KERO Hivi kwanini vituo vingi vya afya vya serikali taarifa ya matibabu mgonjwa hapewi?unapewa tu dawa daftari wanabaki nalo kwanini?

KERO Hivi kwanini vituo vingi vya afya vya serikali taarifa ya matibabu mgonjwa hapewi?unapewa tu dawa daftari wanabaki nalo kwanini?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

polokwane

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2018
Posts
4,158
Reaction score
7,667
Hiki kitu huwa najiuliza sana na nimekutana na hii changamoto vituo vingi sana hasa vya serikali yaan unatibiwa lakini unacho toka nacho ni dawa basi lakini taarifa zingine za maandishi wanabaki nazo wao na hata daftari walilo kuandikia dawa na maelezo ya matibabu wanabaki nalo wao.

Sasa huwa najiuliza mbona miaka ya nyuma ilikuwa unapewa taarifa zote za za matibabu uliyo pewa na dawa ulizo tumia na sindano ulizo andikiwa ili ikisaidie hata kama una hama hospitali ili iwe rahisi kujua awali ulitumia dawa gani na sasa upewe ipi, lakin kwa sasa naona kama imekuwa siri ya madaktari maana wanabaki navyo wao.

Mimi Huwa nahisi ni njia ya kukwepa tuhuma hasa ikitokea wamekupa matibabu yasiyo sahihi, na mbaya zaidi vituo vingine tena vingi vya serikali hata ile fomu ya NHIF nakala hawakupi yani utatoka na dawa au kama sindano utachomwa na hujui ni sindano gani maana huna REFFERENCE yeyote

Hebu wajuvi mtupe maelekezo imekaaje hii!? Labda mimi ndio nipo nyuma ya wakati
 
Back
Top Bottom