Hivi kwanini wasanii (mfano MC Pilipili) huuziwa magari bei juu kuliko watu wengine?

Hivi kwanini wasanii (mfano MC Pilipili) huuziwa magari bei juu kuliko watu wengine?

Kwani bei za magari ya mtumba zinafanana? Mmoja akinunua vitz ya 10mil sio lazima wote wanunue kwa bei hiyo.

Bei za magari zinatofautiana, japo zaweza kuwa mwaka mmoja, i.e 2010, inawezekana sana moja likauzwa $2000, na lingine likauzwa $5000.
Kweli kabisa sababu inategemea na gari imetembea kilometer ngapi pia sababu huwezi fananisha bei ya gari iliyotembea km 100,000/= na gari iliyotembea km 20,000/=
 
Jana nimeshangaa kumsikia MC Pili pili akijidai kuwa ameuziwa gari aina ya BMW X3 kwa zaidi ya sh milioni thelasini, wakati mimi nikipiga garama za kuagiza hiyo gari wala hata hazizidi milioni ishirini na mbili.
Ya MC ni toleo la mwaka gani na yakwako unayotaka kuagiza ya mwaka gani...ebu tupe specifications zote za ya kwako na ya MC, huku wadadisi tuchunguze wenyewe kama kuna ukweli kwenye hoja yako. Pia tuambia na mlolongo mzima wa kupata hiyo gari....!!
 
Bei za magari hazifanani hata siku moja. Inategemea na muuzaji wa gari, na condition ya gari husika. Unaweza kukuta huyo MC Pilipili amenunau gari ambayo ni 0 km au ipo low millage, wakat wewe hiyo yako ya milion 22 imetembea millage za kufa mtu!!!
Ila hata kwa kuiangalia (you tube) sio ya sifa unazozitaja mkuu
 
Mimi hua sielewi pale ninaposikia eti msanii fulani kanunua gari JIPYA! wakati ukilitizama gari lenyewe sio jipya! Yaani mpaka magazeti huandika mfano Ali kiba/Diamond anunua ndinga mpya,ila gari ni used!!!!

Sasa sijui kusema gari "Jipya" hua wana maanisha nini?!
Yaan wanamaanisha jipya kwao mwanzon hakuna nalo.
 
Una uhakika gani kama bei aliyotaja ndo aliyonunua.!?
 
BMW X3 zipo model nyingi so inawezekana kununua kwa bei hiyo.

Kuna X3 ambazo ni ///M Sport version.

Zipo X3 za hivi karibuni kuanzia 2010 bila M60 hupati.

Pia kama gari yake ipo Modified sana na kit za taa suspension seat engine mods etc possible.

Ila kama ni stock X3 generation ya kwanza bei yake haifiki huko unless amelaliwa.
 
Mimi najiuliza pia why kila msanii anaona BMW??
Sifa kuu ya msanii ni kutaka attention za watu na kuonekana tofauti na sisi watu wa kawaida.

Msanii kumiliki gari za Japan wanahisi tutawaona wa kawaida tu. Unless wanunue madude kama LC J200 ambazo bila M70 hupati.

Option pekee ni Germany kwa Audi BMW au MBenz.

Wangeenda Italy kwa wakina Ferrari Lamborghini Maselati Porsche etc ila bajeti inakaba.

BMW ni affordable kiasi ku run na maintenance.
 
Back
Top Bottom