwa wakati mmoja hasa kikiwa kwenye utulivu wa kutokupokea mambo mapya kutoka nje, hali hii huwa inanifanya niweze kufanya vitu nusu nusu).

Sasa leo kwenye playlist yangu nimejikuta niko na ngoma kadhaa za hao jamaa wakuitwa navy kenzo, na kilichotokea ni kwamba wakati ngoma inahama kutoka kwa hawa jamaa kwenda kwenye ngoma ya msanii mwingine kuna test tofauti kabisa ambayo inatosha kusema ile ngoma iliyopita haiwezi kuwekwa kwenye mzani sawa na hii iliyoingia kutokana na ubora wa sound yake.

Yaani kuanzia kwenye midundo hadi mixing, na uimbaji wao na midundo ni kama imefungana kiasi cha kuleta test fulani ya tofauti yaani ile test ya ki-Grammy Grammy kabisa.

Kila siku tumekua tukistruggle juu ya wasanii wetu kupenya kwenye soko la kimataifa ili hali tobo la kutupeleka huko ni kama lipo wazi kabisa ila ni vile tu hatujaamua, kwa mfano "Nahreel on the beat" ingekua inaskika kwenye ngoma nyingi za wasanii wetu wanaopambana kwenda kimataifa nadhani wangefika wanapotaka kutokana na sound ya jamaa jinsi ilivyo(au nimefika mbali sana😅).

Anyway, unahisi ni nini shida inayopelekea hawa jamaa wakose support kwa mtaa, ukiachana na sababu ya kuyajenga maisha yao kwenye engo ngumu ya kutokufungamana na mambo mengi ya kijamii ikiwemo ya kisiasa (sijui kama wameshawahi kwenda Dodoma kiuoto wa asili hawa), au sound yao iko mbele ya muda sana?.
Uwezo ni mdogo wale tu pesa , ukileta uzungu bongo unaangukia mbavu .
 
Back
Top Bottom