Sure mkuu. Nikiwa mtoto niliwahi kumuuliza Bimkubwa mmoja ambaye alikuwa Mwalimu wangu wa sayansi. Mwalimu huyu alivunjika mguu.
SWALI:
Mwalimu mbona sisi tukiugua unatwambia twende hospitali kisha tulete vyeti shuleni, lakini wewe umevunjika mguu na huendi hospitali unaombewa tuu je utapona bila kula dawa? ALIISHIA KUPATA KILEMA CHA KUDUMU KWA UZEMBE WAKE. Namimi niliangukia kichapo kila akiikumbuka SWALI LANGU Hadi Nika hamishwa shule!
HAKUNA ALIYE WAHI PONA TATIZO LINALO ONEKANA KWA MAOMBI!
Kupona inawezekana kama tatizo litakuwa limeshikiliwa na mtu Ki uchawi.
Kuna kijana alikuwa mtaani kwetu yeye alizariwa akiwa mremavu. Kuna muda walikuja watu wa mikutano ya injili, nae akapelekwa Na wazazi wake. Wazazi hawakuwa ni watu wa kusali kabisa. Walikuwa ni watu wa kuuza pombe za kienyeji.
Basi alifanyiwa maombi siku ya kwanza.
Siku ya pili
Mpka ya nne. Mabadiliko yakaanza kuonekana. Aliacha kutumia magongo na kiasi akaanza kutembea kwa miguu yake jambo kwa shida.
Basi wale waliomwombea wakatoa sharti moja tu.
Ambalo lilikuwa gumu kidog kutekelezwa.
Wao walikuwa na mkutano wa siku 7 tu.
Wazazi waliambiwa waanze kumpeleka kwenye moja ya kanisa la mitaa ya Jirani. Ambako wanamahusiano furan na hawa waliokuja na mkutano.
Sharti hilo lilikuwa gumu sana Kwa wazazi wa huyu kijana kwani ilikuwa Lazima waokoke kisha wabadili maisha yao. Kitu ambacho kilikuwa kigumu sana kwao.
Basi siku zilivyosonga mtoto akaanza kurudi kwenye ile hali yake.
Kuombewa na kupona kupo. Ila si kwa kiasi hicho ambacho tunaonyeshwa.
Mimi ni mmoja ambaepia niliwahi kuombewa na ikawa miujiza kwangu.