Hivi kwanini Nyerere aliidhinisha kunyongwa Mwamwindi?

Sibishi kwamba alipatikana na hatia kama alivyokiri mwenyewe na hukumu aliyopata ni stahili yake. Hoja ni kwamba kwanini Nerere asi sign za wengine waliouwa kwa ukatili mkubwa na akaidhinisha Mwamwindi anyongwe haraka?
nadhani ungetoa mifano ya hao wengine amabao hakusaini hati zao itasaidia kuwaelewesha watu
 
*MNYALUKOLO SAID MWAMWINDI ALIMUUA RC DR. KLERUU SIKU YA KRISMASI HUKO IRINGA!!!*

Leo tarehe 25/12/2018, siku ya Krismasi, ni miaka 47 imepita toka Mnyalukolo, SAID ABDALLAH SIULANGA MWAMWINDI, ammimimie risasi na kumuua aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Iringa, marehemu Dr. WILBERT KLERUU. Mauaji hayo yaliyokea tarehe 25/12/1971 kijijini Mkungugu, Isimani, Iringa.

Dr. WILBERT KLERUU alikuwa ni mzaliwa wa Mwika, Kilimanjaro ambaye alikuwa ni mmoja wa Watanzania wachache wakati huo waliokuwa na shahada ya uzamivu(PHD) ya uchumi wa kijamaa.

Dr. KLERUU alikuwa ni kipenzi cha Baba wa Taifa, Mwalimu JK NYERERE, kutokana na weledi na utendaji wake usio na mfano. Mwanazuoni mwa mwaka 1971, DR.
.KLERUU alikuwaamehamishiwa mkoani Iringa kutokea Mtwara.

Dr. KLERUU alikuwa ni kiongozi machachari sana na ilikuwa kawaida kwake na alikuwa hana hiana kuwafokea hadharani watumishi wa umma wazembe. Kwa hakika, Dr. KLERUU alikuwa mbabe sana. Akiwa Iringa, kuna wakati gari yake ilipigwa "overtake" na gari hilo lililompiga"-overtake" likamziba kwa mbele. Kufumba na kufumbua, Dr. KLERUU alishuka kama komandoo na kwenda kumuwasha vibao dreva wa gari hilo! Dr. KLERUU, mara kwa mara, alipenda kuwafokea watu kwa kuwaambia *"Hamnijui Mimi? Kawaulizeni watu wa Mtwara"* na yeye hakuwa mtu wa kukaa ofisini kama viongozi wengi wa wakati huo, bali alijumuika na wananchi na kufanya nao shughuli za maendeleo bega kwa bega ambapo ilikuwa ni kawaida kwake kushika jembe kwa masaa kadhaa bila kula!.

Kipindi hicho kulikuwa na kampeni kubwa ya kuwafanya wananchi walime mashamba ya pamoja na hivyo wakulima waliokuwa na mashamba makubwa walinyang'anywa, kitendo ambacho hakikuwapendeza Wanyalukolo waliokuwa matajiri wenye mashamba makubwa ya mahindi.

Dr. KLERUU alihamishiwa Iringa ili akatekeleze mpango huo wa serikali na alipofika tu akatangaza kwamba mashamba yote binafsi yanapaswa kuwa ya ujamaa kufikia Novemba 1971.

Bw. MWAMWINDI alihamia eneo la Mkungugu, Isimani mwaka 1954 akitokea Iringa mjini alikokuwa dreva. Alianza kilimo kidogo kidogo hatimaye akawa na mashamba makubwa ya mahindi ya hekari takriban 160. Akawa analima mashamba yake kwa trekta katika eneo hilo ambalo awali lilikuwa ni pori. Kipindi hicho, hakukuwa na sehemu Tanzania iliyokuwa ikizalisha mahindi mengi kama Isimani.

Jumamosi ya tarehe 24/12/1971, Dr. KLERUU alitembelea mashamba mbalimbali maeneo ya Tarafani, Igulu na Ndolela kuhamasisha kilimo cha pamoja. Kesho yake, Jumapili ya tarehe 25/12/1971, Dr. KLERUU( ambaye hakuwa na Jumapili wala skukuu) aliendelea na shughuli hizo za kutembelea mashamba ya wakulima.

Muda wa saa 11 jioni, Dr. KLERUU alifika kwenye shamba la MWAMWINDI na kumkuta akilima kwa trekta lake. Pamoja nae kulikuwa na mtoto wake(Mohamed) na watu wawili aliowaajiri( Yadi Chaula na Charles Mwamalata), Bw. Joseph Kusava ambaye ni mkwe wake pamoja na wake zake waliokuwa wakishirikiana nae kulima siku hiyo. Dr. KLERUU alifika shambani hapo akiendesha gari lake binafsi aina ya Peugeot 404 rangi ya bluu na ubavuni ikiwa imeandikwa RC-Iringa. Baada ya kushuka alimfuata moja kwa moja MWAMWINDI na kuanza kumuhoji maswali mengi kwanini hataki mashamba yake yawe ya ujamaa. Akamwambia *"Unafanya nini hapo?"Shuka shenzi we"*. MWAMWINDI akamuuliza *"kwanini unanitukana?"* Dr. KLERUU akamjibu *"Funga mdomo wako, n'ge n'ge n'ge nini? Kwanini nawaambia hamsikii? Blood fool"*. Katika eneo hilo walikuwa wao wawili tu kwani watu wengine walikuwa mbali kidogo. Dr. KLERUU aliyekuwa na kawaida ya kutembea na kifimbo kidogo akakitumia kumchomachoma nacho MWAMWINDI.

MWAMWINDI akafura sana hivyo akaanza kwenda ndani kupitia eneo la makaburi ya baba yake na ndugu wengine huku Dr. KLERUU akimfuata na alipoyaona makaburi akasema *"Tazama unaendelea kujenga nyumba za kudumu"*. MWAMWINDI akamjibu *"Hizi sio nyumba, ni mahali ninapozika ndugu zangu"*. Dr. KLERUU akajibu *"Ni mahali unapozikia mirija wenzio, mbwa we!"*.

Mnyalukolo MWAMWINDI akawaamehamaki sana. Akasema *"Swela"*, akaingia ndani akachukua gobore akatoka nalo nje na kumfyatulia risasi Dr. KLERUU ambaye alianguka na kufariki hapohapo!!! MWAMWINDI aliuchukua mwili wake akauweka kwenye buti ya gari ya Mkuu huyo wa Mkoa, akachukua na kofia ya Pama ya Mkuu wa Mkoa akaivaa yeye na kuanza safari ya kilometa 40 kwenda Iringa mjini.

Mjini Iringa, watu walishangaa kuona gari ya Mkuu wa mkoa inapita upande wa kulia kwa vile mtaa wa Jamatini ulikuwa ni "One way" lakini wakahisi huenda Mkuu wa mkoa ana dharura. Saa 1 jioni, MWAMWINDI akafika kituo kikuu cha polisi akaenda moja kwa moja kaunta akamkuta PC MBETA KASONDA na kukwambia *"Ebu nenda kwenye buti ukaitoe mbwa yenu nimeishaiua"* na kumkabidhi bunduki pamoja na funguo za gari. PC KASONDA hakuamini macho yake alipouona mwili wa Dr. KLERUU ukiwa umetapakaa damu. Dr. KLERUU alikuwa amevaa ovaroli nyeusi na miwani. Hivyo, mara moja PC KASONDA akamuweka MWAMWINDI chini ya ulinzi. Mtu mwingine aliyekuwepo kituoni hapo ni mzee DAVID BUTITINI(ambaye alikuwa askari polisi na baadaye kada wa CCM Iringa). Tarumbeta likapulizwa na askari wakakusanyika na kupewa rasmi taarifa ya kifo hicho cha Mkuu wao wa mkoa na gari lake likahifadhiwa nyuma ya kituo cha polisi. Askari wanne wakaenda kuleta kitanda cha magurudumu toka hospitali na hatimaye mwili wa Dr. KLERUU ukapelekwa "mortuary". Kesho yake, siku ya jumatatu, mji mzima wa Iringa uligubikwa na simanzi kubwa.

Kuna kundi la watu ambao walikuwa wakimchukia sana Dr. KLERUU kutokana na aina ya uongozi wake hivyo lilipopata tu taarifa za kifo chake wakanunua makreti ya bia usiku huohuo na kuanza kunywa kwa kushangilia hadharani! Msako ulipoanza usiku huohuo, jamaa hao walikuwa wa kwanza kukamatwa!.

Mzee BUTININI ambaye pia alikuwa Mtwara wakati DR. KLERUU alipokuwa Mkuu wa Mkoa, anakiri kuwa ni kweli DR. KLERUU alikuwa mtu wa shoka- *"Ni kweli hata kule Mtwara alionekana mtemi sana mwenye kuhimiza mambo kwa nguvu. Lakini lazma muelewe maeneo ya Mtwara yalikuwa ya vita na tulikuwa tukiwasaidia ndugu zetu wa Frelimo hivyo kule kulihitaji mtu kama DR. KLERUU. Mtwara DR. KLERUU hakukumbana na upinzani ila Iringa hali ilikuwa tofauti. Kwa mawazo yangu, Dr. KLERUU alipaswa kwanza kujifunza juu ya mila na desturi za watu wa Iringa. Maana watu wa Iringa ni watu wa Iringa tu."*

Mauaji hayo ya Dr. KLERUU yalimsikitisha sana Mwalimu NYERERE, wakuu wa mikoa na wananchi mbalimbambali. Lilikuwa ni tukio lililoongelewa nchi nzima. Majirani na wazee wengi waliokuwa wakilima pamoja na MWAMWINDI walisombwa na vyombo cha usalama na kumwekea ndani kuisaidia polisi ambapo walikuwa wakikamatwa na kusafirishwa usiku kwa ndege za jeshi. Takribani watu 30 walikamatwa wakiwemo wazee maarufu kama IBRAHIM KHALILI, PESAMBIL, MURSALI na wengineo na kupelekwa sehemu mbalimbali za nchi mf Shinyanga, Mwanza na Zanzibar. Cha kusikitisha ni kwamba ndugu zao hawakujua wamepelekwa wapi! Aidha, nyumbani kwa MWAMWINDI huko Mkungugu kukawa kunalindwa na askari wa FFU muda wote.

Kitendo cha kukamatwa majirani na marafiki wa MWAMWINDI kilileta uhasama mkubwa baina ya ndugu wa majirani hao na familia ya MWAMWINDI.

Ikabidi mwanae (AMANI MWAMWINDI)(21) alazimike kutafuta kibali cha DC Iringa kwenda gereza la Dodoma alikokuwa anashikiliwa MWAMWINDI. Alipoganikiwa kukipata alikwenda na akamueleza hali hiyo ambayo ilimsukitisha sana Mzee MWAMWINDI. AMANI akamshauri baba yake aandike barua kwa Rais NYERERE, nae akafanya hivyo siku hiyohiyo. Katika barua hiyo, MWAMWINDI alimueleza Mwalimu kwamba yeye ndiye aliyemuua Dr. KLERUU hivyo wengine hawahusiki hivyo waachiwe. Baada ya kupita siku kadhaa, wazee hao majirani wakaachiwa na kurejea kijijini hapo, Isimani. Hata hivyo, tafrani hiyo iliyokuwaimewakumba ikafanya wengi wahame eneo hilo kwani waliishaona "togwa limeingia nzi"!.

Upelelezi wa mauaji hayo ulienda haraka na MWAMWINDI akafunguliwa kesi ya mauaji ya kukusudia Mahakama kuu. Kesi ilipoanza kusikilizwa, ilivuta hisia za watu wengi na umati wa watu uliokuwa ukitamalaki kila siku mahakamani ulikuwa "si wa nchi hii!.

Tarehe 2/10/1972, baada ya mashahidi wa pande zote kutoa ushahidi wao akiwemo RPC wa Iringa (Abubakar Hassan) aliyetoa ushahidi upande wa MWAMWINDI kwamba hakuwa na taarifa kwamba Mkuu huyo wa Mkoa angetembelea eneo hilo ndio maana hakumpa "Police escort", Jaji GABRIEL CHIKE ONYIUKE toka Nigeria(aliyehudumu Tanzania toka 1970-1973) alimtia MWAMWINDI hatiani na kumuhukumu kunyongwa hadi afe. Hii ilikuwa ni baada ya kuukataa utetezi wake kwamba alitenda kosa hilo baada ya kurukwa na akili na pia alikasirishwa "provoked" na marehemu, Mh. Jaji aliona kwamba ingawa ni kweli MNYALUKOLO wa kawaida huwa si mtu wa mchezo-mchezo anapodhihakiwa hasa mbele za wake zake lakini kitendo cha MWAMWINDI cha kwenda ndani kufuata bunduki kilionesha, pasina shaka, kwamba aliua kwa kudhamiria.

Adhabu hiyo ya kifo ilitekelezwa mara moja kwani Mwalimu NYERERE alisaini hati ya kifo cha MWAMWINDI
. Hayo hiyo, ilikuwa ni moja ya hati tatu za vifo zilizosainiwa na Mwalimu NYERERE kuidhinisha kunyongwa kwa binadamu katika uongozi wake wa miaka 24 katika taifa hili.

Kesi hii ilikuwa ya aina yake na haikuchukua hata mwaka mmoja toka tukio kutokea na adhabu kutolewa tofauti na kesi nyingine za mauaji ambazo, kwa kawaida, huchukua miaka mingi kabla ya hukumu kutolewa. Kesi hii ilichukua miezi kumi tu.

Baada ya msiba, familia ya DR. KLERUU ilirudi Kilimanjaro. Hata hivyo, Mwalimu NYERERE na KARUME na baadae ABDU JUMBE walikuwa karibu sana na mjane wa DR. KLERUU na wakawasomesha wanawe nchini Urusi na Bulgaria. Aidha, viongozi wengine waliwatia moyo na kuwafariji sana mf. Marehemu Mzee RASHID KAWAWA na mama GETRUDE MONGELA. Dr. KLERUU aliacha watoto wanne ambao ni Eva, Andrew, Carmen na Edwin.

Mwezi Machi 2014, familia ya DR. KLERUU na ya MWAMWINDI zilikutana kwa furaha ili kusameheana kwa tukio hilo. Bi. EVA KLERUU(60) ambaye ni mtoto mkubwa wa Dr. KLERUU na Bw. AMAN MWAMWINDI(67) (aliyekuwa Meya wa mji wa Iringa) walifanya jambo hilo la kihistoria na hivyo kuyaishi kivitendo maandiko ya vitabu vitakatifu yatutakayo wanadamu kusameheana. Picha hii chini inawaonesha wawili hao wakiwa na bashasha baada ya tendo hilo la kihistoria na lisilo la kawaida.

Mnara wa DR. KLERUU umejengwa kwenye "mji" wa MWAMWINDI mahali ambapo alipigwa risasi . Nyumba ya Mkuu wa Mkoa DR. KLERUU bado ipo. Picha hizi hapa chini zinamuonesha Mnyalukolo MWAMWINDI baada ya kujisalimisha polisi pamoja na nyumba ya DR. KLERUU.

REST IN PEACE:

1. Dr. W. KLERUU
2. S. A. MWAMWINDI
 
inasemekana kuwa mwamwindi alikuwa mkaidi sana wa amri ya kulima shamba la kijiji ,,mwamwindi alikuwa na trekta ,nini logic yake alikataa amri kubwa sana kipindi hicho,kipindi cha vijiji vya ujamaa wewe ukijenga mbali ilikubidi ubomoe nyumba yako na usogee karibu na kijiji ukikaidi unawekwa PINGU.
 
Kwanza nikiri kiumri sikuwepo wakati suala la mwamindi linatokea, ila nimeisoma hii kesi yote (Judicial Proceeding), Pia nimefika Iringa na kupata masimulizi ya hili suala kwa wenyeji, pia nilisoma makala moja ya Mjengwa juu ya 'mashuhuda': Mtazamo wangu

-Dr alikuwa mtu mwenye majivuno na dharau sana kwa anaowaongoza, yasadikika alienda mbali hadi 'kuingilia familia za watu'. Hivyo kiuongozi huyu bwana alikuwa na makosa sana.

-kisheria huyu Mwamwindi alikuwa na makosa kabisa hivyo kimahakama ilikuwa sahihi kuhukumiwa adhabu ya kunyongwa.

-Kunyongwa.

Ticha alipata shida sana kutoa uamuzi huu, sababu kuu moja. Alijua fika Dr alikuwa na matatizo na ndiye mchokozi.

Lakini angeacha kumnyonga, angewaweka kwenye mazingira magumu sana kiutendaji ma RC wengine na vitendo vya Kina mwamwindi vingehalalishwa kwa wananchi wengine.

Hivyo ili watumishi waendelee kufanya kazi kwa amani ilibidi tu Ticha amtie kitanzi Mwamindi.
 
Said mamwindi ni kweli aliua. Alimuua Dr Wilbert Kileruu hilo aliilikiri mwenyewe Mamwindi mahakamani. Ila kwa jinsi mtiririko wa kesi Ile ulivyokua, mamwindi Angeweza kukwepa kitanzi kile, likaja swala la usalama wa viongozi. Hilo ndilo lililopekea Kileruu akala kitanzi. Kwamba ilionekana endapo Mamwindi angepewa adhabu nyepesi basi kuua viongozi ingekua mchezo wa mazoea. Hivyobasi kulinda usalama wa viongozi ikabidi itolewe adhabu kali ili liwe funzo na pia kuzui kosa lile kujirudiarudia kwa viongozi wengine.
 
Sibishi kwamba alipatikana na hatia kama alivyokiri mwenyewe na hukumu aliyopata ni stahili yake. Hoja ni kwamba kwanini Nerere asi sign za wengine waliouwa kwa ukatili mkubwa na akaidhinisha Mwamwindi anyongwe haraka?
Nafikiri wewe nimejibu vizuri sana na kwa kifupi wengine wote wataleta siasa
 
Said mamwindi ni kweli aliua. Alimuua Dr Wilbert Kileruu hilo aliilikiri mwenyewe Mamwindi mahakamani. Ila kwa jinsi mtiririko wa kesi Ile ulivyokua, mamwindi Angeweza kukwepa kitanzi kile, likaja swala la usalama wa viongozi. Hilo ndilo lililopekea Kileruu akala kitanzi. Kwamba ilionekana endapo Mamwindi angepewa adhabu nyepesi basi kuua viongozi ingekua mchezo wa mazoea. Hivyobasi kulinda usalama wa viongozi ikabidi itolewe adhabu kali ili liwe funzo na pia kuzui kosa lile kujirudiarudia kwa viongozi wengine.
Nakubaliana nawe mkuu, inawezekana ikawa kama usemavyo
 
Kwanza nikiri kiumri sikuwepo wakati suala la mwamindi linatokea, ila nimeisoma hii kesi yote (Judicial Proceeding), Pia nimefika Iringa na kupata masimulizi ya hili suala kwa wenyeji, pia nilisoma makala moja ya Mjengwa juu ya 'mashuhuda': Mtazamo wangu

-Dr alikuwa mtu mwenye majivuno na dharau sana kwa anaowaongoza, yasadikika alienda mbali hadi 'kuingilia familia za watu'. Hivyo kiuongozi huyu bwana alikuwa na makosa sana.

-kisheria huyu Mwamwindi alikuwa na makosa kabisa hivyo kimahakama ilikuwa sahihi kuhukumiwa adhabu ya kunyongwa.

-Kunyongwa.

Ticha alipata shida sana kutoa uamuzi huu, sababu kuu moja. Alijua fika Dr alikuwa na matatizo na ndiye mchokozi.

Lakini angeacha kumnyonga, angewaweka kwenye mazingira magumu sana kiutendaji ma RC wengine na vitendo vya Kina mwamwindi vingehalalishwa kwa wananchi wengine.

Hivyo ili watumishi waendelee kufanya kazi kwa amani ilibidi tu Ticha amtie kitanzi Mwamindi.
Umechambua vizuri tena kwa muhtasari mkuu kile kinachoweza kuwa chanzo halisi cha maafa yaliyomkuta RC Kleruu

Inasemekana kesi hii ilichukua miezi kumi tu toka kukamatwa hadi kuhukumiwa Mkulima Mwamwindi, katika kesi za mauaji uzoefu unaonyesha kwamba hii ni kati ya kesi iliyoendeshwa na kuamuliwa kwa haraka na pengine hata utekelezaji wa uhukumu ulifanyika haraka
 
Adhabu hiyo ya kifo ilitekelezwa mara moja kwani Mwalimu NYERERE alisaini hati ya kifo cha MWAMWINDI
. Hayo hiyo, ilikuwa ni moja ya hati tatu za vifo zilizosainiwa na Mwalimu NYERERE kuidhinisha kunyongwa kwa binadamu katika uongozi wake wa miaka 24 katika taifa hili.

Kesi hii ilikuwa ya aina yake na haikuchukua hata mwaka mmoja toka tukio kutokea na adhabu kutolewa tofauti na kesi nyingine za mauaji ambazo, kwa kawaida, huchukua miaka mingi kabla ya hukumu kutolewa. Kesi hii ilichukua miezi kumi tu
Asante sana mkuu, hoja kubwa ya uzi huu upo katika point zako hizi hapo juu kiongozi wangu. Mashtaka na kesi nzima na hata utekelezwaji wa adhabu ilipekwa kwa supersonic speed ambayo haijazoeleka kwa taratibu za kimahakama hasa kwa kesi za aina hiyo

Though nawaelewa na pia nakubali waliotoa hoja kwamba Mwalim Nyerere alitaka ku set precedence ya kua tough kwa watu watakao jaribu kuwadhuru wateule wake
 
Sibishi kwamba alipatikana na hatia kama alivyokiri mwenyewe na hukumu aliyopata ni stahili yake. Hoja ni kwamba kwanini Nerere asi sign za wengine waliouwa kwa ukatili mkubwa na akaidhinisha Mwamwindi anyongwe haraka?
umri na mihemko ya ujana wa kiongozi wa nchi wakati huo inawezekana ulichangia pia kwa kuwa rais alitumia zaidi akili kuliko busara na umri ulikuwa unaruhusu hivyo. lingekuwa ni tukio la miaka ya 90 asingefanya hivyo.
 
Tunaambiwa katika kipindi chake chote cha cha miaka 23 kama Rais wa Tanzania Mwalimu Nyerere alisaini hati chache sana za kunyongwa watu waliopatikana na makosa mahakamani na kupewa adhabu ya kifo. Miongoni mwa hati za kunyongwa alizowahi kuziidhinisha ni ile ya aliyekua mkulima mkubwa wa enzi hizo mkoani Iringa Bwana Saidi Mwamwindi aliyeshtakiwa kwa kosa la kumuua aliyekua Mkuu wa Mkoa wa Iringa wakati huo Dr Kleruu

Kama umewahi kupitia hati za mashtaka, mwenendo wa kesi na maelezo ya hukumu ya watu waliopatikana na makosa ya kuua kwa kukusudia utagundua kwamba wengi wao walitekeleza mauaji hayo kwa ukatili sana wengine ukijiuliza hawa kweli walikua ni binaadamu wenye roho!? Pengine haitakupata huruma kwa hukumu inayopitishwa juu yao

Said Mwamwindi ni kweli aliua, na wala hakuisumbua mahakama kwani alikiri hivyo mwenyewe na akahukumiwa kunyongwa hadi kufa. Ila kuna simulizi nyiingi sana zinanazohusiana na mauaji aliyofanya na hata baadhi ya watu wanahalalisha kitendo alichofanya na kukiita cha kishujaa!

Wengi ya wanaomuana kua ni shujaa wanasema RC Kleruu alikuachanzo cha mauaji yake mwenyewe. Alikua kweli anamnyanya sana huyu Bwana Mwamwindi. Kwanza alikua anatoka kimapenzi na mkewe halafu alikua anamfatafata sana na kumtolea lugha za kashfa(abusive languages). Kibinadamu hiyo ni dharau na ni adhabu kubwa sana kumpa mwanaume mwenzio hasa kama umemzidi kwa cheo au hata pesa

Kwa intelijensia aliyokua nayo Mwalimu Nyerere lazima atakua alijua chanzo halisi cha Mkulima Mwamwindi kumpiga risasi RC Kleruu., na ingawa mazingira yaliyomfanya atende kosa lile yalikua hayampi nafuu yoyote kisheria linapokuja suala la adhabu kwa maoni yangu hati ya kunyongwa Said Mwamwindi haikupaswa kusainiwa harakaharaka hasa ikiwa inajulikana (angalau kwa uwazi) kua Nyerere hakupenda adhabu ya kifo

Nawauliza wakongwe waliopo JF wenye kujua vizuri historia ya tukio hili na yaliyotokana na jambo hilo, haraka ya Nyerere kusaini hati ya kunyongwa hadi kufa Said Mwamwindi ilitokana na;

1. Hasira za Nyerere kuuliwa RC wake?

2. Mauwaji aliyofanya Mwamwindi yalikua ni ya kikatili kuliko wauwaji wengine walioua kwa kukusudia?

3. Chuki za Nyerere kwa aliowaita Makabaila(wamiliki wa mashamba makubwa) ambapo Mwa
mwindi anaangukia hapo?

4. Double standards wanazokua nazo wanasiasa wengi hasa wa kiafrika katika kuwatendea
watu wao?

Naomba kuelimishwa wakuu
Nadhani teacher alikuaga over_rated
 
Bwana kurunzi picha ziko wapi sasa

Back
Top Bottom