Hivi kwanini wasomi wa Tanzania wanaamini kuajiriwa ni Serikalini tu?

Asikudanganye mtu ndugu yangu serikalini patamuuu haswa haswa !!! Sector binafsi ni shida tupu tupu tupu uliza uambiwe !!! Serikalin pesa ni ya uhakika kuliko sector binafsi!!! Serikalini walim walio fundisha muda wako juuu sana mshahara mfano aliyefundisha 10 years plus anaongelea G ambaya nafikiri itakya 1600,000/ per month !!! Nani sekta binafsi atakulipa hiyo!??
Watu wanakopa benk mpaka 40,000,000/ wapi sector binafsi ataruhusi hiyo!?? Bima za afya kwa familia nk !!! Watu wanapigwa kiinua mgongo mpaka 150,000,000/
Na bado monthly pension 800,000/ kila mwezi mpaka ufe na kutibiwa bure mpaka ufe!!! Nani mwenye akili atakataa hilo!!??
Private ni mavi takataka asikwambie mtu !!! Uliza private gani inaweza lipa mwalimu hata 1200,000!?? Zipo ngapi!!???
 
Nenda ukaulize kama hizo ofa zipo tena ndugu hali ni mbaya private schools asikudanganye mtu
 
Mimi nilimaliza chuo 2000 nikavimba kichwa nikaenda private sector kufika 2014 nilikimbilia serikalin baada ya kuona ubabaishaji sector binafsi!!? Kwa kifupi najuta wenzangu walioingia gvt wanazungumzia mshahara wa 1.8/m mm ndo kwanza naongelea 960,000/ yani najuuuuuuuta !!! Ni nani sekta binafsi anaweza lipa mtu wa diplama hivyo!?? Mnaongea msicho kijua
 
Niko sector binafsi mwaka wa 9 huu ila sio kwenye ualimu, na wala sijawahi kujitoa kwakweli. Naona maisha yangu yako Safi na kama ni salary inapanda hata enzi zile serikali haipandishi kwa wafanyakazi wake.
Benefits zipo nyingi tu, km bima ya afya, housing allowance, air time allowance, staff development, promotions za hapa na pale, mwajiri katufanyia mambo ukitaka kukopa anakuwa mdhamini wake, napata social security fund
So, inategemea kwakweli. Sio sekta binafsi zote Ni majanga.
 
Wapinzani ndiyo wanawapoteza vijana kwa kuwajaza huu upuuzi ili waichukie serikali iliyo madarakani. Cc Erythrocyte
 

Wengi kinachotupeleka serikalini ni opportunities za kuiba. Mtu akikwambia Kitu kingine ni muongo huyo.
 
Serikalini hamna kufukuzana kama unafukuza malaya ndani kwako! Ila sekta binafsi hutegemea na boss kaamka na kisirani kiasi gani!

Benefits ni nyingi serikalini kwa title ya mtumishi wa umma kuna privilege kibao wala huwezi compare!
 
Kumbe unakubali kuwa private nyingi ni majanga!
Asante kwa kushiriki
 
Nadhani ungeulaumu Kwanza Mtaala wa Elimu wa Tanzania ambao unauandaa Ubongo wa Msomi wa Kitanzania kuwa Tegemezi, asiyejiamini na hata Kujielewa pia tofauti na Mitaala ya Elimu ya Mataifa mengine ambayo humuandaa Candidate kuwa Pro Active and Creative hadi hata kuweza Kujiajiri Mwenyewe.
 
Ungeonesha mfano kwanza wewe mtoa mada!
Wewe uko serikali hutaki kuacha kazi serikalini halafu unawaaminisha wengine kuwa hapo ulipo serikalini ni pabaya kuliko upande wa binafsi!
Unaambiwa uache kazi uoneshe mfano unasema eti ...
"NIKIPATA KAZI PRIVATE NAACHA KAZI YA SERIKALINI"____

Wewe hapo upo kwenye ajira tayari kwa kipindi fulani na angalau umepokea vihela kadhaa LAKINI hujiamini kama unaweza kukaa bila ajira katika kipindi ambacho utakuwa huna kazi unatafuta sehemu ya kupigia kazi ...
Halafu unamwambia kijana ambaye hana ajira amepambana kutafuta ajira kwa miaka kadhaa mfano 3++ bila mafanikio kuwa ajira zipo nyingi private na kuwaambia wasitamani kuja serikalini!

..Hujui unachoongea mkuu,, wahenga husema kitanda usichokilalia hujui kunguni wake...
.

Kama kweli unaamini katika mantiki ya mada yako basi fanya hivi:-
Acha kazi, baki bila ajira halafu ungana na watafuta ajira katika sekta binafsi! Halafu rudi hapa kuja kuandika tena.
Hapo ndipo tutaelewana vizuri
 
Mada haihusu kujiajiri wee jamaa
 
Ahsante sana Ndugu you said it all.Tangu Mwaka 2015 nilikuwa sector binafsi lakini yalionikuta nilijuta kwa nini nilikataa kwenda kureport ajira yangu serikalini mwaka 2017.

Nilifukuzwa kazi nikiwa nina week 2 kwenda kufunga Ndoa.

Sa hivi nipo Serikalini nina peace of mind japo mshahara sio wa kufanyia Anasa kwa kuwa ni kiduchu.
 
Watu ni wavivu kufanya kazi, sekta binafsi unapigika balaa, serikalini hata uwe mlevi wa kulewa siku nzima na kazi unafanya kwa kusuasua utaendelea kuwepo na mshahara pale pale. Hiyo ndo security ambayo wengi wanaitaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…