Hivi lengo la kuja duniani ni nini?

Hivi lengo la kuja duniani ni nini?

Ukifikiria sana, ata hizi mbwembwe tunazozifanya ni ubatili tu. Maisha yako ya kuishi duniani ni ndani ya miaka 80; baada ya hapo, lazima upotee na usaaulike, waje viumbe wengine waendelee kujimwambafai.​
 
Ni ngumu kujua, kusudi la kuja Duniani, kiasi hata aliyetuleta hataki tumuone tukiwa hai hapa Duniani!
 
Mungu ametuumba ili TUMJUE,TUMPENDE,TUMTUMIKIE na mwisho tufike MBINGUNI.
 
Siku utapoamia kujiuliza hayo maswali wewe mwenyewe, ndo siku utapata majibu
 
Kuna swali huwa linanizunguka kichwani hasa linaniambia lengo la kuja duniani nini?

Kwanini wengine duniani watajirike na wengine wawe masikini? Na kwanini wengine wamake Impact ila wengine wasimake impact?

Kwanini wagunduzi wengi wa Teknologia wengi ni ngozi nyeupe? Kwamba waAfrika wengi wetu tumekuja kusindikiza wengine?

Lengo la kuumbwa ni nini? Akiachana na kuja kuabudu je lengo hasa nini? 💫💫💫
Naona kama tuliletwa kuwatumikia wanasiasa tu
 
Back
Top Bottom