Hivi kwanini wasomi wa Tanzania wanaamini kuajiriwa ni Serikalini tu?

Na kuiba serikalini ni rahisi zaidi pia kuliko sekta binafsi.
Serikalini hamna kufukuzana kama unafukuza malaya ndani kwako! Ila sekta binafsi hutegemea na boss kaamka na kisirani kiasi gani!

Benefits ni nyingi serikalini kwa title ya mtumishi wa umma kuna privilege kibao wala huwezi compare!
 
Tatizo kubwa ni mfumo wa elimu yetu,

Tunasoma ili tuwe akina Nani, toka utoto tulishaanza kuaminishwa na wazazi, walimu, rafiki na jamaa wanaotuzunguka kuwa mafanikio ni kuwa na kazi serikalini na walimu wengi wanajivunia tulimfundisha Fulani leo ni katibu Mkuu/mkurugenzi wa wizara au taasisi Fulani kitu ambacho kinajenga mwelekeo wa wahitimu.


Njia nzuri ni Serikalini kuja na mtaala ambao umejikita zaidi kwenye ujasiriamali na ubunifu ili kuwajengea uwezo na Nia ya Kila anayehitimu kuwa na akili ya ubunifu fulani au ujasiriamali/ufanyabiashara na ajira ya Serikalini au taasisi binafsi iwe chaguo la mwisho hapo tutakuwa na Tanzania tunayoitamani.
 

Trust me
Nilichokiandika hujaelewa kabisa
 
Kwahiyo tunakubaliana kuwa Tanzania hakuna Tatizo la ajira isipokuwa watu hawathamini ajira kwenye sekta binafsi.
 
Sawa lakini hapa point kubwa ya mleta mada ni kuonesha kuwa TZ hatuna sana tatizo la ajira ila tunataka ajira ya aina moja tu serikalini tu. Waganda na wakenya wanalilia hizi fursa sisi tunazikimbia kwa sababu serikali inatudekeza sana.
 
Akiingia serikalini ataambulia laki tano na ushee baada ya makato. Na kibaya zaidi atatupwa vijijini ndani baada ya muda mfupi atakumbuka alipotoka.
 
Serikalini Kuna faida kuu tatu;

1. Usalama wa ajira, mtu hawezi kuwa terminated TU at the will ya mwajiri, Kuna taratibu za kumwajibisha mtumishi, private sector pia zipo Ila hazizingatiwi kama serikalini.

2. Fursa za elimu; serikalini ni rahisi kujiendeleza kielimu kuliko private sector.

3. Mikopo; kwakua serikalini Kuna usalama wa ajira, ni rahisi Kwa Taasisi za kifedha kumpatia mtumishi mkopo ukilinganisha na mwajiriwa mwingine.
 
Swali lako kimsingi kulijibu inatakiwa ufanye utafiti juu ya trend ya ajira hapa nchini.

Na ukifanya hivyo unaweza kuta shida kubwa ilianzia awamu ya tano ambapo;

1. Serikali iliacha kuajiri kama ilivyokuwa hapo awali

Hivyo kusababisha out flow kuwa si sawa na inflow

2. Serikali ilichangia kuua sekta binafsi ambayo ilichangia kuchukua baadhi ya wahitimu.

4. Elimu bure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…