The Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 11,099
- 13,709
Kenya inasifika kwa kupinga unyanyasaji. Walianza Mau Mau waliokinukisha hadi Kenya ikawa huru.Baada ya hapo, waltokea Young Turks waliompa taabu imla Daniel arap Moi hadi walipomfurusha mwaka 2002.
Baada ya hapo,, juzi juzi walitokea Gen Z wakakinukisha hadi kulazimisha majambazi yao ya kisiasa kufunga ndoa ya mkeka (shotgun marriage).
Ukiondoa akina mzee Nyerere na wenzake, Tanzania haijawahi kuwa mapambano ya haki. Je tuna tatizo gani hadi tunaitwa machawa na kukubali? Je Gen Z wetu kwanini hwajifunzi kwa kwenzao wa Kenya?