Responded HOJA Hivi kwanini TANESCO wasiwe wanakopesha Luku mteja anapohitaji kama inavyofanya Mitandao ya Simu🤔

Responded HOJA Hivi kwanini TANESCO wasiwe wanakopesha Luku mteja anapohitaji kama inavyofanya Mitandao ya Simu🤔

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika

wa stendi

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Posts
26,597
Reaction score
29,527
Kuna mazingira unakuwa unashida au huwezi pata huduma labda ya kuweka hela kwenye simu wakati huo unauhitaji labda wa kumunua units (LUKU) hadi unalazimika kulala giza au kushindwa kufanya kazi kwa sababu ya umeme kuisha.

Kwenye Mitandao ya Simu kuna huduma ukitaka kukopa vocha/salio muda wa maongezi au bando unapewa bila wasiwasi, ukiweka hela kwenye simu yako au kununua vocha hapohapo wanakata chao.

Hivi TANESCO mtu amejisajili tena kwa namba yake ya simu kabisa na majina yote yapo pale hadi mtaa wa nyumba na namba ya nyumba kabisa wanashindwa nini kuweka hii huduma, mtu akikopa apewe units kulingana na kiasi cha alichokopa halafu huko baadaye akija nunua units mnazikata units zetu kwanza kama upande wa simu wanavyofanya?

Naomba mlifanye kazi hii hoja.



TANESCO YASEMA IMEPOKEA USHAURI👇🏽​
 
Mitandao ya simu kuna wajuba wanavunja laini wakishasongesha.. Tanesco nyumba za kupanga wenye nyumba wataachiwa misala sana
Wanaweka utaratibu mbona cm mtu kasajili kwa jina si lake lakini anakopeshwa.
 
Utaratibu kama upi? Mpangaji aje akope umeme wa 50,000 autumie uishe ahame.. wabongo tuna balaa sana
Na tena waweke limit ya ukopaji labda isizidi elfu 5,au kama kuna deni mita ijipini hadi lilipwe alafu wapewe kodi ya kuifungu kama inavyotempa unapewa namba au wanakuja wanakufungulia.
Hili linawezekana sana tena ni simpo mno
Utaratibu kama upi? Mpangaji aje akope umeme wa 50,000 autumie uishe ahame.. wabongo tuna balaa sana
 
Mbona hata songesha ina NIDA na wajuba hawajali wala nini wanavunja line😁
Sawa kunakua na limit ya kiasi cha ukopaji ikivuka labda wiki bila kulipa wanabloku mita hadi deni lilipwe
 
Mitandao ya simu kuna wajuba wanavunja laini wakishasongesha.. Tanesco nyumba za kupanga wenye nyumba wataachiwa misala sana
Duh,ni ujinga kuvunja line.mfano tigo naweza kopa mpaka laki nane...
 
Au waweke ussd code ya units tano za mkopo then next recharge wanakata au sio. Sasa nawaomba muamke msije mkojoe vitandani msingizie watoto
 
Back
Top Bottom