Elections 2010 Hivi kwanini NCCR, TLP hawapatani na CHADEMA?

mwambie huyo tanzania kwanza mbona analysis yake imekomalia uchaga ameacha cuf km kweli na cuf pia wachaga aseme.. Ila kwa kifupi naona km hana hoja ya msingi

cuf wao wanaambiwa chama chao ni cha wapemba!!! Mada hapa inamhusu mrema, mbowe na mbatia (mmm) wote hao ni wenyeviti wa vyama vikuu vya upinzani, na ningeshauri hawa wavuliwe uenyekiti kwa mfano, mwenyekiti wa chadema awe slaa, wa tlp atoke musoma na nccr atoke kigoma hapo ndipo itanoga lakini kuwaachia viongozi wote waandamizi watoke kilimanjaro! Hisia za uchagga hazitakoma!!!
 
wenyeviti wa chadema, tlp na nccr wote ni wachagga lakini hawapatani kwasababu wanatoka sehemu tofauti kama mrema ni mmrangu, mbatia ni mkibosho na mbowe ni mmachame na kiasili makabila haya huwa hayaivi ktk chungu kimoja!!!

Yaani hamwezi kuargue bila kuingiza kabila la mtu? mkuu unaonaje ukienda nje ya nyumba yako? I mean think big outside your borders!
 
Ndugu wapigania nchi,msiipuuze hoja ya Tanzania Kwanza . As Great Thinkers should not leave any stone un-turned. Jinsi nzuri ya kuwaelimisha watanzania kuwa hiyo si kweli ni kwa kuonyesha. You prove something to be wrong by showing what is right (Counter-Example).

Suala si kuwa CHADEMA ni ya Wachaga au la, ila kwa baadhi ya watanzania,wapiga kura wanaamini hivyo. Wameaminishwa hivyo makusudi ili tushindwe. Tutafutie dawa hili.

 
kwani mikoa mingine huwawezi wakaanzisha vyama??? mi nadhani pia tukubali ukweli kuwa uenyekiti haupewi kwa umkoa wako au ukabila wako hilo kwa Tanzania halipo ila kuna watu wasiopenda kuona upinzani unakua na kuchukua madaraka ndio chanzo kikubwa cha yote haya wapinzani kuto kuelewana, mfano uliundwa umoja wa upinzani vizuri tuu, pale ndio ilikuwa tunazika uongozi wa upande mmoja kabisa. kila mtu anajua nini kilitokea baada ya hapo kifo cha kijasusi cha wangwe kikatokea ndo kilisambalatisha muungano ule bado tuu hatujaelewa sababu ya wapinzani kuto kuelewana ?? NAJARIBU KUJENGA PICHA KAMA MUUNGANO ULE UNGEKUWEPO MPAKA UCHAGUZI HUU TUNGEKUWA NA HISTORIA MPYA KABISA SASA LAKINI WOTE TULIINGIA KWENYE MTEGO WA MASHUSHU WA SISIEM WALIOPO UPINZANIA NA TUKANASA SASA TUNAANZA KUTAFUTANA WENYEWE KWA WENYEWE.
 
Wengi ni makachero wa CCM kama unavyojua upinzania hapa Tanzania aliuanzisha Mwl. Nyerere ilikuwa tu kuwafurahisha au kuwapumbaza wahisani ambao waliweka shinikizo.. Hivyo mtu kama Mrema alikuwa CCM atatoka na kwenda uanzisha upinzani japo CCM walimgeuka..

Akatoka akaenda TLP ambapo uko hadi leo ila unaona hana jipya kwani umaarufu umepungua na pia ameshindwa kuendeleza chama na mwisho ni majungu ya ndani na pia ubabe..

Mbati na NCCR Mageuzi yeye nadhani tu kitu ameshindwa ni hali ngumu ya kiuchumi japo angalau mwaka huu amefanikiwa kupata angalau 4.. hiii ni changamoto kwake kujipanga vizuri na kuweka sera zake vizuri...

CUF kilionekana na kinaonekana zaidi kama chama cha waislam ndiyo maana hata sehemu walizopata ni za asili ya Uislamu zaid.. japo nakiri kusema kuwa kiongozi wao Lipumba ni kichwa na hazina kubwa ya Taifa. Kama tungekuwa na serikali ya mseto huyu jamaa wizara ya fedha ingemuhusu..

Chadema tangu mwanzo ni wapinzani wa ukweli japo waasisi wake hawakuweza kukifikisha mbali pamoja na mambo yaliyozuka kuwa ni chama cha wachagga. Ila ukiangalia viongozi wengi walikuwa siyo wachanga zaidi ya Mzee Mtei aliyekuwa mwenyekiti. ila wengine akina makani, marando siyo hata wachanga. Ila nadhani kwa mwaka 2015 lazima nguvu ziongezwe hata kule kwenye zile sehemu ambazo waliibiwa.

Kule walikoshinda waendeleze sera zao za maendeleo kusudi watu wawakubali na kuamishia sehemu nyingine ambazo bado..

2015 Mtu kama mrema atakuwa amekwisha kabisa kisiasa, hivyo nadhani Lipumba ataungana na wenzie kusimamia chama.
 
Hawa ni CCM B hivyo wanaisaidia CCM kuipunguza nguvu Chadema.
 
Hivi hata kama ungekuwa ni wewe ,unaona mazingira ya kuhesabiwa kura haukuwa wazi ukawaeleza NEC na kweli wakakubali kuwa walichanganya baadhi ya majimbo kama GEITA na Nyang'wale ..je kuna majimbo mangapi yaliyochakachuliwa kama hivyo?Slaa sio mnafiki na hawezi kuwa mnafiki hata siku moja palipo na ukweli atausema maramoja,na hata angejiunga nao maana yake angekuwa amewasaliti wannchi wengi waliomwamini hivyo kwa kuzingatia mengi aliona ni bora tu kutohudhuria hizo sherehe za mafisadi..
 
HII KWA KWELI IMEBIDI NIIPRINT ILI NIWE NAISOMA SOMA kwa maana UKITAKA KUUKATAA ukweli lazima uwe na UONGO wenye uzito KANUSHI.:smile-big: embu subiri tuone na wengine wanalisemeaje hilo.

AHSANTE SANA WARIDI, KWA kuitoa elimu hiyo. (maana wapinzani wote nawaona ni "mwaga mboga nimwage ugali) sasa sijui nafuu iko wapi:A S angry:
 
na wengine ni ndumilakuwili.....chadema imewashtukia
Umeniwahi binti mrembo weweee!! HIYO NDIYO TOFAUTI KUBWA, tlp na nccr wao wanaonekana kama ni vibaraka wa kuvuruga upinzani wakati chadema ni wana mapinduzi halisi na wazalendo wa kweli wenye uchungu ni nchi.
 
Wivu tu unawasumbua wakiangalia walikuwa wote level moja au zaidi yao, na leo wao wako juu kuliko wao meaning wanapata popularity sana kuliko wao lazima wachukie, uzuri haya mambo huwa yanategemea kwa binadamu.
 

Mbowe alimaanisha kwa mwaka 2005!
 
Kakwambia nani mbatia ni mkibosho? we nawe acha kukurupuka Mbatia ni mwenyeji wa kirua bana acha kutulisha matango pori.
 
Kulikoni hapo jameni? Mbatia analia na Chadema!! Mzee wa Nji hii nae vivyo hivyo!! Hivi kwanini na wote wako jahazi moja?? kuna siri gani iliyo sirini hapo???:thinking:

Ni kwa sababu wenyeviti wao wote ni WACHAGA! full stop. Waarabu wapemba wajuana kwa viremba. Kila mtu ni mjuaji ati!!!.
 
Wivuuu tu vyama vyao vimedumaa kwa hiyo wanaona bora wakose wote
 

Mwaka huu Chadema waliamini kwa nyomi iliyokua ikihudhuria kampeni basi wangeshinda Urais, ndio maana wakasusia kwani hawakuamini kilichotokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…