Tatizo tff imejaa wapigaji, wambura kwa cheo chake ndiye mwenyekiti wa kamati ya fedha na mipango wa tff hivyo akawa anawabania wapigaji kuchota pesa za tff ila kwa kuwa wao ni wengi wakakaa kama kamati wakamuundia fitina wakammaliza. So, kwa kifupi tatizo la wambura ni uadilifu wake ndio maana wamemtimua bila kumpa haki ya kusikilizwa na wanazingua hata kusikiliza rufaa yake. Uliona wapi mtu mwenye cheo cha makamu wa rais anatimulia kirahisi rahisi hivyo bila kusikilizwa
1. Muundo wa uongozi/utawala wa TFF ni kwa mujibu wa FIFA au kuna mambo ni ya Tanzania? kama ndivyo, inakuwaje makamu wa rais wa TFF awe mwenyekiti wa moja ya kamati za ufundi: fedha na mipango, nafasi ambayo pia anaweza kukaimu nafasi ya raisi ambaye ana maamuzi ambayo anaweza kuwa ameyatengeneza mwenyewe kutoka kwenye kamati husika? yaani kutokuwepo kwa kutotegemeana kwa maamuzi?
2. Hivi hatujiulizi miaka tangu miaka 20 iliyopita unakuta a good set of individuals is going around the same positions in an organization. Ina maana for the past 20 years, Tanzania imeshindwa kupata watu au kwa mfumo au kwa kukuzwa, ambao wangeweza kuwabadili hawa? hivi huyu hakuwepo tangu enzi za Ndolanga na Rage?
3. Possibly, anahangaika na fraternity ambayo haelewi politics zake mbona anahangaika mara Simba, wanamnyima, mara TFF, wanamkorofisha if at all those allegations are true or not true?.
4. Anapigania kitu gani kwenye soka ambacho hata wasio karibu sana na vyombo hivyo wanaweza kumtetea kwa maana ya kutueleza ni kitu gani anakiweza zaidi ya wenzie ktk kuongoza: ni michezo? au mpira specifically? au kudhibiti mipango na uchumi?. Hii ni kwa maana ya taaluma yake kwenye uongozi, michezo na uchumi na mipango na any appreciable past performance!
5. Otherwise tunamtakia maisha mema na ikiwezekana shitaka lake ashinde ila siyo lazima aende tena TFF, Simba n.k. anaweza kuanzisha academy ataweza kuwa prove wrong wanaomsumbua.