Ukitaka kujua ukweli kuhusu 'kuhasimiana' kwa NCCR-Mageuzi na CHADEMA rejea mambo kadhaa katika historia ya vyama hivi. Kwa machache ninayoweza kuwahabarisha hapa ni kwamba;
- Waasisi wa chadema ni miongoni mwa watu wa awali kabisa waliohusika na uanzishwaji wa NCCR wakati huo ikiwa kamati kabla ya kugeuka kuwa chama cha siasa pale mfumo wa vyama vingi uliporejeshwa nchini. habari kutoka ndani kabisa ya makundi haya zinasema kwamba, maneno demokrasia na maendeleo yalikuwa kaulimbiu ya awali kabisa ya NCCR, na hadi leo maneno hayo yanaonekana katika logo ya chama hicho. Ilitokea wakati fulani kwamba Mzee Mtei aliishauri kamati ya NCCR iitwe Chama cha Demokrasia na Maendeleo kwa kutumia ile kaulimbiu, lakini ushauri wake haukutumika badala yake akalitumia hilo wazo kuanzisha chama kipya pembeni, yaani CHADEMA ya leo.
- Waasisi wangine wa NCCR ambao leo ni watu muhimu sana katika CHADEMA, mf.Prof Baregu, waliondoka NCCR baada ya Mrema na Marando kukipasua chama katikati.Waliondoka hapo wakiiona NCCR kama jahazi linaloelekea kuzama, kutozama kabisa kwa NCCR nadhani ni kwa mshangao wao hadi leo.
- Kuna kundi kubwa la wanachama wa CHADEMA ambao waliondoka NCCR kutokana na kutoelewana na Mwenyekiti wa sasa wa chama hiki, J.Mbatia.Orodha ya hawa ni ndefu, kuanzia kwa marehemu, Chacha Wangwe, Komu na wengineo. Mkitaka kujua hili mwulizeni aliyehama hivi karibuni, Mhe.Selasini Mbunge mpya wa Rombo. Wote hawa matarajio yao ni anguko kubwa la NCCR, lakini ajabu bado inadunda japo kwa kuchechemea.
- Mbatia na Mbowe hawaivi kihivyo, hasa hasa kwa sababu Mbatia alimpinga hadharani Mbowe wakati akiwania Ubunge kule Hai mwaka 2000, ambapo (huenda kwa sabau hiyo)Mbowe hakufanikiwa
- Kifo cha Wangwe ndio kiliharibu zaidi, hata yale makubaliano ya ushirikiano yaliyosainiwa kati ya vyama hivi (pamoja na CUF na TLP)yakafa.
- Vijineno vingi vya kutotakiana heri vimekuwa vikiendelea kati ya vyama hivi. Mfano wakati Zitto aliwambia wakazi wa Tanga kwamba NCCR imekufa, Sungura wa NCCR aliibatiza CHADEMA aka ya Chagga Development Manifesto. CHADEMA nao hivi karibuni wamejibu, ati NCCR sasa ni NCCR-Manunuzi!
Kwa maoni yangu wote ni watafuta tonge lile lile, hakuna anayetaka kuona mwenzake kapata yeye kakosa.