Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
1. Kiwango cha jumla cha elimu kipande. Watu wajinga ni watu ambao ni rahisi kuwadanganya. Hakuna demokrasia kwenye ujinga. Kwa sababu, hata mfumo wa kupiga kura unataka mtu anayeweza kuchambua mambo ili kupiga kura kwa ufanisi.Hoja maridhawa sana mkuu.
Kwa uzoefu wako na ukongwe wako katika mambo ya siasa, unadhani nini kifanyike ili kula za wananchi ziheshmiwe kitu ambacho kwa Africa nakiona ni kigumu sana labda kwa miaka mingi ijayo. Huku kwetu Afrika na Tanzania ikiwemo, aliyepo madarakani ana uhakika wa kushinda kwa 75%..Yaani akishinda mpinzani ni habari kubwa sana...nini kifanyike mkuu.
2. Kiwango cha jumla cha kujiamini na ushupavu kipande. Hata wananchi wakielimika, lakini wakikosa ushupavu na kujiamini, elimu yao wataiweka mfukoni na kukubali ujinga kama tulivyoona kwenye miaka sita iliyopita mtu mmoja mjinga anaamrisha nchi ya mamilioni ya watu kufanya ujinga.
3. Kiwango cha jumla cha ushirikishwaji wa umma (inclusivity) kipande. Ushirikishwaji wa umma si tu jambo zuri kisiasa kwa kuwa litawapa wananchi wengi zaidi nafasi ya kuchangia uendeshwaji wa nchi yao na kujiona wana hisa katika nchi yao, bali pia utasaidia kupata mawazo mengi zaidi na tofauti zaidi kutoka kwa watu wengi zaidi. Mfumo wa sasa ni wa usiri na wa kuongozwa na wachache, kitu kinachopelekea nchi kuacha vipaji vingi. Suala hili limetajwa katika kitabu cha "Why Nations Fail:The Origins of Power, Prosperity and Poverty" cha Daron Acemoglu wa MIT na James A Robinson wa University of Chicago. Hiki ni kitabu kizuri kilichachambua mengi sana kuhusu suala hili.
4. Mabadiliko ya kiutamaduni. Watu wengi wanaongelea mabadiliko ya katiba, wakisema katiba bora itatupa maendeleo na uhakiki mzuri zaidi wa uongozi. Lakini, wengine tunasema, katiba mpya ni jambo zuri, hatupingi, bali, inakuwaje hata mazuri ya katiba ya sasa hatuyatumii? Hivi kweli hapa katiba ndiyo tatizo? Ama utamaduni wa hewala hewala wa watu ndiyo tatizo?
Hivi, katiba yetu mbaya ndiyo imetuletea matatizo? Au matatizo yetu ndiyo yametuletea katiba mbaya?
Sasa, mimi nasema tubadilishe utamaduni. Tuondokane na utamaduni wa hewala hewala. Tujue kudai haki zetu. Tukishaweza hilo, hata tukibadilisha katiba, kwanza tutaibadilisha vizuri. Na zaidi, tutaitumia vizuri.
Tusipoweza hilo la kuji assert, kubadilisha utamaduni na kudai haki zetu, hili la kubadilisha katiba ndugu zangu litabaki kuwa gumzo tu miaka nenda rudi. Na hata kwa muujiza likiwezekana, hiyo katiba mpya itabaki kuwa mapambo tu. Hatutaweza kuitumia.
Si tumeona rais Magufuli kakataza mikutano ya hadhara, kitu ambacho kimeruhusiwa kikatiba under "right to assembly". Wazi kabisa. Katiba, si sheria ya kawaida. Sheria mama. Rais kaja, kaitupilia mbali katiba aliyoapa kuilinda. Na hakuna yeyote aliyembishia na kumuadabisha mpaka kafariki. Sasa kama hii ya sasa wanaivunja, hiyo mpya tutahakikishaje hawataivunja hivyo hivyo bila kubadilisha utamaduni wetu?
Kwa hivyo ni muhimu tubadilishe utamadunin wetu.
5. Katiba mpya itakayoondoa ujinga wa rais kuteua tume ya uchaguzi, na kuwa na miguvu ya ajabu ajabu. Itakayostawisha mfumo wa demokrasia shirikishi zaidi na endelevu. Itakayowapa nguvu zaidi wananchi.
Wewe unaongelea term limits?
Term limit mbona cha mtoto.
Mimi nataka katiba inayoweza kuwapa wananchi nguvu za kufanya recall election.
Yani mmemchagua mbunge kwa kipindi cha miaka mitano, baada ya mwaka mmoja mkamuona huyu ovyo hafai, mkikusanya saini za kutosha mnaitisha uchaguzi nwingine na kumtoa baada ya mwaka huo mmoja!
That's better than term limits.
Mbunge anayependwa anakaa anavyotaka kama watu wanamtaka.
Mbunge asiyependwa hata miaka mitano hamalizi. Anafanyiwa recall ndani ya mwaka mmoja kama kura zinatosha.