Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,662
- 6,888
Nimesikia wasomi wawili wa ngazi ya PhD wakitofautiana katika kutaja desimali (decimal notation). Mmoja ana PhD ya kusomea na mwingine ya heshima. Alianza yule mwenye PhD ya kusomea na kusema kwa majigambo na kujiamini kuwa mteuliwa amepata asilimia themanini na tisa nukta arobaini na mbili (89.42), mfano, na yule mwenye PhD ya heshima alitamka asilimia themanini na tisa na point nne mbili (89.42), mfano. Je, kati ya hawa wasomi wawili nani yuko sahihi?!
View: https://youtu.be/Wqta-LFAN18?si=xdvWoNLvFLxF6V8e
View: https://youtu.be/Wqta-LFAN18?si=xdvWoNLvFLxF6V8e