Responded HOJA Hivi kwanini TANESCO wasiwe wanakopesha Luku mteja anapohitaji kama inavyofanya Mitandao ya Simu🤔

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Idea nzuri, watu wa mifumo watapiga sana hela, waandae mfumo mmoja wakawauzie Tanesco
 
Hiyo watu wanalipa tu na shirika linapata hasara. Wakikopwa si litakufa kabisa?
 
Habari, ndugu wateja wetu mliochangia hii hoja, na asante kwa kuwasiliana nasi.

Kwanza, tunaomba radhi kwa kuchelewa kukujibu. Katika kipindi hiki, tulikumbana na changamoto kwenye akaunti yetu, lakini kwa sasa tatizo hilo limetatuliwa na huduma inaendelea kama kawaida.

Tunaomba tupokee ujumbe huu kama maoni muhimu yatakayotusaidia kuboresha huduma zetu. Tutayawasilisha katika kitengo husika kwa ajili ya kufanyiwa kazi.

Asante. ^FL
 
Wangefanya kwanza mtu ukinunua umeme unaingia moja kwa moja kwenye mita.
Habari, Ndugu Mteja.

Pole kwa kuchelewa kukujibu kuhusu swali lako. Kama tulivyokueleza awali, akaunti yetu ilikumbwa na changamoto katika kipindi hiki, lakini kwa sasa tatizo hilo limetatuliwa.

Tunatumaini kuwa maoni yako yamefanyiwa kazi. Tafadhali fahamu kua tulianzisha kampeni ya Mita Janja, ambapo baada ya kufanya manunuzi, unit huwekwa moja kwa moja kwenye mita yako.

Kampeni hii inaendelea nchini kote. Ikiwa huduma hii bado haijafika katika eneo lako, tunaomba uwe mvumilivu. Kampeni itakapofikia eneo lako, utapewa taarifa kubadili mita yako kwa hiari.

Asante. ^FL
 
Mimi sioni kama ni sahihi kukopesha umenme, mfumo uliopo ubaki hivyohivyo. Watanzania punguzeni kupenda mikopo mnanyonywa sana kupitia mikopo ila utasikia bora ninatumia ninakidhi haja yangu, inaumiza sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…