Hivi leo waTanzania tukiamua kutumia bidhaa zinazozalishwa ndani tu kwa miaka mitano, hatutakuwa nchi ya dunia ya kwanza?

Hivi shit hole countries zilizopo Afrikan zilotajwa majina!!

Nadhani haziwezi kuzalisha vitu vyenye ubora.

Uzalendo ni pamoja na kuachana na tabia ya kununua mabomu na bunduki za kuua wananchi kwa hofu ya kukosa kura halali.

Hayo mengine ni utapeli wa wanasiasa Dunia ni kijiji kama mwenzako anazalisha shati na kuuza sh. 500.
Hakuna haja ya kutengeneza kiwanda kutengeneza nguo cha kuharibu mazingira bure.
Tununue huko wanakouza rahisi.
Sisi tuzalishe Mali ghafi na chakula tuuze dunia nzima.
Tuchimbe madini yaliyojaa ardhini ambayo yana bei hata hapo Kenya kuliko hapa kwetu nchi iliyokaaniwa na Shetani mkuu Mwenge.

Tutaendelea siku tukiwaza kama Taifa sio chama kinachotugawa mpaka kwenye mambo ya kuiga kama mpira.

Namkubali sana Trump.
 
Hakuna mawazo finyu kama haya. Leo mnalalamika tshs kushuka thamani, ajira hamna, tutauza madini na kuingiza toothstick n.k.
The only secreat here is yo improve domestic production.. Hii ya dunia kijiji wewe ndo unasema wenzio hawaoni hizo mataifa makubwa duniani USA, Russia and China wanahaha kulinda viwanda vyao mtu mweusi umebaki kijiji kama dunia. Sehemi pekee tunayofeli ni economic inteligence yanayochagizwa na mawazo mgando kama yako
 
 
Hata shaver za kunyolea maeneo binafsi tunaagiza labda utafute papuchi pale kimboka ndio utapata za bure ambazo ni made in Tanzania
 
Hoja ya ufala hasa ni ipi? Maana vitu vingine ni kasumba tu, mtu akisikia bidhaa hii ni ya Tz automatically anaiona haifai, ila akiambiwa ni ya ujerumani anaichangamkia, tujitafuna wenyewe.
Kuna vitu really ni ufala aisee. Unakuta Chinese product iliyolipiwa sea transport, taxes, etc ni cheaper than locally manufactured. Watanzania tuko price oriented, hapo no way tutaenda for Chinese product tu. Uzalendo sio kununua kitu cha bei kubwa kisa tu Made in Tanzania.
 
Na ndio China walichofanikiwa, mwaka 1960 tulikuwa nao sawa kiuchumi
Kingine China kuna vitu viwili vikuu viliwabeba. Na vyote vinachangiwa na population yao kubwa. Since wako wengi means ni ngumu serikali kumuajiri kila mmoja au wengi wao. So in order for them to survive they had to think more more hence wengi wakaanzisha small private industries. It was a matter of being creativity to think what can be demanded more.

Cha pili sasa kwa uwingi wao huo, means market ikawa available. So whatever produced there by then got market instantly.
 
Sasa na wewe copy na upaste content / heading za huu uzi ambapo nimeitaja Kenya au ambapo nimesema bidhaa toka nje zisiruhusiwe kuingia nchini, hahaha
 
Shida yako unaishi usiyo ielewa...!
 
Mie kwanza uchumi wangu binafsi then ndio nitafikiria iyo nchi | naminyika kitusua then niwaze nchi.
 
Fenicha za china hawatumii miti pori au miti ya kapandwa, wanatumia vumbi la miti, hivyo kabati la china ni rangi tu na si ugumu au ubora, hivyo bei ni nafuu.
 
Hivi kitambaa cha nguo cha Tanzania na nje kipi chenye ubora?
 
Yale yale kila mfanyakazi wa serikali awe na line ya Ttcl, Aisee biashara na siasa huwa vinajitenga kama mafuta na maji watu wanaangalia unafuu tu na ubora
 
Ni mawazo yangu na sio lazima nitegemee ngonjera za wanasiasa wanaotumiwa na Mabeberu wa nje kuja na agenda za viwanda kwa lengo la mabeberu kuleta viwanda vilivyochoka na visivyohitajika tena huko kutokana na kuwa ni viwanda vinavyoharibu mazingira kwa moshi na Kemikali kubwa.

Unaleta ubishi wa ajabu tu na maneno yasiyo na staha lakini hata Mwalimu Nyerere mnayemuenzi kinafiki alishauri hivyo kuwa dunia ni kama kijiji. Ndio maana China ananunua nyama ya Punda Tanzania. Ni fursa tulipaswa tuwatumie wataalam wetu wa mifugo kuzalisha kwa wingi badala ya kuwaachia wachina.
Haihitaji kiwanda wala uharibifu wa mazingira .
Wachina wanakula nyoka na paka na mbwa lakini ukipita barabarani kutokea Dsm mpaka Arusha kwa siku moja unaweza ukakuta Mbwa mia mbili wakegongwa na magari na kubaki mizoga tu .
Tafakari cha kufanya hapo ilikua nini!
Wasomi wanasubiri ajira ya Kiwanda kinachomilikiwa na Mchina RAIA wa China

Nilichosema ni kuwa Kama mchina anazalisha kwa bei rahisi kuna haja gani na sisi kuzalisha bidhaa hiyo hiyo wakati inapatikana muda wote na kwa wepesi kuliko ile inayozalishwa nchini?
Kwa nini tusifanye utafiti tukajua mahitaji yao tukazalisha na kuwauzia kwa wingi ili wao wabaki na mauchafu yao ya viwanda na sisi tubaki na ardhi yetu nzuri isiyo na uchafu mkubwa wa mazingira?

Umezungumzia tooth pick bila kujua kuwa mtanzania amekopi na kupest hizo tooth pick na sio ubunifu wake.
Miaka 30 ilitopita hapakua na hivyo vijiti lakini. Wenzetu wakavibuni na kutuuzia.
Hujui kuwa kuvitengeneza vinahitaji miti huko kwao. Tuwaache wamalize misitu yao na sisi tuwauzie samaki wa Sangara na Sato, nyama ya mbwa,nyoka, punda, na hata nyama za nyumbu ,nyati n.k.

Tuwauzie maparachichi na matunda.
Tuwauzie madini kwa bei kubwa huku wao wakituuzia Vijiti na nguo kwa bei rahisi.


Tukizalisha tu Chakula cha kutosha tutaingiza pato kubwa sana la nchi kuliko kuuza toothpick nje ambayo inatokana na ukataji wa miti.

Korosho tu na pamba inaingiza pato kubwa sana la fedha za kigeni kuliko kiwanda chochote cha kichina.

China ni Nchi yenye pato kubwa kwa sababu ya wingi wao mana inaweza kukusanya kodi kubwa sana kutoka kwa watu zaidi ya Bil. Moja. Lakini China ni nchi yenye watu wengi maskini sana sana. Huwezi kulinganisha na nchi kama Qatar au Kuwait ambayo haina viwanda vingi zaidi ya utajiri wa asili.

Sisi tungekua na Viongozi wanaoweka mbele utaifa kuliko vyama na siasa zao tungekuwa na maisha ya juu sana kuliko wachina ambao wengi wana maisha magumu sana na ni matajiri wachache tu wenye maisha ya juu ukilinganisha na wingi wa watu kwenye taifa hilo.

Mpaka leo tunawaza kuleta wawekezaji toka China kwa ajili ya kuvua samaki.
Kusindika Nyama.
Kuzalisha maparachichi n.k.
Kufuga Punda wa nyama, kufuga mbwa wa nyama n.k wakati tulipaswa kuwapa utaalama huo watu wetu ili wawauzie wachina

Kwa nini mpaka sasa hatuwapeleki vijana wetu kusoma huko kwa mkataba wa kuja kufanya kazi ya uvuvi na kusindika samaki?
Wasomi wapo wengi lakini wengi wanawaza kuajiriwa kwenye viwanda vya wachina kwa mishahara midogo inayosaidiwa na wizi ili wakidhi mahitaji yao.

Wizi wa Mali za umma unaofanywa na wawekezaji unatokana na kushirikiana na wasomi na wafanyakazi wachache wenye mishahara duni na kuacha nchi ikiwa kama Dampo la viwanda vyenye kuharibu mazingira tu.

Badala ya kulima Pamba na kugundua viwanda vidogo vidogo vya kutengeneza nguo huko majumbani na kuuza kwa bei nafuu huko mitaani ili watu watoke Sudani waje kununua nguo Tanzania tunamsubiri mchina ili atuajiri kwenye kiwanda kikubwa kinachoitwa cha mwekezaji.
Zamani kule magerezani walifundishwa kutumia nyuzi kutengeneza vitambaa vigumu sana kwa kutumia mashine rahisi sana zilizotengenezwa na mbao tu. Leo mitaani nani anaweza kutengeneza nguo kwa mashine ndogo ya mbao tu na isiyohitaji hata umeme wala grisi wala dizeli ni mikono na miguu tuu na kitambaa kinatoka kigumu kama kombati ya mgambo.

Kwa nini watu wasiruhusiwe kuvua kwa wingi sana ili wakikosa soko wawaze na kubuni namna ya kusindika samaki ili wauze nje kidogokidogo.

Kwa nini wasomi wenye Diploma ,digrii n.k wasijifunze namna ya kusindika maparachichi na kutengeneza bidhaa ndogo ndogo kwa maparachichi lakinu wanawaachia kazi hizo wachina ili waombe ajira ya mwisho wa mwezi?

Viwanda endelevu ni lazima viwe vimebuniwa ndani kutokana na ushindani wa ndani sio wa nje.

Bidhaa za mchina kwa miaka mingi zilikua hazina soko Ulaya mpaka walipoziboresha baada ya kuruhusu wawekezaji wakubwa binafsi. Ushindani wa nje ukaanzia hapo.

Tuna ardhi kubwa yenye rutuba ,maji mengi ,utalii mwingi, madini mengi lakini hatuna mfumo mzuri wa elimu ya kuvitumia hivyo kama fursa zaidi ya kuwadanganya watu kuwa viwanda ndivyo mkombozi wetu wakati viwanda navyo pia vinahitaji Mali ghafi toka ardhini .

Tunafungua viwanda ambavyo Mali ghafi yake tunaagiza toka nje.
Kiwanda tumeagiza ,wataalam tunaagiza na malighafi pia.
Ukombozi wa ajira uko wapi hapo?

Kenya na hata Tanzania tumejenga Reli ya SGR, lakini 75 % wataalam wanatoka nje na wameshika idara zote muhimu.
Mataruma tunaagiza badala ya kuzalisha kutokana na Madini ya Chuma tuliyo nayo.
Treni nayo tutanunua toka nje.
Kwa miaka ya mwanzo tutahitaji wataalama wa kusimamia uendeshaji toka nje halafu tuanaona ni sawa.
 
Fenicha za china hawatumii miti pori au miti ya kapandwa, wanatumia vumbi la miti, hivyo kabati la china ni rangi tu na si ugumu au ubora, hivyo bei ni nafuu.
Hiyo nimetolea mfano tu , zipo bidhaa nyingi tu ghari kuliko zinazotoka nje
 
Ok. Sijasoma hii tamthilia sina muda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…