Hao waliomo ndani ya vyama hivyo unavyoviita magenge ndiyo kila siku wanateswa, wanauawa, wanazuiwa kufanya mikutano ya hadhara, vyama vyao vinaingiliwa kila siku na msajili wa vyama vya siasa, wakishiriki chaguzi wanaporwa ushindi wao, hao watanzania wenzako wanaofanyiwa kila aina ya ufidhuli ni binadamu kama wewe, inakuwaje wewe unaona sawa. hizo ni akili timamu kweli?
Ndugu yangu
Allen Kilewella, Tanzania iliwahi kuitwa kisiwa cha amani nyakati fulani. Sifa ya Tanzania ilijulikana huko nje hadi watoto walipozaliwa wazazi waliona fahari kuwapa majina ya Kitanzania.
Mtanzania aliheshimiwa na katika nchi nyingi hukuhitaji hata hiyo viza kuingia. Ilikuwa ukionesha pasipoti ya Tanzania tu mlango unafunguliwa uingie uendelee na shughuli zako bila bughdha.
Hivi sasa inabidi Rais wa nchi ashiriki katika filamu inayoitwa Royal Tour eti kuitangaza Tanzania.
How did we sink this low? What happened in between? Jibu ni rahisi sana, taifa letu pendwa limetekwa!
Wengine wetu tukikumbuka zama hizo tunajikuta tunalia na kutoa machozi. Lipo genge limeiteka nchi yetu na hivi sasa wengi tunaishi ndani ya taifa letu kama mateka...genge hilo si lingine bali CCM!
Sasa hivi iko sera isiyo rasmi inaitwa jaribu uone...
likosoe hilo genge uone cha moto. Wapo ndugu zetu wamemwagwa mitaani na mtandaoni kama huyo
Jay One, Mtanzania anatishwa na kuwindwa kama nguchiro ndani ya taifa lake!
Kosa? Kudai haki, kudai usawa, kudai uhuru wa mawazo, kuikosoa serikali yetu wenyewe Watanzania, kuwakosoa viongozi watumishi wetu, kupinga uonevu katika sura zake zote, kudai utawala wa sheria na kudai Katiba mpya.
Ukiwa na akili timamu huwezi kuishabikia CCM!