Juzi, waziri mkubwa, Lameki Madilu wa nchi ya Ahaha aliacha dunia hoi. Katika kujipendekeza, kumpendezesha na kumpamba aliyempa cheo si akaropoka eti kutegemea misaada kumepitwa na wakati na dunia imebadilika.
Hapa, kuna mambo ya kufikirisha na kudurusu.
Mosi, je, amelijua hili leo au ni baada ya kupigwa pini tokana na mauaji ya Oktoba 29?
Je, haya yanatoka moyoni au ni rongorongo mdomoni kumpendeza mama chawa?
Je, kama asemayo ni kweli, mbona haelezi mikakati ya kujitegemea?
Je, Tanzania ina utamaduni wa kujitegemea au utegemezi?
Je, kati ya hawa vitegemezi waibao kodi zetu na kuzifuja na wanaowapa misaada nani kapitwa na wakati?
Je, kwa utawala wa hovyo wa sasa, ataweza kusimamia maneno yake au kuramba matapishi yake kama aliyebweka 'who are you' utadhani hawajui hao aliobwekea?
Je, watanzania ni mataahira hadi kuamini upupu utokanao na uchawa na ukosefu wa busara?
Je, kati ya watawala na wananchi nani anaishi kwa kutegemea misaada?
Kweli yajayo yanafurahisha.
Eti na Lameki ni daktari! Mmmejua kututenda jamani.