Inawezekana hivyo lakini wewe unakosea ukijumlisha kusema wote ni wezi.Ndio ,kuna wale waliotumia mamlaka yao vibaya kujitajirisha ,yani kwa kizungu - abuse of office for gain or influence peddling.Je inakuwaje familia za viongozi wote wa Kenya baada ya Uhuru ni matajiri?
Pengne ikawa wewe na ndugu zako 100 ndio sawa na mkenya 1 but sio Watanzania wengne,tatzo hampendi kusoma histolia mkaelewa mambo kazi kutembelea mawazo ya watu wengine kisa wanawajaza propaganda za kishamba.Watanzania 100 sawa na mkenya mmoja ukizijumuisha fikra zao ccm wapo madarakani toka 1961 maisha bado kama tupo chini ya mjerumani.
Pengne ikawa wewe na ndugu zako 100 ndio sawa na mkenya 1 but sio Watanzania wengne,tatzo hampendi kusoma histolia mkaelewa mambo kazi kutembelea mawazo ya watu wengine kisa wanawajaza propaganda za kishamba.
Kenya kukataa kuungana na Tz ilitokana na uroho wa madaraka wa viongoz wake wa kwanza kwa kuona kama wangeungana na kua nchi moja wasingekua na nguvu hasa ya kijeshi.
Soma vizuri maelezo yangu, nilimzungumzia mzee Jommo Kenyatta na watu wake wa karibu, na sera zake za ubepari, sijui kama nilisema juu ya wakenya woteInawezekana hivyo lakini wewe unakosea ukijumlisha kusema wote ni wezi.Ndio ,kuna wale waliotumia mamlaka yao vibaya kujitajirisha ,yani kwa kizungu - abuse of office for gain or influence peddling.
Sasa unakana uliyosema? Angalia vizuri ulisema viongozi wote baada ya uhuru 1963 wamekuwa matajiri kumaanisha wote ni wezi,mafisadi na mabepari.Soma vizuri maelezo yangu, nilimzungumzia mzee Jommo Kenyatta na watu wake wa karibu, na sera zake za ubepari, sijui kama nilisema juu ya wakenya wote
Unatakataa kwamba viongozi waliopigania uhuru Kenya karibu wote walijitajirisha wao wenyewe mara tu baada ya kuingia madarakani?Sasa unakana uliyosema? Angalia vizuri ulisema viongozi wote baada ya uhuru 1963 wamekuwa matajiri kumaanisha wote ni wezi,mafisadi na mabepari.
Hivi kweli Tanganyika ilikuwa hata na nguvu ya Kuifanya Kenya Koloni lake ndani ya Mfumo wa Shirikisho kweli ???
Haingii akilini kabisa na hata ukiangalia vizuri Mwalimu Nyerere alipendekeza huu Muungano hata kabla ya Tanzania kuwepo
Kwa Kenya lilikuwa ni suala la ulafi tu...Kumbuka hata katika kuivunja jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977 Wakenya ndio waliokuwa mbele na walifurahia mno kuvunjika kwa Jumuiya hiyo na hasa akina Njonjo na wenzake ambao waligonganisha glasi za mvinyo kusherehekea...Ieleweke kuwa wakati nchi hizi zinapata uhuru Kenya ilikua mbele kiuchumi kwa kuwa Waingereza waliwekeza sana huko kwa viwanda, elimu na kadhalika...Kenya ilikuwa ni kama nyumbani kwa Waingereza, ma-settler walikuwa wengi..lile lilikuwa ni colony hasa...Tanzania ilikuwa ni trusteeship territory ambapo waingereza waikuwa wanatawala kwa niaba ya Umoja wa Mataifa (UN) huku wakijua kuwa ipo siku watakuja kuondoka tu...Hivyo Waingereza hawakuwa na moto sana wa kuiendeleza Tanzania au Tanganyika wakati ule. Kwa hiyo pale nchi hizi ziliipopata Uhuru (Tanganyika mwaka 1961 na Kenya mwaka 1963) Kenya ilikuwa juu kiuchumi na kielimu..Wakenya wengi kwa maana ya elites au viongozi na wafanyabiashara wakaona kuwa hakuna haja ya kuikumbatia Tanganyika ambayo ni maskini...Hilo lilikuwa ni kosa kubwa la kimkakati...kwani Tanzania ina raslimali nyingi ikiwemo ardhi... Kwa hiyo baada ya kuvunjika Jumuiya bidhaa nyingi za Kenya ilibidi zianze kutafuta soko ambalo liko Tanzania na nchi nyingine..Kwa hiyo wakawa sasa wanataka ushirikiano wa kiuchumi na Jumuiya kwa maana ya bidhaa zao zipate soko...Pia Wakenya wanapigania free movement of labour ili Wakenya wengi waje wachukue nafasi ajira nyingi kwenye nchi kama Tanzania...Yaani experts na wataalamu mbalimbali wa kenya wanaaka soko la ajira lipanuke zaidi kwani kwao soko limevimba.....Halafu lipo suala la ardhi ambapo Wakenya wengi wangependa waje Tanzania kuwekeza kwenye kilimo kwa kuwa Tanzania ina ardhi kubwa...Kenya suala la ardhi ni nyeti kwani watu wanahodhi ardhi na ni mali ya mtu tofauti na Tanzania ambako ardhi ni mali ya serikali.
Hiyo sikatai hata kidogo,kumbuka hatukuwa na kitu inaitwa "ethics in governance" ,no integrity test ,hapakuwepo anti corruption commission hadi miaka ya 90's ...na hata leo ingawa tumepiga hatua kidogo kupambana na ufisadi bado mambo yale yapo.Unatakataa kwamba viongozi waliopigania uhuru Kenya karibu wote walijitajirisha wao wenyewe mara tu baada ya kuingia madarakani?
Mkuu wangu wewe ni mtu muwazi sanaa, natumai wengi watajifunza kitu kikubwa kutoka kwako!
Sasa naomba nisikie maoni yako katika hili la Rwanda na Burundi kutaka kuwa sehemu ya Shirikisho la Afrika Mashariki.
Je, unahisi Ukabila wa Rwanda na Burundi unaweza kuisha baada ya wao kuingia kwenye Shirikisho la Afrika Mashariki ??
Ok binafsi siamini kama ukabila wa Rwanda na Burundi utaisha....ni mawazo yangu tu kwamba nchi hizi mbili ziliharakishwa mno kuingia kwenye Jumuiya hii...Suala la uhasama wa kikabila huko Burundi na Rwanda ni historical...una mizizi mikubwa tangu ukoloni...Watutsi ingawa ni wachache waliandaliwa kama ni watawala na Wahutu kama wanaotawaliwa ingawa ni wengi..ni suala la perception, attitude na mentality...siyo rahisi kumaliza ukabila huo kwa kuingizwa tu kwenye Jumiya....Ni mkakati unaohitaji kazi kubwa ya kuimarisha uchumi kwa watu wote kwa maana ya wahutu wawe imara kiuchumi na watutsi pia wawe imara kiuchumi na watu wote wa nchi hizi za jumuiya ya Afrika Mashariki waimarike kiuchumi na pia demokrasia...hilo likifanyika hapana shaka ukabila utaisha..lakini kwa trend ya uchumi wa dunia sioni hilo kutokea..nchi hizi zetu za Afrika mashariki zitaendelea kuwa maskini na wenye nacho wataendelea kuwa nacho kwani huu ndio mfumo wa uchumi wa dunia. Kwa mawazo yangu nchi hizi za Burundi na Rwanda na sasa Sudan ya Kusini zimeharakishwa kuingizwa kwenye jumuiya kwa sababu za kuchumi tu..Yaani viwanda viilivyopo huko Kenya na kwa mbali Uganda wanataka soko la bidhaa...Nahisi Kenya na Rwanda wana uhusiano mzuri wa kibiashara...Siamini kama Tanzania ilikuwa na moto sana kuhusu Rwanda na Burundi na hata Sudan ya Kusini kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki...Tena basi kwa Tanzania, Burundi ndiyo nchi ya kuiamini zaidi kuliko Kenya na Rwanda...Watanzania walio wengi wako symphathetic zaidi kwa Burundi kuliko ilivyo kwa Rwanda...Lakini huu ni mtazamo wangu tu kwa uzoefu wangu...Watanzania mara nyingi wako sensitive sana na masuala ya utaifa wao na hasa suala la ardhi...Watanzania whether they are right or wrong huwa wanawaangalia Wakenya kwa jicho tofauti kabisa au jicho la hofu na tahadhari pamoja kwamba Wakenya lengo lao siyo ushirikiano wa dhati bali ni kwa kuwa Kenya hawana namna kwani viwanda vyao vitakosa soko....Ndiyo maana Watanzania walio wengi wanakuwa emotional pale foreigners wanapokuja kugusa raslimali na hasa ardhi na hivi sasa madini...Ndiyo maana Watanzania walio wengi hawapendi kusikia kitu kinaitwa free movement of labour..wanajua hiyo ikitokea foreigners na hasa wakenya watakuja kuhodhi ardhi na pia ajira... Na ajabu ya yote ni suala la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar...Watanzania wengi wakiwemo wa Bara wanapenda muungano huo uendelee...Lakini kwa watu wa Bara huwa wanakerwa sana tena kimya kimya kuhusu kelele kutoka kwa baadhi Zanzibar kuwa inamezwa na Bara...In fact Wabara wengi, kwa uzoefu wangu, wanaona kuwa Wazanzibar ndio wanaofaidi zaidi kuhusu Muungano, kwani Wazanzibar wengi wako bara wamewekeza kwenye majumba, viwanda na biashara...Wazianzibari wengi pia wanamiliki ardhi bara na hata kuajiriwa kwenye nafasi mbalimbali za kazi bila tatizo ingawa ni wabara wachache wanaoweza kumiliki ardhi huko Zanzibar na hata kuweza kupata ajira kule...Hofu kwa baadhi yetu ni kuwa kama kelele kutoka kwa baadhi wa Zanzibar zikizidi inaweza ikatokea siku moja wabara wakasema to hell with Zanzibar. Lakini hii ni hofu tu kwa baadhi yetu. Kwa ujumla wake suala la ushirikiano na jumuiya ndani ya nchi za Afrika Mashariki ni gumu na nyeti...
Mkuu nakubaliana kabisa na wewe!
Hili ndilo nimelisema jana kwa ndugu yetu TsafuRD kwenye bandiko langu la #46. Ujenzi wa Muungano ni sawa na Mnara wa babeli, kuna sehemu mtafika ni lazima mtapishana lugha tu. Sasa msipokuwa makini na kujenga malengo sawa kwa pamoja basi wale wenye malengo yanayolingana, lugha moja na tabia fanana ni lazima watajivuta kivyao na kuharibu kila kitu kwenye huo muungano. Marekani yalitokea hayo mwaka 1861, wale wazungu wa kusini na Biashara yao ya Utumwa na wale kwa Kaskazini na uchumi wa viwanda. Nchi ikaparanganyika vibaya na damu ikamwagika kwa zaidi ya miaka minne. Tena usisahau hawa waliingia kwenye Muungano kwa makubaliano kabisa; sembuse sisi Afrika Mashariki tunaotaka kuungana kwa msukumo wa masoko na uchumi.
Inabidi tupeane muda wa mpito na malengo ya pamoja yawe wazi kabisa,
Kwasababu kama nchi imeunganishwa na nguvu ya masoko basi siku huo uchumi wa masoko unapoteza dira taifa litagawanyika kama Uchumi wa kikomunisti ulivyosambaratisha jumuiya ya kisovieti. Kama tulishindwa kuungana kwa kutumia undugu mwanzoni wakati tunapata uhuru nadhani ni bora tubakie tu na umoja wa kibiashara ambao haulengi kuingilia mizizi ya maslahi ya kila taifa.
Wasitegemee Free Lunch hapa Tanzania.
Hapa ni ukweli, Waingereza wengi walibaki Kenya na wana mashamba makubwa sana Kenya. Pia kuna waItaliano waliokuwa wakinyakua mashamba makubwa makubwa. Hili ni mojawapo ya reasons wakenya hawana mashamba.Kenya ilikuwa ni kama nyumbani kwa Waingereza, ma-settler walikuwa wengi..lile lilikuwa ni colony hasa...Tanzania ilikuwa ni trusteeship territory ambapo waingereza waikuwa wanatawala kwa niaba ya Umoja wa Mataifa (UN) huku wakijua kuwa ipo siku watakuja kuondoka tu