Hivi kwanini taasisi nyeti inayoongoza nchi inadanganya wananchi wake?

Hivi kwanini taasisi nyeti inayoongoza nchi inadanganya wananchi wake?

J93

Member
Joined
Jun 20, 2016
Posts
55
Reaction score
159
Ikumbukwe Mei mosi ilivyofanyika siku ya wafanyakazi mkoani Arusha, ambapo ilitangazwa Mgeni rasmi angekuwa Rais Samia, ila haikuwa hivyo na wala haikutangazwa wazi sababu za yeye kutokuhudhuria, ila baadae ilielezwa alikuwa nchi nyingine kutekeleza majukumu yake!

Kauli mbiu ya siku ile ilibeba zaidi kile wanachohitaji wafanyakazi, hasa ongezeko la mshahara, ambapo makamu wa Rais aliyemwakilisha Rais alitoa kauli nzito kuwa tudubiri Rais kutoa kauli juu ongezeko na uboreshaji wa maslahi ya wafanyakazi mapema kabisa mara baada ya shughuli ile, ila hadi kufikia sasa ni mwaka mpya wa fedha hakuna lolote na hata ongezeko lenyewe hakuna!!!

Wazanzibar walitangaza wazi maboresho ya maslahi ya wafanyakazi wao!

Samia ni mzaliwa wa Zanzibar, anayeongoza Jamhuri ambayo sehemu kubwa ni Bara!

Wao Zanzibar mapato ya kuwaongezea mishahara wanatoa wapi, angali bara tumewazidi kila kitu!?

Kwa kweli hii taasis imetundanfanya, Mpango aombe aombe radhi kama hakutumwa kusema yale aliyosema mbele ya kadamnasi ile!!!
 
Back
Top Bottom