Mkuu nakubaliana kabisa na wewe!
Hili ndilo nimelisema jana kwa ndugu yetu
TsafuRD kwenye bandiko langu la #46. Ujenzi wa Muungano ni sawa na Mnara wa babeli, kuna sehemu mtafika ni lazima mtapishana lugha tu. Sasa msipokuwa makini na kujenga malengo sawa kwa pamoja basi wale wenye malengo yanayolingana, lugha moja na tabia fanana ni lazima watajivuta kivyao na kuharibu kila kitu kwenye huo muungano. Marekani yalitokea hayo mwaka 1861, wale wazungu wa kusini na Biashara yao ya Utumwa na wale kwa Kaskazini na uchumi wa viwanda. Nchi ikaparanganyika vibaya na damu ikamwagika kwa zaidi ya miaka minne. Tena usisahau hawa waliingia kwenye Muungano kwa makubaliano kabisa; sembuse sisi Afrika Mashariki tunaotaka kuungana kwa msukumo wa masoko na uchumi.
Inabidi tupeane muda wa mpito na malengo ya pamoja yawe wazi kabisa,
Kwasababu kama nchi imeunganishwa na nguvu ya masoko basi siku huo uchumi wa masoko unapoteza dira taifa litagawanyika kama Uchumi wa kikomunisti ulivyosambaratisha jumuiya ya kisovieti. Kama tulishindwa kuungana kwa kutumia undugu mwanzoni wakati tunapata uhuru nadhani ni bora tubakie tu na umoja wa kibiashara ambao haulengi kuingilia mizizi ya maslahi ya kila taifa.
Wasitegemee Free Lunch hapa Tanzania.