MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Umeonge kiushabiki sana bila kuangalia mambo kitaalamu;
Mosi, tatizo kubwa na la pekee ndani ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni kuwepo na Mfumo Mbovu usioeleweka.
Haueleweki kama ni nchi moja au shirikisho. Hivyo kama tukiweza kumaliza hili Tatizo bila woga wowote ule basi nakuhakikishia hapa Afrika hakuna Muungano Imara na wenye faida kama ule wa Tanganyika na Zanzibar. Ulichokisikia wewe kule Zenji ni hisia tu ambazo zimejengwa zaidi na mihemko ya Kisiasa na kidini bila kuangalia uhalisi; ni sawa tu na kusema Tanzania kuna Baa la njaa, wengi waliamini na kuhisi kweli wanaumwa njaa kumbe hakuna kitu.
Pili, umesahau kwamba Tanganyika ilipendekeza kuwepo kwa Shirikisho (A Federal Republic) tofauti na Zanzibar ambako Karume alitaka kuwepo na nchi moja tu yenye iliyoungana katika kila kitu. Nadhani mfumo wa Shirikisho la Afrika Mashariki usingekuwa na Maneno mengi sana kwasababu tungeunganishwa tu kwenye mambo muhimu ya Shirikisho chini ya mwamvuli wa FEDERAL COMPACT. Kenya mngekuwa na yenu, vivyo hivyo Tanganyika, Zanzibar na Uganda wangekuwa na yao ya ndani kama nchi wanachama.
NB: Muhimi ni tufanye nini ili turudishe imani baina ya nchi hizi mbili ndugu ???
Sijaongea kiushabiki, ila nimegusia uhalisia wa mambo ambayo nimeyaona kwenu kaka, japo huwa mnayafumbia macho lakini yapo na hayaondoki kiulaini. Kwanza kabisa mchakato wa kupata katiba yenu mpya ulianguka baada ya kushindwa kupata suluhu kwa hili la muungano, mara serikali tatu, mara mbili mara hiki mara kile.
Watanganyika wengi wanataka wawe na rais wao kama ilivyo Zanzibar, halafu ndio pawe na rais wa muungano. Ukienda kule Zanzibar utakuta siku baada ya siku ni kama wanajitenga. Niliona sehemu sasa wameibuka na sheria kwamba lazima uwe mzawa wa Zanzibar ili uajiriwe sehemu yoyote kwenye serikali yao.
Hivyo kwa kifupi, muungano ni shughuli sana, kuudumisha inahitaji nguvu nyingi na pia hatungeweza kuungana kisa Nyerere na Kenyatta wamekubaliana, ilifaa iwe mchakato unaowahusisha watu wote wa nchi zote hizi na tuelewane tunaungana vipi. Hayo mambo ya watu wawili kukutana boardroom ndio yanawatatiza nyie, pale Nyerere na Karume walikaa na kukubaliana wao kwa wao na hayo makubaliano mlishagoma kuyaweka wazi.
Mimi naona kwa jinsi tunavyokwenda ndivyo inavyofaa, kwamba tunaungana taratibu kwenye baadhi ya vitu, yaani people driven union.