saigilomagema
JF-Expert Member
- Jun 5, 2015
- 4,683
- 7,222
Kuna tabia ya ajabu hapa stand kuu Arusha, mabasi makubwa hasa yanayotoka Moshi hayapakii abiria hata km kuna nafasi. Ila matajiri wanamdharau huyu rais wa sasa, haya mambo sikuyaona kabla, wakati nauli ni TZS 6,000 mabasi yalikuwa yanapakia abiria. Sahivi nauli ya serikali ni TZS 8,000, pamoja na kwamba wanachaji TZS 10,000 lakini hawakupakii. LATRA ipo wananchi wananyanyaswa na wenye mabasi na mawakala wao, kuna LATRA kazi yao nini? Kwanza kwanini wajipangie nauli? Halafu hawajali wanakuambia wapigie hao LATRA hawawaogopi maana mabasi ni ya kwao siyo ya LATRA. Tuambieni haki ya abiria ni ipi kisheria? Utafikiri nchi haina utawala. Huyu mkurugenzi mkuu wa LATRA apelekwe kwengine hajui ht majukumu yake. Pili waziri wa Uchukuzi abadilishwe, huyo mpemba km mama anampenda sana ambadilishie wizara. Hii sekta wapewe watu km Herrison Mwakyembe, Mwakyembe alikuwa anafuatilia kero za wananchi, ndio maana DSM kuna treni ya Mwakyembe, ule ulikuwa ubunifu wake. Makame Mbarawa Mnyaa ni mswahili asiyejitambua, au kwa vile huku ni bara? Ndio maana Magufuli aliwachukia matajiri, matajiri hawana utu, ni wanyama, Rais simama kuwatetea wananchi wako maana ht siku ya kupiga kura hakuna tajiri atapanga foleni kukupigia kura. All in all hao wamiliki wa mabasi wafuate sheria za nchi.