Responded HOJA Hivi kwanini TANESCO wasiwe wanakopesha Luku mteja anapohitaji kama inavyofanya Mitandao ya Simu🤔

Responded HOJA Hivi kwanini TANESCO wasiwe wanakopesha Luku mteja anapohitaji kama inavyofanya Mitandao ya Simu🤔

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Idea nzuri, watu wa mifumo watapiga sana hela, waandae mfumo mmoja wakawauzie Tanesco
 
Hiyo watu wanalipa tu na shirika linapata hasara. Wakikopwa si litakufa kabisa?
 
Yani kuna mazingira unakuwa unashida au huwezi pata huduma labda ya kuweka hela kwenye simu wakati huo unauhitaji labda wa kumunua units (luku) hadi inakuchukulia kulala giza au kushindwa kufanya kazi kwa sababu ya umeme kuisha.

Kwenye mitandao ya simu kuna huduma ukitaka kukopa vocha/salio muda wa maongezi au bando unapewa bila wasiwasi,na ukija weka hela kwenye simu yako au kununua vocha hapo hapl wanakata hela yao.

Hivi TANESCO mtu amejisaji tena kwa namba yake ya simu kabisa na majina yote yapo pale hadi mtaa wa nyumba na namba ya nyumba kabisa wanashindwa nini kuweka hii huduma,yani mtu akikopa apewe units kulingana na kiasi cha alichokopq qlafu huko baadae akija nunua units mnazikata units zetu kwanza kama upande wa simu wanavyofanya?
Naomba mlifanye kazi hili swala
Habari, ndugu wateja wetu mliochangia hii hoja, na asante kwa kuwasiliana nasi.

Kwanza, tunaomba radhi kwa kuchelewa kukujibu. Katika kipindi hiki, tulikumbana na changamoto kwenye akaunti yetu, lakini kwa sasa tatizo hilo limetatuliwa na huduma inaendelea kama kawaida.

Tunaomba tupokee ujumbe huu kama maoni muhimu yatakayotusaidia kuboresha huduma zetu. Tutayawasilisha katika kitengo husika kwa ajili ya kufanyiwa kazi.

Asante. ^FL
 
Wangefanya kwanza mtu ukinunua umeme unaingia moja kwa moja kwenye mita.
Habari, Ndugu Mteja.

Pole kwa kuchelewa kukujibu kuhusu swali lako. Kama tulivyokueleza awali, akaunti yetu ilikumbwa na changamoto katika kipindi hiki, lakini kwa sasa tatizo hilo limetatuliwa.

Tunatumaini kuwa maoni yako yamefanyiwa kazi. Tafadhali fahamu kua tulianzisha kampeni ya Mita Janja, ambapo baada ya kufanya manunuzi, unit huwekwa moja kwa moja kwenye mita yako.

Kampeni hii inaendelea nchini kote. Ikiwa huduma hii bado haijafika katika eneo lako, tunaomba uwe mvumilivu. Kampeni itakapofikia eneo lako, utapewa taarifa kubadili mita yako kwa hiari.

Asante. ^FL
 
Kuna mazingira unakuwa unashida au huwezi pata huduma labda ya kuweka hela kwenye simu wakati huo unauhitaji labda wa kumunua units (LUKU) hadi unalazimika kulala giza au kushindwa kufanya kazi kwa sababu ya umeme kuisha.

Kwenye Mitandao ya Simu kuna huduma ukitaka kukopa vocha/salio muda wa maongezi au bando unapewa bila wasiwasi, ukiweka hela kwenye simu yako au kununua vocha hapohapo wanakata chao.

Hivi TANESCO mtu amejisajili tena kwa namba yake ya simu kabisa na majina yote yapo pale hadi mtaa wa nyumba na namba ya nyumba kabisa wanashindwa nini kuweka hii huduma, mtu akikopa apewe units kulingana na kiasi cha alichokopa halafu huko baadaye akija nunua units mnazikata units zetu kwanza kama upande wa simu wanavyofanya?

Naomba mlifanye kazi hii hoja.



TANESCO YASEMA IMEPOKEA USHAURI👇🏽​
Mimi sioni kama ni sahihi kukopesha umenme, mfumo uliopo ubaki hivyohivyo. Watanzania punguzeni kupenda mikopo mnanyonywa sana kupitia mikopo ila utasikia bora ninatumia ninakidhi haja yangu, inaumiza sana
 
Back
Top Bottom