Hivi kwanini wasomi wa Tanzania wanaamini kuajiriwa ni Serikalini tu?

Private jobs hakuna security of employment. Wakati wowote unaweza kufukuzwa kazi. Mfano mwaka jana kipindi cha corona wengi waliachishwa kazi na hawajarudi kazini. Najua mtu mpaka leo anahangaika hajapata kazi. Kungkuwa na security nadhani watu wangeprefer kuajiriwa huko. Serikalini hakuna aliyefukuzwa na waliendelea kulipwa mishahara. Serikalini mpaka ufukuzwe ni process ndefu. Kwenye sekta binafsi unaajiriwa kwa mkataba wa miaka michache sana miwili nadhani. Mtu anataka akipata kazi iwe ya kudumu e.g unakaa 30 yrs na hata pensheni itakuwa nzuri. Ila kwa sasa fursa ni nyingi za kujiajiri. Tatizo kuijua hiyo fursa na nadhani mtaji pia ni tatizo. Wasomi wanaweza kujiajiri.
 
Acha upotoshaji ( uchochezi )
Watu ni wavivu kufanya kazi, sekta binafsi unapigika balaa, serikalini hata uwe mlevi wa kulewa siku nzima na kazi unafanya kwa kusuasua utaendelea kuwepo na mshahara pale pale. Hiyo ndo security ambayo wengi wanaitaka.
 
Watu ni wavivu kufanya kazi, sekta binafsi unapigika balaa, serikalini hata uwe mlevi wa kulewa siku nzima na kazi unafanya kwa kusuasua utaendelea kuwepo na mshahara pale pale. Hiyo ndo security ambayo wengi wanaitaka.
Nayo ni faida kwani unapenda upunda
 
Kwa tuliofanya kazi sector binafsi na sasa tupo serikalin tunajua shida ya sector binafsi mshahara tarehe 50 ,bima za afya za kubumba ,full kubanwa na kufuatiliana fuatiliana hata kama serikalin mshahara pungufu wa ule wa mwanzo ni heri nipate hii 300k ya uhakika kuliko 500k ya masimango
 
Kuna mtu wangu wa karibu anapokea 800k Take home 580k Bonus za katikati ya mwezi za kutosha ..yaani inafika mpaka milioni moja ukijumlisha na mshahara .. kasoma diploma pekee,
Shirika binafsi.. ety kwa shinikizo la wazazi kaaply ajira za serikali.. namwangalia nacheka hihiii...
Hivi nurse ngazi ya diploma serikalini analipwa Tsh ngapi vile?
 
Haya madogo yanadanganyana.
Neno "security ya kazi" bado ni msamiati kwao.
 
Ni kwasababu serikalini kuna job security.

Private companies ni nzuri ila mikataba yao ni mifupi

Na haina guarantee kama kampuni ita renew mkataba na wewe pindi mkataba wako unapoisha
 
Kwa sababu hata wewe ni Kati ya wajinga sambamba na hao wasomi kwa sababu huelewi changamoto za mfumo wa.elimu walioupata.
 
Tsh 680,000 Gross
 
wewe acha huko njoo huku private sector sisi tuje huko..
 
Pole sana
 
Sekta binafsi kuna ile kitu bosi akiamka vibaya tu hauna chako pale na pia hizi sekta binafsi zina yumba kiuchumi unashangaa umepunguzwa na wengi wa wasomi hatupendi njia zingine za kujipatia kipato ukishaajiriwa basi umemaliza unatulia unategemea mshahara tu
 
Taja wapi!!! ???
 
Utapanda tuu wala usihofu mambo yatakaa sawa tuu!!!ukiona MTU anatetea sekta binafs hasa hizo shule zao jua huyo ni kiherehere mzoefu
 
Ukiona MTU anafagilia sekta binafsi jua huyo ni kiherehere mzoefu
Wakujipendekeza kwa bosi
Wapo wengi sana hasa shule binafsi hakufai
 
Kazi kubwa ya serikali sio kudhibiti sekta binafsi bali kuitengeneza mazingira mazuri iweze kuwa na ushindani wa wafanyakazi ili waweze kulipwa vizuri.

Kutajirikia katika ajira yoyote ni jambo gumu sana sio sekta binafsi tu hata serikalini ni hivyo hivyo. Wengi wanotajirika serikalini ni wezi na mafisadi na kwa sababu sio rahisi kuwajibishwa serikalini ukifanya ufisadi tofauti na kwenye kampuni binafsi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…