Hivi kweli Raila na CORD ni watetezi wa demokrasia au wanatetea matumbo yao?


na huu nao ni mchango?
 
Pamoja na kelele zote uchaguzi ukirudiwa bado watashindwa tu. Sioni kama kuna uwezekano wowote wa hawa jamaa kushinda labda wapate msaada wa moja kwa moja kutoka ICC.

uchaguzi kamwe haurudiwi. Hivi ukienda kwenye ATM kutoa hela na ikakugomea unaenda mahakamani au unaenda kwa teller akuhudumie........................???????????????

Raila anasema unaenda mahakamani! Kweli mahakama gani itakubaliana na huu upuuzi?
 
behind every push on democratic change in Kenya.....raila was involved tangu enzi za Moi. it is better kusoma historia ya mtu kisiasa kwanza kabla ya kuanza kumpaka matope.
 

Supreme Court of Kenya haina mamlaka ya kutoa tamko ambalo Raila anadai maana kwa kufanya hivyo itakuwa inaingilia uhuru na mamlaka ya Mahakama Kuu kuhusiana na chaguzi nyinginezo zote zilizosalia ukiondoa hii ya Uraisi.

Kwa hiyomadai ya Raila kwanza hayatelezeki. Pili hana ushahidi na tatu, vigezo vilivyowekwa na nchi nyinginezo duniani ikiwemo Uganda, Marekani, Ujerumani N.k Uchaguzi wa Uraisi hauwezi kutenguliwa kwa hisia za ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au ukiukwaji wa taratibu ambao hauathiri matokeo ya sauti ya wapigakura.....................so far Raila hajaweza kuja na ushahidi wa kuonyesha hivi vigezo vimetimilika
 
Rutashubanyuma
Kwenye hii kesi uliandika kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG)ni lazima ahusishwe kama mmoja wa walalamikiwa, lakini hapa hayumo vipi na kulikoni? tujuze mkuu.

Kikawaida ni kuwa bila A.G wadaiwa hawana kesi ya kujibu na haki zao zimekiukwa za kujitetea kwa sababu muhimili wa kwanza wa kuitetea serikali ni A.G.

Tatizo ni kuwa majaji wengi wanawasubiria walalamikiwa kuidai hiyo haki wasipoidai mara nyingi hawaifanyii kazi.

Maoni yangu ni kuwa kosa la kutomshtaki A.G linatosha kuifuta hii kesi kwa kutowapa nafasi wadaiwa haki ya kujitetea. Lakini inafaa wao waidai hii haki wakiitegemea mahakama tu wanaweza kutopewa na kesi ikaendeshwa kama vile A.G siyo mahitaji ya kisheria!
 
behind every push on democratic change in Kenya.....raila was involved tangu enzi za Moi. it is better kusoma historia ya mtu kisiasa kwanza kabla ya kuanza kumpaka matope.

kushindwa uchaguzi ni kupakwa matope au ni kuelezwa ukweli? Pili, kutofahamu sheria na mipaka ya kimahakama inahusiana vipi na harakati za kutafuta demokrasia? Hiyo kazi si inafanywa na kila raia au unataka tukuamini kuwa Raila akifa leo kenya is dead? Be4 Raila was born kenya was there and after Raila goes to eternal sleep Kenya will continue to thrive............
 
Hivi kuna utetezi wa demokrasia, au utetezi mwingine wowote ule, ambao auhusishi mtu kutetea maslahi yake pia?
 
HUU ni mwisho wa Raila kama mahakama itamsikiliza na kutengua matokeo maana yke watu wengi waaliompigia kura hawatompigia tena uchaguzi ukirudiwa itaonekana ana uchu wa madaraka, big ego (hawezi kutulia hadi historia ya kenya imuandike na yeye alikua Rais wa Kenya), mpenda shari, na mbinafsi (mtu ambaye anaweza kusaidia watu akiwa siyo kiongozi wa rasmi wa kisiasa-Raila ana nguvu ya kushawishi umma bila ya kua kwenye cheo cha kuchaguliwa na hii ndicho watu wangependa kumuona anafanya kurekebisha serikali, kushawishi wapiga kura kwenye masuala muhimu ya kitaifa....

uchaguzi ukirudiwa Uhuru watu wake wa Kikuyu na watu w Rift valley watarudi kwa wingi ule ule na kupiga kura vile vile wakati wakamba, taita na watu wengine wa pwani wataona uvivu kupiga kura tena ndani ya muda mfupi na luhya watafanya hivyo hivyo kwa sababu kama mchambuaji mmoja ameonyesha kwenye The East African kua kenya kuna makabila ma3 tu yaliyo centrally-politicized and organized to vote as a block na hao ni Kikuyu, Kalenjin na Luo hawa hata uchaguzi urudiwe mara 10 watajitokeza vile vile na kupiga kura vile vile, makabila mengine yote hayana cha kupata sana wala kupoteza sana na hivyo kutoona umuhimu wa kujisumbua tena kwa mara nyingine na kupiga kura tena. kati ya haya uhuru ana kura mil 4+ za kikuyu+kalenjin block, wakati Raila atakua na kura za uhakika za wajaluo pekee yao huku wakamba na waluhya wakiwa hawajulikani watajitokeza kwa kiwango gani kupigabtena kura achilia mbali makabila madogo dogo.

ukitoa hilo Uhuru atatumia hela yake kwa kampeni na safari hii ataonekana ni potential winner na hivyo kuattract funding toka kwa business elites na Moi, mount kenyan mafia na wengineo walioonyesha kutomsupport kwenye uchaguzi ulioisha. Hii itampa shida Raila ambaye ataonekana not a safe bet for the presidency na hivyo kutokua na funders wengi.

kujiweka sawa IEBC hata kama ilikosea haitompa ushindi Raila kwa sababu itataka uprove kua ilifanya kazi sawa sawa na kumtangaza Uhuru japokua kulikua na makosa madogo dogo yasiyoweza kuhatarisha matokeo haya yaliyotangazwa. IEBC wakimtangaza Raila baada ya uchaguzi wa marudio itazua mjadala mwingine ikiwezekana na petitio nyingine na hivyo kuonekana hawawezi kazi na kutishia kuondolewa na bunge.

Kuachiliwa kwa Francis Muthaura mshitakiwa mwenza wa uhuru kunaweza kuwashawishi wengi hata wale waliokua waoga kumpigia kura mara ya kwanza kumpigia kwenye marudio kwa sababu sasa inaonekana kuna dalili za kesi yake huko ICC kushindwa kusimama...na mengi mengineyo

yote kwa yote Raila angefuata ushauri wa kukaa kama kiongozi nje ya serikali kiongozi mkubwa wa kijamii mwenye nguvu na sauti hii ingemjenga sana hata maadui wake wangemuona siyo millitant na radical tena na ingemwezesha kujipanga tena kwa round ya mwisho 2017....aombee mahakama isitengue matokeo na kuruhusu uchaguzi urudiwe hii itakua ni mwisho wa Raila kisiasa....
 

na uchaguz ukirudiwa mudavad ataenda kwa uhuru!
 
na uchaguz ukirudiwa mudavad ataenda kwa uhuru!

Mkuu nina wasiwasi yasije yakatokea ya kusawazisha goli dakika ya 93 halafu katika dakika 30 za nyongeza ukapigwa goli nne, washabiki wakaishia kujutia kitendo cha kusawazisha lile goli moja. Kama kutatokea uchaguzi mwingine kuna hatari ya mtu kushinda kwa zaidi ya 60%
 
Demokrasia katika Nchi zetu changa huwa inahesabiwa kua ipo pale chama kimojawapo kinaposhinda, aliyeshinda ndio anaeona kuwa Democrasia ipo ila aliyeshindwa huwa aamini kua ameshindwa hata kama alipata kura mbili. Hivyo Raila Odinga hatawahi kuona uchaguzi wa kidemocrasia mpaka pale yeye atapokua Raisi wa Kenya
 

Unadhani ni kwa nini inakuwa hivyo?

Huoni kwamba wizi wa kura wa wazi wazi wa watu kama akina Kibaki na Mugabe ndiyo hujenga hizo hali za mashaka?
 
ANKOJEI kuwa na kumbu kumbu zako vizuri RAILA Alisha ilalamikia IEBC tangu walipopanga tarehe ya Uchaguzi mwezi March 2013 badala ya Disemba 2012, hata wakati wa Kampeni kuna masuala alisha lalamika kuhusu tume, pia coverage ya Media ilikuwa inawabeba Jubilee zaidi kuliko CORD au AMANI...!! Ushindi wa JUBILEE ulisukwa kisayansi sana..it needs people who can read between the lines to see the anomalies involved otherwise siyo rahisi kugundua faulo iliyochezwa!!!
 

nakubaliana na wewe but stil he should ask himself kwa nin kaibiwa kama ameibiwa kweli, kwa nin yeye hakuiba Wakati yeye ndio bos wa uhuru? angeenda mahakaman mapema kabla ya uchaguzi, i had once supported this man lakin kwa sasa naona jamaa hawez siasa n kama asenal wanacheza mpira vizur kikombe hakun, so!
 
Unadhani ni kwa nini inakuwa hivyo?

Huoni kwamba wizi wa kura wa wazi wazi wa watu kama akina Kibaki na Mugabe ndiyo hujenga hizo hali za mashaka?

pamoja na kwamba kibaki aliiba kura hadharan kama unavodai, marekan na uingereza walimpongeza mara moja na kumpa ushirikiano wa kidamu had somalia, wakamsahau laila na kumwacha kama kuku mwenye kideri, wakamdanganya na cheo kipya cha prime minister.ujinga wa mwafrika n ndoto kututoka. this time wanamtaka raila kwa udi na uvumba kwa lipi jema alilowatendea?
Mugabe ni level ingine kaka,
 

Kwa hiyo kwa akili yako ukipongezwa na Marekani na Uingereza ndo unakuwa halali?

Na Uhuru wanamtaka kwa lipi jema haswa?
 
ANKOJEI, Raila hakuwa na nguvu kiasi hicho kusema alikuwa boss. Huwezi kufurukuta katika serikali ambayo Mkuu wa majeshi ni Mkikuyu,Usalama wa taifa Mkikuyu,Mkuu utumishi wa umma MKikuyu, executive ministers( finance,internal security,foreign affairs) wote na ps wao ni wakikuyu,Provincial commissioners 90% ni kikuyu..!!! Raila kwenye serikali ya mseto alikuwa Boya tuuuuu. rigging ilifanyika kwa ufundi wa hali ya juu ... Pia kumbuka Uhuru ndiye tajiri anayeongoza Kenya (according to Forbes 2012). Hivyo anatumia msuli wa pesa pia kulaghai. Unadhani hata hawa mashahidi wanao-withdraw ushahidi kule ICC ni nini? The guy is mafioso...
 
Last edited by a moderator:

Ruta bana umenikasirisha kabisa kwa hili hivi wajua kweli kinachoendelea huku? Wajua vizuri alichofanya Uhuru kupata ushindi?? Huyo Isaac wa IEBC alikuwa anakimbia nini na kurudishwa JKIA mara mbili hujiulizi??
 
Ruta bana umenikasirisha kabisa kwa hili hivi wajua kweli kinachoendelea huku? Wajua vizuri alichofanya Uhuru kupata ushindi?? Huyo Isaac wa IEBC alikuwa anakimbia nini na kurudishwa JKIA mara mbili hujiulizi??

Ninakushukuru kwa majibu ya kiungwana. Wengi humu jamvini ukinena kinyume cha wanavyotaka uoni basi jua utaishia kutukanwa au hata nyuzi zako kufungwa eti zimepitwa na wakati kumbe bado. Pole kwa kukukasirisha. Nimefurahishwa na IEBC majibu yao ndani ya Supreme Court hususani pale waliposema Raila has NEVER conceded defeat in presidential elections from 1997, 2007 and now. The impression there is as far Raila is concerned is my way or the HIGHWAY.................now the Supreme court has the opportunity to deal with all issues including those you did not mention.

La pili, public interest versus narrow private interest masquerading as public interest.

The game has only begun. Mengineyo uliyoyaongea kwa vile hujayafafanua sina la kujaziliza! Tatizo ya hayo unayoyaoongea ni kuwa mbona kwenye malalamiko ya Raila mahakamani hajayalalamikia?
 

Kama haya unayoyaandika ni kweli then Raila is a roasted beef....................he will never prevail because God has anointed the son of Jomo to be the fourth president of kenya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…