Hivi kwanini watu wapole wako hivi?

ni kweli kaka,mimi ni mmoja wao. siwezi kukaa na mdada zaidi ya siku tano,ntakuwa nshajua hii chenga so sihitaji endelea nayo. japo si sheria mawazo yng
 
Hapo mkuu naomba tusaidiane kidogo kuwatofautisha kama hutajali
Tunaomba ufafanuzi hapa mkuu
Mtu mpole.
Wanafikiri sana kabla ya kutenda na sio wakurupukaji, na nirahisi kuwaamini na pia wako tayari kutoa msaada.
Watu hawa ni wazuri kuwa nao kama marafiki, na wasikilizaji wazuri ambao wanazielewa hisia za wengine.
Wapole wanaweza kudumisha mahusiano yao na wengine na ni rahisi kukaa kwenye uhusiano kwa muda mrefu, na niwagunduzi wa vitu.

Kuna dhana kwamba Watu wakimya wana dharau kutokana na kwamba wakati wewe unaongea kwa mdomo, wao wanatabia ya kuongea kichwani mwao.
Pia inasadikika kwamba unapo ongea naye mara nyingi anaweza asijibu kwa maneno bali vitendo na pia anadaiwa kutosahau haraka alichoambiwa.
 
Kuna wapole na wakimya. Wengi wanadhani wakimya ni wapole na waongeaji ni machakaramu ila wakishashangazwa ndio akili inarudi

Japo wakimya hata mimi nawaogopa maana unaweza fanya jambo na asitoe any reaction kumbe ushawekwa kwenye plan za mbeleni
 
Ni kama asili tu ya wapole kama mimi huwa wadada ninaodate nao wanasemaga sura yangu muonekano na moyo wangu ni vitu tofauti sana.
Sababu mimi ukinikorofisha nakuacha na huwa sina tabia ya kurudia, nikiacha nimeacha hata uje na magoti au unatambaa.
 

🙆‍♀️🙆‍♀️🙆‍♀️Nawazungumzia wote kwa pamoja.
 
Kuna Movie Moja hivi niliangalia mwaka jana, (2019) inaitwa "Plus One". Ni love story flani hivi imechangamka. Anyway ngoja niende kwenye point..

Kuna Jamaa huko anaitwa Ben, kaigiza kama introvert flani hivi (aina ya watu unaowasemea hapo juu, wapole). Kuna mahali aliulizwa swali na bestie yake, Alice kuwa kwanini anashindwa ku date muda mrefu (or kudumu kwenye mahusiano)?

Nafikiri jibu alilotoa linaweza ku fit kwenye huu uzi..

Alisema "Watu wa aina yake (wapole) huwa sio rahisi sana kuwa kwenye mahusiano kwa sababu ni ngumu sana kuwazoea (especially wanaume), kwaiyo hii inawafanya wawe Single kwa muda mrefu sana. Sasa kuwa Single kunawafanya wajijue zaidi, kunawafanya wajue ni vitu gani hasa wanahitaji kwenye mahusiano. Kwaiyo hii inawapelekea kujua kwa haraka zaidi kuwa mtu wanayekutana nae hafai au hataendana naye kwenye mahusiano, na hapotezi muda akishagundua hilo, anaamua kuachana naye tu."

Nadhani hiyo point ina ukweli ndani yake kulingana na uzi wako!
 
Ni ukweli kwa kiasi kikubwa sana, mtu mpole akiamua kukupenda huwa kamaanisha hana ukinyonga.

Ila pia ukimzingua akaamua kufanya revenge hamna rangi utaacha ona maana analipiga tukio kwa ustadi na umakini bila kukurupuka.
 
Mkuu umejibu swali nililojiuliza mda marefu kwamba Mimi Ni mkimya au mpole nimegundua sina sifa za upole ila Nina saifa za ukimya ila huwa hatuna dharau kama mnavotuchukulia sema tu huwa hatuna maneno ya kuongea matokeo yake ndo tunaonekana tuna dharau ila huwa hatusahau haraka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…