Tangantika
JF-Expert Member
- Aug 12, 2018
- 5,586
- 7,087
Uko tayari kuziacha nyapi za kina shilole,lulu nk?Kaka yangu alipona, alianza kuumwa macho akiwa form one. Alikua anatumia miwani alivyofika form four macho yakagoma kabsa kuona hata kwa miwani. Jumapili moja alikuja kuchukuliwa na mchungaji wa kanisa fulan la kilokole. Siku hiyo alirudi anaona vizuri. Nilichojifunza
1. Maombi yanaponya maradhi Ila hasa maradhi ya kurogwa.Maradhi yanayoingia mwilini kiroho Kama kurogwa hayawez kutibiwa hospital, maombi ndio suluhisho
2.Imani kwamba Mungu atakuponya ni muhimu sana, Kaka yangu yule alikua haamin kbs ktk maombi. Sisi ni wakatoliki hivyo bro alikua haamin kbs makanisa mengine. Alikua akisisitiza maneno ya kanuni ya Iman" nasadiki kwa kanisa moja takatifu katoliki la mitume" hivyo tulikua tukimlazimisha kwenda kuombewa bila yeye kupenda na hakupona. Siku aliyopona aliamua mwenyewe kwenda kuombewa na aliondoka home anasema anakwenda kuona.
3. Kama umeponywa maradhi ya kichawi inabidi uwe karibu Sana na Mungu Kwan wachawi wataendelea kukusumbua. Ndugu yangu huyu aliendelea kusumbuliwa na wachawi. Alikuja kupata homa Kali akakimbizwa akalazwa hospital Ila ajabu asubuhi yake hakuwepo hospital akaja kuokotwa porini akiwa hoi na akafariki akiwa anarudishwa hospital. Yapo matukio mengi kwake yalomkuta mpaka tukahis anarogwa, sijayaandika hapa.
4. Kuna nguvu kubwa Sana ktk maombi. Nikiwa darasa la 3 nilipoteza viatu shule, tulikua tunavua na kuweka uwanjan Kama magoli ya mpira baada ya mchezo sikuvikuta viatu vyangu. Mama akagoma kuninunulia viatu. Usiku ule nilisali Sana rozali nikamuomba Mungu anisaidie. Asubuhi nilitoka home pekua njiani niliokota elfu kumi. Nikanunua sendoz nikaenda nazo shule na Jumapili mnadani nikanunua viatu. Mara nyingi nilikua nikipata shida naomba na Mungu anajibu. Ila nilipoanza tabia ya kugongana na Mungu akaacha kunisikiliza mpaka leo. Mambo yakitulia ntarudi kanisani kwa nguvu zote.
Upo tayari kuwapinga staff member wezi wa mali ya uma?
Upo tayari kuwapinga wafanyabiashara wezi?
Upo tayari kuwapinga wezi wa kura?