Hivi kweli kuna watu wanapona kwa maombi?

Jiulize kama maombi yanaponyesha kwanini wagonjwa wakiumwa wanakimbilia hospital badala ya kanisani au msikitin
Ukiona mtu anaombewa ujue ana ugonjwa wa akili tu
 
Jiulize kama maombi yanaponyesha kwanini wagonjwa wakiumwa wanakimbilia hospital badala ya kanisani au msikitin
Ukiona mtu anaombewa ujue ana ugonjwa wa akili tu
Sure mkuu. Nikiwa mtoto niliwahi kumuuliza Bimkubwa mmoja ambaye alikuwa Mwalimu wangu wa sayansi. Mwalimu huyu alivunjika mguu.
SWALI:
Mwalimu mbona sisi tukiugua unatwambia twende hospitali kisha tulete vyeti shuleni, lakini wewe umevunjika mguu na huendi hospitali unaombewa tuu je utapona bila kula dawa? ALIISHIA KUPATA KILEMA CHA KUDUMU KWA UZEMBE WAKE. Namimi niliangukia kichapo kila akiikumbuka SWALI LANGU Hadi Nika hamishwa shule!
HAKUNA ALIYE WAHI PONA TATIZO LINALO ONEKANA KWA MAOMBI!
 
Mimi pia nimepona kwa maombi na si siku nyingi ni jana tu! Na ni maumivu nilikuwa na yasikia kabisa ila yakaachia kabisa! Namtukuza Mungu juu ya uponyaji huo
Mkuu hayo yasiyo onekana Sina Shaka nayo yanapona ila YANAYO ONEKANA BILA SHAKA YOYOTE HAYAPONI!!!!!!
 
Labda niseme kwa ueleo wangu unazungumzia DINI ipi na Mungu yupi hapo ndio tuje kwenye maombi yenyewe,kumbuka DINI ya Mwenyezi Mungu ni Moja na Mitume wake wote walikuwa DINI Moja na ndiyo Maana hakuna Mtume aliyekuja akampinga mwenzake zaidi ya kuendeleza alipoishia Mwenzake.
Na hakuna Mtume aliyefanya muujiza kwa jina lake,yaani walifanya kwa kumuomba Mwenyezi Mungu. Sasa hapo ndipo tunapokuja kwenye ukweli hayo maombi ni kwa Mungu yupi? Ukisema kwa jina la Mtume Muhamad unakosea au kwa jina la Yesu, wewe muombe Mungu wako aliyekuumba
 
Kaka yangu alipona, alianza kuumwa macho akiwa form one. Alikua anatumia miwani alivyofika form four macho yakagoma kabsa kuona hata kwa miwani. Jumapili moja alikuja kuchukuliwa na mchungaji wa kanisa fulan la kilokole. Siku hiyo alirudi anaona vizuri. Nilichojifunza
1. Maombi yanaponya maradhi Ila hasa maradhi ya kurogwa.Maradhi yanayoingia mwilini kiroho Kama kurogwa hayawez kutibiwa hospital, maombi ndio suluhisho

2.Imani kwamba Mungu atakuponya ni muhimu sana, Kaka yangu yule alikua haamin kbs ktk maombi. Sisi ni wakatoliki hivyo bro alikua haamin kbs makanisa mengine. Alikua akisisitiza maneno ya kanuni ya Iman" nasadiki kwa kanisa moja takatifu katoliki la mitume" hivyo tulikua tukimlazimisha kwenda kuombewa bila yeye kupenda na hakupona. Siku aliyopona aliamua mwenyewe kwenda kuombewa na aliondoka home anasema anakwenda kuona.

3. Kama umeponywa maradhi ya kichawi inabidi uwe karibu Sana na Mungu Kwan wachawi wataendelea kukusumbua. Ndugu yangu huyu aliendelea kusumbuliwa na wachawi. Alikuja kupata homa Kali akakimbizwa akalazwa hospital Ila ajabu asubuhi yake hakuwepo hospital akaja kuokotwa porini akiwa hoi na akafariki akiwa anarudishwa hospital. Yapo matukio mengi kwake yalomkuta mpaka tukahis anarogwa, sijayaandika hapa.

4. Kuna nguvu kubwa Sana ktk maombi. Nikiwa darasa la 3 nilipoteza viatu shule, tulikua tunavua na kuweka uwanjan Kama magoli ya mpira baada ya mchezo sikuvikuta viatu vyangu. Mama akagoma kuninunulia viatu. Usiku ule nilisali Sana rozali nikamuomba Mungu anisaidie. Asubuhi nilitoka home pekua njiani niliokota elfu kumi. Nikanunua sendoz nikaenda nazo shule na Jumapili mnadani nikanunua viatu. Mara nyingi nilikua nikipata shida naomba na Mungu anajibu. Ila nilipoanza tabia ya kugongana na Mungu akaacha kunisikiliza mpaka leo. Mambo yakitulia ntarudi kanisani kwa nguvu zote.
 
...ukisikia story inaanza 'kuna jamaa flani'! Ujue tayari ni fake !
 
daaaaaaa,nimecheka sana
 
Labda ungeumwa ukaombewa usingepona ukaleta ushuhuda,ningekuelewa.Lakin hujaumwa unapinga nini?
 
Jiulize kama maombi yanaponyesha kwanini wagonjwa wakiumwa wanakimbilia hospital badala ya kanisani au msikitin
Ukiona mtu anaombewa ujue ana ugonjwa wa akili tu
Katika ulimwengu wa roho na msalaba wa kuzimu, tambua kuna magonjwa ambayo chanzo chake ni kutoka msalaba wa kuzimu. Magonjwa haya huwa ni halisi kabisa kama pressure, kisukari na hata tatizo ambalo linakuwa sugu bila kutibika (sio kama maleria, nk) hivyo basis magonjwa haya yaliyotokana na msalaba wa kuzimu huponyeka kirahisi kwenye maombi, kupitia kwa imani yako, na mtumishi wa Mungu wa kweli!!
Pia magonjwa mengine ambayo ni hayo hayo kwa mapenzi ya Muumba yanatibika ila sio kwa imani haba
 
Hayo magonjwa ya msalaba ya kuzimu hata kama yapo lakini yakishaonyesha dalili za magonjwa ya kawaida ni ngumu kupona kwa maombi ukiona umeenda hospitali na vipimo vikaonyesha huna kitu na ww bado hujisikii vizuri haimanishi umerogwa hii science bado vitu vingi haijui mfano ugonjwa kama shizophrenia medicine inashindwa kutambua why katika ubongo kunakuwa na abnomal neurons sign inayopelekea mtu kupata halllucination na delusion
Kushindwa kwa science kuelewa pathophysiology ya ugonjwa wa shizophrenia haimanishi huyu karogwa au ana mapepo ugonjwa kama huu mtaan watasema karogwa
 

Of all names bro you chose Iblis[emoji23]
 
Jaman watu wanapona kuna jamaa nilikuwa nasoma naye alikuwa na tatizo la kigugumizi kipindi chote tukiwa tunasoma naye lakini aliombewa akapona kabisa
 
Maradhi ya kutupiwa yanapona kwa maombi, ila kama ni Malaria wewe kunywa tembe za dawa sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…