Hivi kwanini tunaambiwa tuishi na wanawake kwa akili wakati kimsingi tunatakiwa tuishi na kila mtu kwa akili

Hivi kwanini tunaambiwa tuishi na wanawake kwa akili wakati kimsingi tunatakiwa tuishi na kila mtu kwa akili

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Unajua me huwa sielewi hapo kwamba kuna akili nyingine ya ziada tofauti na hii unayotakiwa kuitumia ili ukae na mke..nachojua kila mtu aliye mbele yako unatakiwa utumie akili uwe mjanja uwe mwerevu ila pia uwe mpole uwe kama njiwa pia uwe kama nyoka yaani full akili muda wote.ukifanya hivyo utaepusha shari na watu ila pia hutokaa utapeliwe maana muda wowote una wasiwasi na unajua jinsi ya kumjibu mtu..

Mimi binafsi nakaa na mwanamke kiukweli nachotumia ni upendo na sio akili labda akili huwa naitumia tu kwenye suala la fedha maana me mke wangu mbahili ukimpa hela yote akushikie siku ukitaka hata ya bia mbili tatu hakupi inakuwa shida ..so akili nayotumia ni kumpa kiasi cha fedha kumkadiria.mfano nimepata laki tano nachomwambia tumelipwa laki tatu hii hapa shika ni ya nyumbani..maana me najijua siwezi kukaa na hela so hii nyingine laki mbili ndo yangu inanilinda mtaani kunywa na kubet kdg ikiisha basi najua imeisha ila nyumbani misosi ipo kama yote. Hiyo ndo akili yangu inapotumika ila tofauti na hapo sijaona lingine kwa kweli.nachokiona ni upendo kumpa muda wako na kutosikiliza ya watu maana furaha ya ndoa yako inaanza na wewe


DR HAYA LAND ongezea neno hapo
 
Tunatakiwa tutumie akili kwa wanawake maana usipotumia madhara yake ni makubwa sana ila kwa watu baki hata usipotumia madhara sio makubwa na yanaepukika ila kwa mwanamke ukipigwa unapigwa kwelikweli ki mwili na kiroho hivyo tumia akili ili kupunguza madhara kama yatatokea
 
Wanawake ni viumbe wa hisia mno unaweza ukafanya kitu cha kawaida tu ila yeye akakichukulia serious mno hivyo nahisi ina akili ni kujua nini cha kufanya na kusema kwa muda gani na mazingira gani
 
Back
Top Bottom