Hivi kwanini Nahreel na Aika hawapati sapoti ya kutosha Bongo ili hali wako na sound ya tofauti kuzidi wasanii wengi wa kwenye A list

Hivi kwanini Nahreel na Aika hawapati sapoti ya kutosha Bongo ili hali wako na sound ya tofauti kuzidi wasanii wengi wa kwenye A list

Haiwezekani iwe watu wengi wapende kitu kibaya na waache kitu kizuri
Wanaozipenda ni watoto 😃 the songs are catchy. Come on bwana...
Chapati.. cha pa ti
Kwi kwi kwi kwiii nitaliaaa
Sukari nampatia sugar sukari
Unataka kuniambia kuna watu wazima wanafurahia?😂
 
Wanaozipenda ni watoto 😃 the songs are catchy. Come on bwana...
Chapati.. cha pa ti
Kwi kwi kwi kwiii nitaliaaa
Sukari nampatia sugar sukari
Unataka kuniambia kuna watu wazima wanafurahia?😂
Sasa hizo unazosema ni za watoto mbona ndio zina idadi kubwa ya streams kwenye platforms zote.
Sasa hao watoto wanasikiliza nyimbo boomplay,audiomack,YouTube na Spotify kuliko watu wazima?
 
Chuma ni 🔥 🔥 🔥
Screenshot_20250222-001053_1.jpg
 
Muziki wa bongo kizunguzungu sana, imagine singeli ndio inataka kufanywa utambulisho wa muziki ya taifa
Sema singeli iko na kitu hasa hii ya sasa ambayo waimbaji wanaandika vyakueleweka, midundo yake iko na vibe fulani hivi, ukiwa na maadali unaweza kukaza ile kikaksi ila huwezi kuipotezea ile vibe yake.
 
Sasa hizo unazosema ni za watoto mbona ndio zina idadi kubwa ya streams kwenye platforms zote.
Sasa hao watoto wanasikiliza nyimbo boomplay,audiomack,YouTube na Spotify kuliko watu wazima?
Hahahaa...ndugu mdau, hizo nyimbo zinautofauti gani na nyimbo za watoto mf. ukuti ukuti wa mnazi wa mnzai. Ni aina ambayo kabisa Bi Zuhura anaweza kuimba ikahit wiki 1 tukasahau. There's nothing special or memorable about the music they make. It lacks dimension. Haiwezi kukufanya ukawa nostalgic kama baadhi ya nyimbo nyingine

Kuhusu views nyingi, hiyo sio hoja. Ni mambo ya usasa..nyimbo nyingi mpya za sasa zinaangaliwa kwenye hizo streaming platforms kuliko za zamani au watu wenye following ambazo si kubwa
 
Mimi huwa niko na kawaida ya kutengeneza playlist tofauti tofauti na kuzisikiliza wakati naendelea na kazi zangu (huwa napata utulivu wa kubaki kwenye jambo moja kwa wakati huo, kwasababu kichwa changu huwa kina shida ya kufungua mafile mengi kwa wakati mmoja hasa kikiwa kwenye utulivu wa kutokupokea mambo mapya kutoka nje, hali hii huwa inanifanya niweze kufanya vitu nusu nusu).

Sasa leo kwenye playlist yangu nimejikuta niko na ngoma kadhaa za hao jamaa wakuitwa navy kenzo, na kilichotokea ni kwamba wakati ngoma inahama kutoka kwa hawa jamaa kwenda kwenye ngoma ya msanii mwingine kuna test tofauti kabisa ambayo inatosha kusema ile ngoma iliyopita haiwezi kuwekwa kwenye mzani sawa na hii iliyoingia kutokana na ubora wa sound yake.

Yaani kuanzia kwenye midundo hadi mixing, na uimbaji wao na midundo ni kama imefungana kiasi cha kuleta test fulani ya tofauti yaani ile test ya ki-Grammy Grammy kabisa.

Kila siku tumekua tukistruggle juu ya wasanii wetu kupenya kwenye soko la kimataifa ili hali tobo la kutupeleka huko ni kama lipo wazi kabisa ila ni vile tu hatujaamua, kwa mfano "Nahreel on the beat" ingekua inaskika kwenye ngoma nyingi za wasanii wetu wanaopambana kwenda kimataifa nadhani wangefika wanapotaka kutokana na sound ya jamaa jinsi ilivyo(au nimefika mbali sana😅).

Anyway, unahisi ni nini shida inayopelekea hawa jamaa wakose support kwa mtaa, ukiachana na sababu ya kuyajenga maisha yao kwenye engo ngumu ya kutokufungamana na mambo mengi ya kijamii ikiwemo ya kisiasa (sijui kama wameshawahi kwenda Dodoma kiuoto wa asili hawa), au sound yao iko mbele ya muda sana?.
Hata wao wenyewe hawatulii na muziki. Labda ndiyo shida ya kufanya muziki ndani ya uhusiano wa kimapenzi.

Wakitibuana ratiba zinasimama hadi waweke mambo sawa. Ndiyo maana wanawaka na kuzima mara kwa mara.

Hata Pa One ilipotea kwa mapenzi ya hawa wawili.

Ova
 
Tukiongea ule ukweli kabisa hawana uwezo wanafanya mziki kitajiri , kiufupi hata wanachoimba hakisikiki . Mfumo wa mziki wanaoimba ni nchi kama Jamaica ila jamaa hawana mashairi mazuri labda wakaimbie matajiri na watalii .

Unataka kusema nyimbo gani wameimba hata kiitikio kikabamba ? Kiufupi wanachanganya lugha kama sio watanzania , sikiliza ile nyimbo yao kamatia chini 😀...John makini anapiga hizo za Jamaica sana ila anaelekewa sauti inatoka kabisa ila hao wenzetu hata kiswahili hakieleweki.

Uwezo mdogo , angalia beat aliyoipiga Nahrel kwenye nyimba ya weusi ''gere'' ila bado weusi wameimba wakasikika ndani ya beat yenye nguvu ila wao binafsi na mkewe beat ikiwa juu wanatafuna maneno : Mfano kwenye kamatia chini na ile walioimba na Diamond.
Duh hapo nasikiliza Usinibwage nasikia kila kitu hadi back vocals.
 
Hata wao wenyewe hawatulii na muziki. Labda ndiyo shida ya kufanya muziki ndani ya uhusiano wa kimapenzi.

Wakitibuana ratiba zinasimama hadi waweke mambo sawa. Ndiyo maana wanawaka na kuzima mara kwa mara.

Hata Pa One ilipotea kwa mapenzi ya hawa wawili.

Ova
Nahisi hilo kundi combination yao haikuwa perfect sana, wakibaki wawili yeye na mkewe inanoga zaidi kuliko walivyokua na wale jamaa
 
Hizo ni points za kujibia mtihani , huo ndio ukweli , nyimbo za Navy kenzo ni kama za bob junior za miaka ile ...Mziki nje ya production ni kipaji basi wakina Master j na Majani wangekuwa wasanii.

Abigal ana mbwembwe kama zako ila mziki hamna kitu ,mziki ni talent zilikuwepo kabla ya kuja hayo maandishi yenu...Navy kenzo hawajui kiufupi .

Kiufupi hawajui kuimba wanatumia vyanzo ili kuimba mziki kama Marehemu Mr.Ebo na nyimbo zake zile hazieleweki kwa vile alikuwq na studio.
Kuna kitu unajaribu kushindana nacho na hutakuja kufanikiwa hata siku moja. Kujaribu kumuelewa na kufuatilia kila aina ya mziki ukiwa na lengo la kutafuta ukuburudishe.

Simuelewi Khadija Kopa anachoimba na Taarabu kiujumla ila haimaanishi ni mziki mbaya na msanii mbaya pia.

Pale Wasafi wana msanii anaitwa D Voice mimi simuelewi ila naamini ana fanbase yake.

Kuna rapa Marekani aliwahi sema "This shit is not for everybody.".

Don't try to be everybody, utakosoa hata pazuri.
 
Unacho kiona wewe kizuri haimanishi kilamtu anaona hivyo...
Uzuri wa kitu au mtu upo machoni au masikioni mwa mtu...
Kwahio usilazimishe mwingine aone au asikie unavyohisi wewe...
 
Itakua issue n mitonyo tu.. wasanii wa kibongo kumlipa producer hua mbinde.
. .. Joh Makin alipotea mara tu baada ya Nahreal kuacha kumpigia midundo n issue inasemekana ilikua mitonyo
 
Back
Top Bottom