Hivi kwanini Nyerere aliidhinisha kunyongwa Mwamwindi?

basi kifungo chepesi kwani ni hasira za ghafla ila alichokiri mahakamani ni shida . Ila hakimu hana vifungu vinavyomlinda kulingana na maamuzi ya busara ? Yanayoelezwa kama ni kweli Mwambungu alidhalilishwa vya kutosha
 
Nyerere, Kleruu na Mwamwindi, wote ni marehemu. Wapumzike kwa amani huko walipo. Labda tuangalie hawa waliotaka kumuua Lisu hawatanyongwa wakija kugundulika?
 
Ilikuwa ni lazima Nyerere asaini ili kuweka precedence juu ya wananchi kujichukulia sheria mkononi dhid ya viongoz


Ila Mwamindi ni shujaa
 
Umeshawahi kujiuliza labda inawezekana intelijensia ya Mwalimu ilionyesha kwamba kwa kitendo alichokifanya huyu bwana Mwamwindi labda nyuma yake kulikuwa na kundi la watu ambao walimpa support na ilikuwa ianze huko Iringa kisha ienee kote nchini kushinikiza jambo fulani lifanyike hivyo ikabidi immediately adhabu kali itolewe ili kutoa onyo kwa wale wengine waliotaka kujaribu?

Historical hili tukio limetokea miaka ile bado ndo kwanza tunajaribu kujitawala so inawezekana ni mapepe tu ya viongozi kujaribu kutuma ujumbe kwa wabaya {waliowahisi} ili kuwatisha zaidi!
 
Mambo ya mahakani, mbinu, (Technical). Za kisheria uhusika katika kushinda, au kushindwa kesi.

Kwahiyo siyo ajabu aliekua ameshinda, sio ajabu kushindwa kwenye rufaa, ama alishindwa akashinda.
 
Inawezekana ikawa hivyo lakini kuna watu wanasema vilianza visa kwanza ambapo Dr Kleruu alikua anatumia nafasi yake kumdhalilisha Mwamwindi
 
Well explained.
 
basi kifungo chepesi kwani ni hasira za ghafla ila alichokiri mahakamani ni shida . Ila hakimu hana vifungu vinavyomlinda kulingana na maamuzi ya busara ? Yanayoelezwa kama ni kweli Mwambungu alidhalilishwa vya kutosha
Hivi hakimu, aneamua kwa kuzingatia busara, badala ya ushahidi uliopo mbele ya mahakama huyo hafai.
Mawazo yako tofauti inavyotekelezwa, kila kosa hukumu linamuongozo wa hukumu yake, labda kama hakimu asietenda haki tu, ndiye hazingatii haya.
 
Inawezekana ikawa hivyo lakini kuna watu wanasema vilianza visa kwanza ambapo Dr Kleruu alikua anatumia nafasi yake kumdhalilisha Mwamwindi
Sasa kwa hivi mkuu tunakosa hints za kumuingiza raisi ktk hili sakata.maana kama ulivyosema miaka ile kwa sehemu kubwa ilikuwa inatumika intelijensia kuyajua mambo kama haya hivyo inawezekana Mwalimu alipelekewa arifa ikisema tofauti na jinsi tunavyosikia kwenye simulizi mbali mbali kuhusu hii issue ndo maana akachukua maamuzi yale.
 
Hili ndilo jibu.
 
Hapana Nyerere alilazimika kuchukua uamuzi huo mgumu ili kuwalinda Ma Rc wengine ni sababu hiyo tu !
 
Mkuu unanikumbusha kesi inayoendelea sasa hivi ya Cintoiya Brown. Hakuna system iliyoovyo ktk utoaji haki kama marekani pale inapomhusisha mweusi.

Darren Wolf kaua watu zaidi ya Tisa kanisani hajauawa..

.Michael Brown kaiba vitu supermarket tu wamemuua

Yule mwanafunzi kaua wenzake shuleni hakuuliwa on the spot lakini mtoto alishika toy gun mwingine alishika simu wakamuua hapo hapo mifano ni mingi
 
Yaani hiki kizazi bado sana, nimefanya kautafiti kadogo, nimegundua asilimia kubwa (88) ya wana jamiiforums hawajui utofauti uliopo kati ya maada na mada.
 
Kiuhalisia kama Nyerere asingechukua maamuzi kama yale ama angechelewa ingewa-discourage RCs na watendaji wengine so ilikuwa kama kuwatia moyo tu kwamba niko na nyinyi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…