Hivi kwanini watu wapole wako hivi?

Jf ni kisima cha maarifa.....[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hatuna matukio bhana, ni kwamba ukiwa ukiwa mkimya unampa nafasi mtu wako afunguke zaidi hivyo unakuwa ushamsoma mwenzio nje ndani. Sasa uchakataji wa taarifa wa mtu mkimya unaishia kichwani kwake tu na ni ngumu kuonesha reaction kama ameshangazwa au kushituka kwa taarifa yoyote utakayo mpa au story yoyote. Hivyo utajikuta unamsimulia story nyingi hususani madhaifu na mengine mengi maana watu wakimya ni wasikilizaji wazuri. sasa akishapata hizo story ndio anajitoa ghafla tu na hatatoa sababu za msingi kwanini anasitisha mahusiano. Atakuacha tu juu kwa juu sasa hiyo ndio inachukuliwa kama ukatili au hayo matukio ya kutisha ila kimsingi mtu mkimya hawezi kukueleza wazi udhaifu/kosa lako. Atajiondoa tu kwenye maisha yako ghafla.
 
Wapole au wakimya, maana kuna watu ambao ni waongeaji lakini ni wapole.


Ngoja nikusaidie tu , watu wengi hasa wanawake wanachanganya kati ya watu wakimya na wapole.

Upole ni tabia ya ndani, ambayo inatafsiwa Kwa MTU kuwa na huruma, caring na upendo. Na kinyume cha upole ni ukatili.

Na kuna ukimya maana sio muongeaji. Kinyume cha mkimya ni muongeaji.

Kuna watu wakimya halafu wapole pia. Lakini kuna watu wakimya halafu ni makatili. Hawana huruma, upendo na sio caring.

Pia kuna watu waongeaji lakini wapole pia.


Watu wengi wanaingia chaka Kwa kushindwa kujua jambo hili wanapochagua wenza wao, Mara nyingine unaingia Kwa MTU mkimya lakini sio mpole unaishia kuchezea kichapo. Unakuta MTU huyo anakuwa mafia, mwenye tabia mbaya, asiyejali kabisa ila ndio hivyo sio muongeaji.
 
Hata sisi hatujui kwanini tupo hivyo
 
Hawa wengi wao hubadlika na kuwa mafirauni baada ya kuonewa maana mapenzi ya kibongo ukiwa lonyalonya kila Siku unalia wewe tu
Duh,kumbe watu ndo wanawafanya wawe hivi
 
Shukrani sana mkuu kwa maelezo yako
 
Mambo ni kimyakimya mwisho wa siku mtu anashtuka kaachwa
AISEE😄😀
 
ni kweli kaka,mimi ni mmoja wao. siwezi kukaa na mdada zaidi ya siku tano,ntakuwa nshajua hii chenga so sihitaji endelea nayo. japo si sheria mawazo yng
Mchezo unaisha mapemaa,
Kila mtu anashuka hamsini zake🏃🏃
 
Akhsante sana mkuu kwa maelezo yako yakinifu,
Kweli Jf ni kisima cha maarifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…