HUU ni mwisho wa Raila kama mahakama itamsikiliza na kutengua matokeo maana yke watu wengi waaliompigia kura hawatompigia tena uchaguzi ukirudiwa itaonekana ana uchu wa madaraka, big ego (hawezi kutulia hadi historia ya kenya imuandike na yeye alikua Rais wa Kenya), mpenda shari, na mbinafsi (mtu ambaye anaweza kusaidia watu akiwa siyo kiongozi wa rasmi wa kisiasa-Raila ana nguvu ya kushawishi umma bila ya kua kwenye cheo cha kuchaguliwa na hii ndicho watu wangependa kumuona anafanya kurekebisha serikali, kushawishi wapiga kura kwenye masuala muhimu ya kitaifa....
uchaguzi ukirudiwa Uhuru watu wake wa Kikuyu na watu w Rift valley watarudi kwa wingi ule ule na kupiga kura vile vile wakati wakamba, taita na watu wengine wa pwani wataona uvivu kupiga kura tena ndani ya muda mfupi na luhya watafanya hivyo hivyo kwa sababu kama mchambuaji mmoja ameonyesha kwenye The East African kua kenya kuna makabila ma3 tu yaliyo centrally-politicized and organized to vote as a block na hao ni Kikuyu, Kalenjin na Luo hawa hata uchaguzi urudiwe mara 10 watajitokeza vile vile na kupiga kura vile vile, makabila mengine yote hayana cha kupata sana wala kupoteza sana na hivyo kutoona umuhimu wa kujisumbua tena kwa mara nyingine na kupiga kura tena. kati ya haya uhuru ana kura mil 4+ za kikuyu+kalenjin block, wakati Raila atakua na kura za uhakika za wajaluo pekee yao huku wakamba na waluhya wakiwa hawajulikani watajitokeza kwa kiwango gani kupigabtena kura achilia mbali makabila madogo dogo.
ukitoa hilo Uhuru atatumia hela yake kwa kampeni na safari hii ataonekana ni potential winner na hivyo kuattract funding toka kwa business elites na Moi, mount kenyan mafia na wengineo walioonyesha kutomsupport kwenye uchaguzi ulioisha. Hii itampa shida Raila ambaye ataonekana not a safe bet for the presidency na hivyo kutokua na funders wengi.
kujiweka sawa IEBC hata kama ilikosea haitompa ushindi Raila kwa sababu itataka uprove kua ilifanya kazi sawa sawa na kumtangaza Uhuru japokua kulikua na makosa madogo dogo yasiyoweza kuhatarisha matokeo haya yaliyotangazwa. IEBC wakimtangaza Raila baada ya uchaguzi wa marudio itazua mjadala mwingine ikiwezekana na petitio nyingine na hivyo kuonekana hawawezi kazi na kutishia kuondolewa na bunge.
Kuachiliwa kwa Francis Muthaura mshitakiwa mwenza wa uhuru kunaweza kuwashawishi wengi hata wale waliokua waoga kumpigia kura mara ya kwanza kumpigia kwenye marudio kwa sababu sasa inaonekana kuna dalili za kesi yake huko ICC kushindwa kusimama...na mengi mengineyo
yote kwa yote Raila angefuata ushauri wa kukaa kama kiongozi nje ya serikali kiongozi mkubwa wa kijamii mwenye nguvu na sauti hii ingemjenga sana hata maadui wake wangemuona siyo millitant na radical tena na ingemwezesha kujipanga tena kwa round ya mwisho 2017....aombee mahakama isitengue matokeo na kuruhusu uchaguzi urudiwe hii itakua ni mwisho wa Raila kisiasa....