Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Nimemsikiliza leo Raila akidai ya kuwa yeye hatetei ajira yake serikalini bali anatetea demokrasia: Swali linakuja kama ni kweli kwanini anayakubali matokeo ya sehemu nyinginezo zote ambazo CORD imeibuka kidedea na kuyapinga maeneo ambayo wamegalagazwa na kupigwa mweleka?
Kama kweli IEBC walicheza faulo basi Amollo na wafuasi wake wanapaswa kuyakataa matokeo yote badala ya kuchagua yale ambayo wamepigwa chali na kuanzia hapo ndipo tutakapoanza kuwaamini ya kuwa wao ni watetezi wa demokrasia ya kweli.,
Mkakati wa Raila unanikumbusha mwaka 2000 pale mgombea uraisi wa Democratic party of USA Al-Gore alipopinga baadhi ya matokeo ya maeneo machache ya Florida badala ya kuomba kura zote zirudiwe kuhesabiwa.
Kwa maoni yangu Amollo awe mkweli na kutangaza masilahi ni binafsi siyo endelevu kama anavyodai.
Pili Amollo amekuwa akidai kuna tawala mbili moja ni ya "status quo" na nyingine ni yake ambayo inalenga kuleta mabadiliko. Kwa kiongozi aliyekuwemo serikalini muda mrefu inabidi ajiulize hivi maana halisi ya "status quo" ni ipi wakati yeye mwenyewe anakiri yuko serikalini ambako amekuwa akitafuna nusu bofloooooooooooooooooooooo.
Wakati wa kampeni Amollo alidai yeye ndiye kiongozi mwenye uzoefu kulikoni wengineo wote kama hili ni kweli yawaje anawaita wenzie ni "statu quo" wakati yeye yupo serikalini tena kuanzi a enzi za Moi ambapo alikuwa waziri wa energy? Kama huu siyo kukosa busara sijui nini? Lakini Miguna wa Miguna kwenye kitabu chake alitujuza ya kuwa Raila ni failure wa darasa la NNE kwahiyo uwezo wake wa kutafakari unatia mashaka makubwa kabisa!
Ujumbe wa Amollo umejaa unafiki na vigumu kwa mtu mwenye akili timamu kumwamini lazima uwe juha kidogo au ziwe zimefyatuka kuafiki hizi khoja za Amollo ambazo zimejaa migongano mingi ya kimantiki na khali asilia............