Hivi kwanini walokole huwa wakali unapokuwa against na nchi ya Israel?

Hivi kwanini walokole huwa wakali unapokuwa against na nchi ya Israel?

Unakuta mtu unamuwekea nyama ya nguruwe na hapa unamuweka muyahudi

Unaweka mafuta ya kukaangia nyama ya nguruwe na bunduki pembeni

Unamuuliza chagua moja kula nyama ya nguruwe au kuua muyahudi

Eti anachagua kuua muyahudi na kumkaanga kabisa eti aende apate malaya siku akifa, sasa hio ni mbigu au kitambaa cheupe

Hii ni mental case
 
Unakuta mtu unamuwekea nyama ya nguruwe na hapa unamuweka muyahudi

Unweka mafuta ya kukaangia nyama ya nguruwe na bunduki pembeni

Unamuuliza chagua moja kula nyama ya nguruwe au kuua muyahudi

Eti anachagua kuua muyahudi na kumkaanga kabisa eti aende apate malaya siku akifa, sasa hio ni mbigu au kitambaa cheupe

Hii ni mental case
Eenh hii kali😂😂😂
 
Unakuta mtu unamuwekea nyama ya nguruwe na hapa unamuweka muyahudi

Unweka mafuta ya kukaangia nyama ya nguruwe na bunduki pembeni

Unamuuliza chagua moja kula nyama ya nguruwe au kuua muyahudi

Eti anachagua kuua muyahudi na kumkaanga kabisa eti aende apate malaya siku akifa, sasa hio ni mbigu au kitambaa cheupe

Hii ni mental case
Wanawaua wayahudi ni wale waarabu wanapambana nao huko mashariki ya kati, hata wayahudi pia huwaua waarabu.

Vipi kuhusu hawa watanzania ambao makanisani Kila kukicha ni kuiombeq nchi ya Israel na kuwalaani wenzao wanaounga wapalestina.
 
Wanawaua wayahudi ni wale waarabu wanapambana nao huko mashariki ya kati, hata wayahudi pia huwaua waarabu.

Vipi kuhusu hawa watanzania ambao makanisani Kila kukicha ni kuiombeq nchi ya Israel na kuwalaani wenzao wanaounga wapalestina.
Unaonaje pale watu wanaomtukuza mtu alie kuwa pedophile?

Aliekuwa ana miliki watumwa?

Aliekuwa anaua watu kama kuku kwa kuwalazimisha kugeuza imani zao?
 
Mimi sio "mlokole", whatever that means.

WHO IS ISRAEL?

KWA KIFUPI:
Waisraeli ni wale wanaomkubali MUNGU wa Israeli na mwana wake YESU KRISTO.

(the years written are approximations)


1) Nchi ya kale ya Israeli kabla haijapotea karne ya 1 na ghafla kurudi karne ya 20 palepale ilipopotea, kwa jina lilelile, ikiwa na lugha ileile, kitabu kilekile, utamaduni uleule, wakiwa na maadui walewale, yani kwa kifupi ni kama wali pause kwa muda (atokee kiazi aseme hiyo ni kawaiiiiida),

Nchi hiyo ilikuwa ni steji ya MUNGU ulimwenguni. Ndo alipachagua hapo kujifunua ulimwenguni. Ndo taifa alilotenga ili kujitofautisha na miungu mingine aliowaachia mamlaka ulimwenguni i.e roho waovu / malaika waasi. Ndio atakaowatumia mwishoni kujiletea utukufu.

Ili dunia imjue MUNGU wa Israeli ndiye MUNGU wa kweli, hawa wengine ni God-wannabe-s.

i) "Mungu Mkuu alipoyagawia mataifa mali yao, alipowagawa wanadamu, kila taifa alilipatia mipaka yake,

kulingana na idadi ya watoto wa Mungu, lakini alijiwekea watu wa Yakobo kuwa wake, hao alijichagulia kuwa mali yake."

Kumbukumbu la Sheria.32.8-9.BHND , BHN, SCLDC10

(other translations zinasema "kulingana na idadi ya wana wa Israeli". According to Dr. Michael Heiser, mtaalam wa Kiebrania/agano la kale (mcheck YouTube), correct translation ni "kulingana na idadi ya watoto wa Mungu.

Kwahiyo baada ya garika, kwenye mnara wa Babeli, MUNGU aligawa watu, akawaachia mataifa malaika waovu, na yeye akachukua moja.

Ndomaana Paulo alisema "vita vyetu si vita kati yetu na binadamu, bali ni vita dhidi ya jeshi ovu la ulimwengu wa roho; tunapigana na watawala, wakuu na wenye nguvu, wanaomiliki ulimwengu huu wa giza." Waefeso.6.12.)


ii) "Basi, waambie Waisraeli kwamba mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Ninachotaka kufanya si kwa faida yenu nyinyi watu wa Israeli, bali ni kwa heshima ya jina langu takatifu mlilolikufuru miongoni mwa mataifa mlikokwenda.

Nitalirudishia hadhi yake takatifu jina langu kuu mlilokufuru miongoni mwa mataifa. Hapo ndipo mataifa yatakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nimesema. Nitawatumia nyinyi kuonesha utakatifu wangu mbele yao."

Ezekiel.36.22-23.BHN


2)
Je MUNGU aliwachagua waisraeli kwasababu ni bora kuliko mataifa mengine? Its the opposite, wakati anawachagua they were the least! Tena walikuwa watumwa!

i) "Fanyeni hivyo kwa kuwa nyinyi mmewekwa wakfu kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Kati ya watu wote ulimwenguni aliwachagua nyinyi ili muwe taifa lake mwenyewe.

Mwenyezi-Mungu hakuwapenda nyinyi na kuwateua kwa kuwa nyinyi ni wengi mno kuliko watu wengine; nyinyi mlikuwa wachache kuliko mataifa mengine duniani."
Kumbukumbu la sheria.7.6-7.BHN


ii)
"Nitatembea kati yenu na kuwa Mungu wenu nanyi mtakuwa watu wangu.

Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, niliyewatoa nchini Misri ili msiwe watumwa wa Wamisri. Mimi nimevunja nira mliyofungiwa shingoni mwenu na kuwafanya mtembee wima."

Walawi.26.12-13.BHN


3)
Na ili kuwatofautisha na mataifa mengine ndo akawapa zile sheria za kuwatofautisha:
  • msile vyakula fulani,
  • mvae vitu fulani (mf. Vifundo/vishada),
  • msivae vitu fulani (mf. nguo zilizoshonwa na material mbili tofauti)
  • sheria za usafi (mf kuhusiana na hedhi, magonjwa, maiti),
  • siku kuu
  • ibada za hekaluni

Sheria hizi tunaambiwa zilikuwa "mlezi" hadi alipokuja Kristo. They point us to Christ.

"Basi, hiyo sheria ilikuwa kama mlezi wetu mpaka alipokuja Kristo, ili kwa njia ya imani tufanywe waadilifu mbele yake Mungu.

Lakini kwa vile ile imani imekwisha fika, sisi hatuko tena chini ya mlezi."

Wagalatia.3.24-25.BHN

Mfano:
- dhabihu zote hekaluni zinaakisi dhabihu ya YESU.

- Siku kuu zote zinaakisi aliyofanya / atakayofanya YESU, tena alifanya / atafanya katika siku hizo specific, mf: Siku ya kuchinja kondoo wa pasaka ndo siku Mwanakondoo wa MUNGU aliuawa. Siku ya kusherehekea mavuno ya kwanza ndo siku YESU alifufuliwa, mavuno ya kwanza ya Ufufuo wa milele.

- Sheria za vyakula ziliakisi uhitaji wetu wa kuwa safi kwa ndani / moyoni, kazi anayoifanya YESU tukimkubali.

"Naye akawaambia, “Je, hata nyinyi hamwelewi? Je, hamwelewi kwamba kitu kinachomwingia mtu kutoka nje, hakiwezi kumtia unajisi,

kwa maana hakimwingii moyoni, ila tumboni, na baadaye hutolewa nje chooni?” (Kwa kusema hivyo, Yesu alihalalisha vyakula vyote.)"

marko.7.18-19.BHN


"Kwa maana ufalme wa Mungu si kula na kunywa, bali ni haki, amani na furaha katika Roho Mtakatifu."
Waroma.14.17.NENO


Hizi ni tofauti na zile sheria za kimaadili na za haki, ambazo ni za milele. Hazibadiliki. Usiseme uongo. Usiue. Jino kwa jino. Damu kwa damu. Zinatuonyesha kuwa tumepungukiwa na utukufu wa MUNGU i.e wenye dhambi, tuko chini y viwango vya MUNGU.

"Maana hakuna binadamu yeyote anayekubaliwa kuwa mwadilifu mbele yake Mungu kwa kushika sheria; kazi ya sheria ni kumwonesha tu mtu kwamba ametenda dhambi."
Waroma.3.20.BHN

"Anayevunja amri mojawapo ya sheria, atakuwa na hatia ya kuivunja sheria yote.

Maana yuleyule aliyesema: “Usizini,” alisema pia “Usiue.” Kwa hiyo, hata ikiwa hukuzini, lakini umeua, wewe umeivunja sheria.

Yakobo.2.10-11.BHN

(BTW zamani nilikuwa namuonea Yakobo huruma kwa kupewa the wrong wife baada ya kufanya miaka 7 kwa ajili yake, nikakumbuka na yeye alimpiga baba yake fix ili apewe urithi, akimdhulumu kaka yake. Jino kwa jino? Wengine waiita Karma?)


4) Kwahiyo baada ya MUNGU kujichagulia taifa lake ili ajionyesje ulimwenguni: akawapa Sheria zake, Akafanya miujiza, akatoa unabii, na muhimu kuliko yote ndipo MUNGU mwenyewe alipoingilia kwenye ulimwengu kama Mwokozi, akiwa sehemu ya utimizo wa mamia ya unabii.


5) Alichodhihirisha Israeli ya kale tena na tena, ni jinsi wasivyo watiifu, despite yooote MUNGU aliyowafanyia.

Ungetegemea taifa alilolichagua MUNGU lijae story za watakatifu! ! Lakini ni mauzauza yamejaa kwemye Agano la Kale!

Which was the point! !

At our current state, hatuwezi kufikia viwango vya MUNGU, we are sub-par, tunahitaji msaada ili tuwe na hadhi hiyo anayoitaka, ili tufae kuishi, so far tunafaa kufa tu!

Ndomaana thoroughout kwenye mpango wake wa ukombozi MUNGU amewatumia watu ambao watu wanawaona hawafai:

Makahaba (Rahabu, Tamari)
Malaya (Samson, Solomon)
Waongo / Matapeli (Yakobo)
Wauaji (Daudi, Paulo)

Vijana wadogo / Watoto (Yeremia, Mfalme Yosia, Samueli)

Tasa (Sarah, Elizabeth)
Maskini (Ruthu, Kijakazi wa mke wa Naamani, Amosi)

Wasaliti (Petro, Yuda kaka wa Yosefu)
Waoga (Yona, Gideoni, Isaka)
Waliofilisika (Ayubu)

Waliopewa talaka (Mwanamke Msamaria)

Wasio wazungumzaji wazuri (Musa)
Wafupi (Zakayo)
Wapenda pesa ( Zakayo, Yakobo)

Matajiri (Ayubu, Abraham, Yosefu wa Arimatheya)

Wageni (Naamani msiria, Nebukadneza mbabiloni, Koreshi muajemi)

Ila throughout MUNGU ameonyesha tena na tena kile anachothamini kutok kwa hawa watu: IMANI.


6) Kipindi cha Israeli ya kale kilikuwa cha MUNGU kujifunua ulimwenguni: Yeye alivyo na mpango wake kwa binadamu.

Baada ya Muokozi kutokea, kilichofuata ni habari za YESU kusambazwa kwa mataifa mengine.

Ni kipindi cha Neema, cha Kanisa, cha mwili wa Kristo kujengwa.

I think YESU huko anatuona kama Puzzle. Kila muamini ni kipisi kimoja.

Sasa wateule wa MUNGU (Israeli) si waliozaliwa Israeli tu, si waliomkubali tu MUNGU wa Israeli na kujiunga na waisraeli (kama wale wamisri walioondoka na waisraeli baada ya mapigo 10 wakahesabiwa kama wana wa Israeli),

Bali Waisraeli wa kweli ni wale waliomkubali Mwana wa MUNGU wa Israeli, YESU.

"Tena ninao kondoo wengine ambao hawamo zizini humu. Inanibidi kuwaleta hao pia, nao wataisikia sauti yangu, na kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja."
Yohana.10.16.BHN

"Ndiyo kusema, si kila anayeonekana kwa nje kuwa Myahudi ni Myahudi wa kweli, wala mtu hawi Myahudi wa kweli ati kwa kuwa ametahiriwa kimwili.

Myahudi wa kweli ni yule aliye Myahudi kwa ndani, yaani yule ambaye ametahiriwa moyoni. Hili ni jambo la Roho, na si jambo la maandishi ya sheria. Mtu wa namna hiyo anapata sifa, si kutoka kwa watu, bali kutoka kwa Mungu."

Waroma.2.28-29.BHN

"Katika kuungana na Kristo nyinyi mlitahiriwa, lakini si kwa tohara ifanywayo na watu, bali inayofanywa na Kristo mwenyewe, na ambayo inahusikana na kukombolewa kutoka katika utu wa dhambi."
Wakolosai.2.11.BHN


7)
Kwahiyo wale wayahudi ambao walimkataa YESU na bado wanasubiri MUNGU wa Israeli alete Muokozi, je MUNGU hawatambui?

a) Kwanza umeona shift kutoka "Waisraeli" kwenda "Wayahudi"?

Lets go back.


MUNGU alichagua taifa moja akaliita Israeli. Katika kuasi kwao likaja kugeuka kuwa falme mbili: wa Kusini (Ufalme wa Yuda, wenye makabila 2) na wa Kaskazini (Ufalme wa Israeli, wenye makabila 10).

Ufalme wa Israeli ndo walikuwa wakora / wasumbufu, waabudu sanamu etc, wafalme wengi waovu walikuwa wa huko.

Ufalme wa Yuda ulikuwa na afadhali, ndo YESU alitokea huko.

i) Ufalme wa Israeli ulikuja kuvamiwa na Waashuru (700BC), watu wakachukuliwa mateka, wakapelekwa huko kwenye mataifa, wakawa watu wa mataifa. Hawakurudi.

"Kisha mfalme wa Ashuru akaivamia nchi nzima na kuufikia mji wa Samaria na kuuzingira kwa muda wa miaka mitatu.

Katika mwaka wa tisa wa utawala wa Hoshea, mfalme wa Ashuru aliuteka Samaria, na kuwachukua watu wa Israeli mateka mpaka Ashuru, baadhi yao akawaweka katika mji wa Hala, wengine karibu na mto Habori, mto Gozani na wengine katika miji ya Media.

Haya yote yalitendeka kwa sababu watu wa Israeli walimwasi Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, ambaye aliwatoa kutoka mikononi mwa mfalme wa Misri, pia waliabudu miungu mingine..."

2Wafalme.17.5-7.BHN


ii)
Ukabaki Ufalme wa Kusini wenye makabila 2: la Yuda na la Benyamini (na Walawi). Ndo wakaja kujulikana kama Wayahudi. Hata hawa waliadhibiwa na MUNGU wakapelekwa uhamishoni Babiloni (500BC) lakini walirudi kama MUNGU aliyosema watarudi baada ya miaka 70.

"Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Baada ya miaka sabini huko Babuloni, baada ya muda huo, nitawajia na kuitimiza ahadi yangu ya kuwarudisha mahali hapa."
Yeremia.29.10.BHN

Na MUNGU alitoa unabii wa wakati wa YESU kuja karne ya 1 akirejea kurudi kwa hawa Wayahudi kutoka Babyloni.


b) Baada ya YESU kuja, baadhi ya wayahudi walimkubali, ndio walikuwa wakristo wa kwanza.

Vipi Wayahudi waliomkataa na bado wanamsubiri Muokozi hadi leo?

"Ndugu zangu, napenda mjue ukweli huu uliofichika msije mkajiona wenye akili sana. Ukaidi wa Wayahudi ulikuwa ni wa muda tu, mpaka watu wa mataifa mengine watakapokuwa wamemfikia Mungu.

Hapo ndipo taifa lote la Israeli litakapookolewa,...


Kwa sababu wanaikataa Habari Njema, Wayahudi wamekuwa maadui wa Mungu, lakini kwa faida yenu nyinyi watu wa mataifa. Lakini, kwa kuwa waliteuliwa, bado ni marafiki wa Mungu kwa sababu ya babu zao.

Maana Mungu akisha wapa watu zawadi zake na kuwateua, hajuti kwamba amefanya hivyo.

Hapo awali nyinyi mlikuwa mmemwasi Mungu, lakini sasa mmepata huruma yake kutokana na kuasi kwao.

Hali kadhalika, kutokana na huruma mliyojaliwa nyinyi, Wayahudi wanamwasi Mungu sasa ili nao pia wapokee sasa huruma ya Mungu.

Maana Mungu amewafunga watu wote katika uasi wao ili apate kuwahurumia wote."

Waroma.11.25-32.BHN

"Basi, nauliza: Je, Wayahudi wamejikwaa hata wakaangamia kabisa? Hata kidogo! Kutokana na kosa lao ukombozi umewajia watu wa mataifa mengine, ili Wayahudi wapate kuwaonea wivu.

Kosa la Wayahudi limesababisha baraka nyingi kwa ulimwengu, na utovu wao wa kiroho umeleta baraka nyingi kwa watu wa mataifa mengine. Basi, ni dhahiri kwamba kuingizwa kwa idadi yao kamili kutakuwa ni baraka zaidi."

Waroma.11.11-12.BHN

MUNGU hajawakataa wayahudi jumla kwa kumkata YESU. Lakini anawaadhibu kwa kosa hilo.

"Maana mimi niko pamoja nawe, kukuokoa. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Nitayaangamiza kabisa mataifa yote, ambayo nilikutawanya kati yao; lakini wewe sitakuangamiza kabisa. Nitakuadhibu kadiri unavyostahili wala sitakuacha uende bila kukuadhibu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema."
Yeremia.30.11.BHN

Sehemu ya adhabu ni kufungwa macho wasimtambue YESU for all these years. Nao wamepitia mateso mengi. Ilibidi wahame kutoka walipokuwa huko Ulaya warudi Israeli kwasababu ya kuchukiwa na mataifa. Na hapo walipo hapapoi hapaboi, they have no peace surrounded by enemies on all fronts.

Kitendo tu cha taifa la Israeli kutokea in 1948 is part of end times prophecy. YESU alisema mambo mengi yatatokea kabla hajarudi na haiku make sense kwasababu taifa la Israeli halikuwepo.

Mfano:
i) YESU kasema akija atashukia Yerusalemu na Wayahudi watapaswa kukimbilia mahali fulani. Ingetokeaje wakati hakukuwa na wayahudi huyo Yerusalemu?

"Kisha Mwenyezi-Mungu atatoka na kuyapiga vita mataifa hayo, kama afanyavyo daima siku za vita.

Siku hiyo, atasimama kwenye mlima wa mizeituni ulio mashariki ya mji wa Yerusalemu. Mlima huo utagawanywa sehemu mbili na bonde pana sana litatokea toka mashariki hadi magharibi. Nusu moja itaelekea kaskazini na nusu nyingine kusini.

Nyinyi mtakimbia kupitia bonde hilo, katikati ya milima miwili ya Mwenyezi-Mungu. Mtakimbia kama wazee wenu walivyokimbia tetemeko la ardhi wakati wa utawala wa mfalme Uzia wa Yuda. Kisha Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, atakuja na watakatifu wote pamoja naye."

Zekaria.14.3-5.BHN


ii)
YESU akija atashuka kuwakomboa watu wake walioko Israeli watakaokuwa wamezingirwa na mataifa. Wangezingirwaje wakati hawapo huko?

"Kwa hiyo, ewe mtu, toa unabii na kumwambia Gogu kwamba mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Wakati taifa langu la Israeli linaishi kwa usalama, wewe utafunga safari....

Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema kwamba, wewe ndiwe niliyesema habari zako hapo kale kwa njia ya watumishi wangu manabii wa Israeli, ambao walitabiri nyakati zile kuwa baadaye nitakuleta upambane na watu wa Israeli.”

Bwana Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Siku ile Gogu atakapoishambulia nchi ya Israeli, nitawasha ghadhabu yangu.....

Ndivyo nitakavyofanya mataifa yote yaone ukuu wangu na utakatifu wangu. Ndipo watakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu."

Ezekiel.38.14-23.BHN


iii)
YESU akirudi Wayahudi walioko Yerusalemu watamlilia YESU, yule waliyemuua miaka 2000 iliyopita. Itatokeaje kama hawapo huko?

"Wazawa wa Daudi na wakazi wa mji wa Yerusalemu nitawajaza roho ya huruma na maombi, nao watamtazama yeye waliyemtoboa; watamlilia kama mtu amliliavyo mtoto wake wa pekee, au kama mtu amliliavyo kwa uchungu mzaliwa wake wa kwanza.

Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu mjini Yerusalemu kama maombolezo ya kumwombolezea Hadad-rimoni katika mbuga za Megido."

Zekaria.12.10-11.BHN


Na YESU kasema haji hadi Wayahudi wamlilie. Watalia bila sababu? Hawa Ndugu zetu watapata kichapo heavy, trailer 7 October, 2023. Ule utungu wa kuzaa aliosema YESU ulishaanza. Do you see it?

Uzuri Wayahudi wamepamba moto kumtangaza Masihi, huwa nacheka nikipita comments kwenye video zao ni wakristo wamejaa huko. This is why it makes sense kwanini watamuitia YESU, Christians will have done their job.

"Yerusalemu! Ee Yerusalemu! Unawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako. Mara ngapi nimejaribu kuwakusanya watoto wako kwangu, kama vile kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka.

Haya basi, nyumba yako itaachwa mahame.

Nakuambia, hutaniona tena mpaka wakati utakaposema: ‘Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana."

Mathayo.23.37-39.BHN


By the way nikisema Wayahudi wa Israeli naamini ni hawa:


View: https://youtu.be/6kVIOOOBFqQ?si=PdfbhSyO3sPrZLva



View: https://youtube.com/shorts/4N97m8E5r0s?si=lgcOywXq69hdCEXN


Sio serikali yao ambayo ni secular, hawajaifanya Torah kuwa katiba yao. Naamini MUNGU anatumia kuwalinda watu wake.

Wala si wale wanaonekana kwenye magwaride ya mauzauza huko Jerusalem, sio wayahudi. Inawezekana ni hawa:

"Theluthi mbili za watu katika nchi zitaangamizwa; ni theluthi moja tu itakayosalimika.

Theluthi hiyo moja itakayosalia, nitaijaribu na kuitakasa, kama mtu asafishavyo fedha, naam, kama ijaribiwavyo dhahabu. Hapo wao wataniomba mimi, nami nitawajibu. Nitasema, ‘Hawa ni watu wangu’, nao watasema, ‘Mwenyezi-Mungu, ndiye Mungu wetu.’"

Zekaria.13.8-9.BHN


8) So WHO IS ISRAEL?


  • Wayahudi (Ufalme wa Kusini) wapo.
  • Ufalme wa Kaskazini ulipotea kwenye mataifa.
  • Tumeambiwa hadi watu wamataifa wamjue YESU ndipo Wayahudi watamtambua pia.

WHO IS ISRAEL?

"Wewe mtu! Chukua kijiti kimoja, uandike juu yake maneno haya: ‘Kwa Yuda na Waisraeli wanaohusiana naye.’ Kisha chukua kijiti kingine, uandike juu yake maneno haya: ‘Kwa Yosefu (kijiti cha Efraimu) na Waisraeli wanaohusiana naye.’

Halafu vichukue vijiti hivyo na kuvishikamanisha ili vionekane kama kijiti kimoja.

Wananchi wenzako watakapouliza, ‘Je, hutatueleza maana ya jambo hilo?’

Wewe utawajibu, Bwana Mwenyezi-Mungu asema hivi: Nitakitwaa kijiti cha Yosefu (kilichomo mkononi mwa Efraimu) na makabila ya Israeli yanayounganika naye, nami nitakishikamanisha na kijiti cha Yuda ili vijiti hivyo viwili vifanywe kijiti kimoja mkononi mwangu.

Ukiwa mbele yao huku umeshika vijiti ulivyoandika juu yake,

waambie kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Nitawatoa Waisraeli kutoka mataifa walikokwenda; nitawakusanya toka pande zote na kuwarudisha katika nchi yao.

Nitawafanya kuwa taifa moja
katika nchi juu ya milima ya Israeli; mfalme mmoja atakuwa mfalme wao wote. Hawatakuwa tena mataifa mawili wala hawatagawanyika tena kuwa falme mbili.

Hawatajitia unajisi tena kwa sanamu za miungu yao na kwa mambo yao ya kuchukiza wala kwa makosa yao. Nitawaokoa wasiwe tena waasi. Nao watakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wao.

Mtumishi wangu Daudi atakuwa mfalme wao; naam, watakuwa na mchungaji mmoja tu. Watayafuata maagizo yangu na kuzingatia kanuni zangu."

Ezekiel.37.16-24.BHN

Ezekieli imeandikwa Daudi ameshakufa siku nyingi, so ni future prophecy ya yule Mwana wa Daudi atakayekuwa Mfalme i.e YESU.


MUNGU ataunganisha tena falme mbili za Israeli:

Kijiti cha Yuda ni Wayahudi (Ufalme wa Kusini)
Kijiti cha Efraim Wakristo (Ufalme wa Kaskazini uliopotea kwa mataifa)

Israeli ni moja tu: Wote wanaomkubali MUNGU wa Israeli na Mwanaye YESU.

Tunawatetea kwasababu ni ndugu zetu waliotiwa upofu kwa muda kwasababu ya uasi wao: kumkataa YESU.

Tunawatetea wayahudi kwasababu muda umefika wa wao kumuitia YESU.

Tunawatetea kwasababu ni utimizo wa Ezekieli 37 LIVE: falme mbili zilizogawanyika zinaunganishwa in real time.
 
Back
Top Bottom