Hivi kwanini Nyerere aliidhinisha kunyongwa Mwamwindi?

Hivi kwanini Nyerere aliidhinisha kunyongwa Mwamwindi?

basi kifungo chepesi kwani ni hasira za ghafla ila alichokiri mahakamani ni shida . Ila hakimu hana vifungu vinavyomlinda kulingana na maamuzi ya busara ? Yanayoelezwa kama ni kweli Mwambungu alidhalilishwa vya kutosha
 
Nyerere, Kleruu na Mwamwindi, wote ni marehemu. Wapumzike kwa amani huko walipo. Labda tuangalie hawa waliotaka kumuua Lisu hawatanyongwa wakija kugundulika?
 
Ilikuwa ni lazima Nyerere asaini ili kuweka precedence juu ya wananchi kujichukulia sheria mkononi dhid ya viongoz


Ila Mwamindi ni shujaa
 
Umeshawahi kujiuliza labda inawezekana intelijensia ya Mwalimu ilionyesha kwamba kwa kitendo alichokifanya huyu bwana Mwamwindi labda nyuma yake kulikuwa na kundi la watu ambao walimpa support na ilikuwa ianze huko Iringa kisha ienee kote nchini kushinikiza jambo fulani lifanyike hivyo ikabidi immediately adhabu kali itolewe ili kutoa onyo kwa wale wengine waliotaka kujaribu?

Historical hili tukio limetokea miaka ile bado ndo kwanza tunajaribu kujitawala so inawezekana ni mapepe tu ya viongozi kujaribu kutuma ujumbe kwa wabaya {waliowahisi} ili kuwatisha zaidi!
 
unakijua unachokiuliza au unataka kumegewa kila kitu
nyuma ya utawala wa Nyerere ulishazaliwa au ulikuwa Msingi?
unamkumbuka yule mhindi aliyekuwa anaweka BIMA za magari na kuwauwa wateja hadi na mkewe
tafuta mwenyewe .............
mm nipo Dodoma lkn tafuta vyanzo mwenyewe
Mambo ya mahakani, mbinu, (Technical). Za kisheria uhusika katika kushinda, au kushindwa kesi.

Kwahiyo siyo ajabu aliekua ameshinda, sio ajabu kushindwa kwenye rufaa, ama alishindwa akashinda.
 
Umeshawahi kujiuliza labda inawezekana intelijensia ya Mwalimu ilionyesha kwamba kwa kitendo alichokifanya huyu bwana Mwamwindi labda nyuma yake kulikuwa na kundi la watu ambao walimpa support na ilikuwa ianze huko Iringa kisha ienee kote nchini kushinikiza jambo fulani lifanyike hivyo ikabidi immediately adhabu kali itolewe ili kutoa onyo kwa wale wengine waliotaka kujaribu?

Historical hili tukio limetokea miaka ile bado ndo kwanza tunajaribu kujitawala so inawezekana ni mapepe tu ya viongozi kujaribu kutuma ujumbe kwa wabaya {waliowahisi} ili kuwatisha zaidi!
Inawezekana ikawa hivyo lakini kuna watu wanasema vilianza visa kwanza ambapo Dr Kleruu alikua anatumia nafasi yake kumdhalilisha Mwamwindi
 
Kuna mengine utokea sababu ya fundisho kwa wengine.Kipindi cha ujamaa kulikua na chuki kati ya viongozi na wananchi wenye uwezo.Kitendo cha kuuliwa RC kingeachwa bila onyo kali kingeweza kua mwanzo wa mauaji mfululizo ya viongozi.Pale ni kwamba Serikali ilionyesha mamlaka yake .
Well explained.
 
basi kifungo chepesi kwani ni hasira za ghafla ila alichokiri mahakamani ni shida . Ila hakimu hana vifungu vinavyomlinda kulingana na maamuzi ya busara ? Yanayoelezwa kama ni kweli Mwambungu alidhalilishwa vya kutosha
Hivi hakimu, aneamua kwa kuzingatia busara, badala ya ushahidi uliopo mbele ya mahakama huyo hafai.
Mawazo yako tofauti inavyotekelezwa, kila kosa hukumu linamuongozo wa hukumu yake, labda kama hakimu asietenda haki tu, ndiye hazingatii haya.
 
Inawezekana ikawa hivyo lakini kuna watu wanasema vilianza visa kwanza ambapo Dr Kleruu alikua anatumia nafasi yake kumdhalilisha Mwamwindi
Sasa kwa hivi mkuu tunakosa hints za kumuingiza raisi ktk hili sakata.maana kama ulivyosema miaka ile kwa sehemu kubwa ilikuwa inatumika intelijensia kuyajua mambo kama haya hivyo inawezekana Mwalimu alipelekewa arifa ikisema tofauti na jinsi tunavyosikia kwenye simulizi mbali mbali kuhusu hii issue ndo maana akachukua maamuzi yale.
 
Mi nadhani nyerere hizo zingine labda halikua hazipi sign yake sababu sometime ilikua inakua ni mauwaji ya watu ambao hawafahamiki wala alie ua sio mtu anae fahamika,,,,hivo walikua hawatengenezi attention yoyote kwa taifa ambayo ingeweza kuwa positive au negative,,,,hivo mauaji ya aina hiyo wengi wao walifungwa kifungo cha maisha..

Lakn tukio hili la kuuwawa kwa mkuu wa mkoa bwana Kleruu tena kuuawa na tajiri mkubwa,,wote wanafahamika sana nchi nzima...hivo hilo jambo hilo lilitengeneza attention kubwa sana ndani na nje ya nchi huki kila mtu akisubiri kuona ni hukumu gani itafikiwa,,,

Lakn pia alie uliwa ni kiongozi mkubwa,,,,,nyerere angeteneza kitu kibaya sana kwa viongozi kutokuheshimiwa na kutokuogopwa japo hata kidogk kama angetoa hukumu nyepesi kwa huyu alie muua kiongozi.

Yote tisa kumi.......yawezekana pia ni mahakama yenyewe ndio ulio fikia huo kuafaka wa jamaa kunyongwa bila nyerere kuchangia lolote kimawazo juu ya hukumu hiyo
Hili ndilo jibu.
 
Wewe, Doble Standards ipo, sana maekani, Kule utakavyochuliwa wewe mweusi sivyo atakavyochukuliwa Mzungu.

Hivi unakumbuka kisa cha yule mtoto, wa kiafrica aliyenyongwa George Stanney, hebu fuatilia huko, utaona jela za huko uone weusi walivyowengi magerezani.

Hata hii adhabu ya kunyongwa inawahusu sana watu weusi, kuliko weupe.
Hizi nchi ziliondelea watu waziangalii mabaya yake, bali huziangalia kwa mazuri yake tu.

Sasa mfano wewe, kunyongwa kwa Mwamindi tu, mnaona alionewa wakati aliua kweli, kama wewe unasimamia haki, sheria insemaje unapoonewa hata kwa makusudi.

Inasema uuwe, na mahakama iamua kwa kutumia busara, jamani sheria haifanyi kazi kwa vikra zenu, bali sheria hufuata sheria.
Mkuu unanikumbusha kesi inayoendelea sasa hivi ya Cintoiya Brown. Hakuna system iliyoovyo ktk utoaji haki kama marekani pale inapomhusisha mweusi.

Darren Wolf kaua watu zaidi ya Tisa kanisani hajauawa..

.Michael Brown kaiba vitu supermarket tu wamemuua

Yule mwanafunzi kaua wenzake shuleni hakuuliwa on the spot lakini mtoto alishika toy gun mwingine alishika simu wakamuua hapo hapo mifano ni mingi
 
Mie bubafsi siioni hoja ya kutuletea humu jf tujadili kwa sababu za msingi zifuatazo;
1. Anaposema nyerere alisaini hukumu ya kifo cha mwamwindi haraka.
- mtoa maada anaposema haraka, ana taarifa Ni siku ngapi Nyerere alisaini toka pale alipohukumiwa. Na anafikiri ingesainiwa siku ngapi baada ya hukumu kutolewa?
- je mtoa maada anajua kipindi ambacho Ni lazima Raisi awe amesaini hukumu ya kifo baada ya hukumu kutoka mahakamani?
- je mtoa maada ana taarifa za wengine ambao raisi aliwahisha au kuchelewesha kusaini hati zao za hukumu za kifo.
Swali kwa mtoa maada!
- Nyerere alisaini hukumu ya mwamwindi ya kifo baada ya siku ngapi tangu kuhukumiwa ili ilinganishwe kama iliwahishwa au kucheleweshwa!
- Mwamwindi alinyingwa siku ngapi baada ya Nyerere kusaini hati yake ya hukumu ili tujilidhishe kuwa aliwahisha!
Mwisho; Nahisi Mtoa maada hana ushahidi na uthibitisho kwa aliyoyaandika!
Raisi na Idara zilizokuwa chini yake zina utaratibu wake wa kufanya kazi.
ASISIKIE STORI ZA VIJIWENI AMBAZO MARA NYINGINE HAZINA UKWELI.
Yaani hiki kizazi bado sana, nimefanya kautafiti kadogo, nimegundua asilimia kubwa (88) ya wana jamiiforums hawajui utofauti uliopo kati ya maada na mada.
 
Kiuhalisia kama Nyerere asingechukua maamuzi kama yale ama angechelewa ingewa-discourage RCs na watendaji wengine so ilikuwa kama kuwatia moyo tu kwamba niko na nyinyi.
 
Back
Top Bottom