Hivi maana ya kuwa na madirisha ya Wahudumu 5 au 7 benki ni nini?

Hivi maana ya kuwa na madirisha ya Wahudumu 5 au 7 benki ni nini?

Tengeneza Njia

Senior Member
Joined
Jul 29, 2022
Posts
121
Reaction score
205
Hii imekuwa ni kero ya muda mrefu sana sana sana, unaenda benki unakuta kidirisha kimoja au viwili tu ndo yana wahudumu mengine yote "closed" na nyomi la watu ni kubwa, watu wamekaa muda mreefu na hakuna kinachofanya na meneja kuangalia urgency na kuamrisha Watendaji wake kusaidia wateja.

Unaenda benki unatumia masaa matano.

Hebu hili liangaliwe.
 
Hii imekuwa ni kero ya uda mrefu sana sana sana, unaenda benki unakuta kidirisha kimoja au viwili tu ndo yana wahudumu mengine yote "closed" na nyomi la watu ni kubwa, watu wamekaa muda mreefu na hakuna kinachofanya na meneja kuangalia urgency na kuamrisha watendaji wake kusaidia wateja.

Unaenda benKi unatumia masaa matano.

Hebu hili liangaliwe.
Halafu ni kama wanaigana huu utaratibu...
Lengo kuhudumia kwa haraka.Ila tatizo huja ktk madirisha5 unakuta moja au mawili yanahudumia inakera!.
 
Ifikie wakati tupaze sauti zetu kukemea huu unyanyasaji. Kwa kweli inachosha sana.

Maana unakaa foleni zaidi ya masaa kupata huduma! Kisa tu wahudumu ni wachache, halafu unakuta madirisha mengine yako wazi tu.
 
Kuna benki moja maarufu sana ni balaa! Madirisha mengi ila zinazotoa huduma ni Moja au mbili
 
Hii imekuwa ni kero ya muda mrefu sana sana sana, unaenda benki unakuta kidirisha kimoja au viwili tu ndo yana wahudumu mengine yote "closed" na nyomi la watu ni kubwa, watu wamekaa muda mreefu na hakuna kinachofanya na meneja kuangalia urgency na kuamrisha Watendaji wake kusaidia wateja.

Unaenda benki unatumia masaa matano.

Hebu hili liangaliwe.
wana - Incourage matumizi ya mawakala wao maana huko wanatupiga zaidi
 
wana - Incourage matumizi ya mawakala wao maana huko wanatupiga zaidi
Kuweka hela kwa wakala ni bure, kuhamisha hela hata kwa simu hata kutoka benk nyingine kwenda nyingine inawezekana.

Mitandao mliyo nayo mnatumia tu kuchat au

Twende ki dijtali wadau, kuna internet banking, unafanya kila kitu kiganjani mwako.
 
Siyo benki tu,hata ukienda kwenye vituo vya mwendo kasi mfano moroco na kimara mwisho ,gerezani ipo hiyoo

Ova
 
kuweka hela kwa wakala ni bure, kuhamisha hela hata kwa simu hata kutoka benk nyingine kwenda nyingine inawezekana
mitandao mliyo nayo mnatumia tu kuchat au
twende ki dijtali wadau, kuna internet banking, unafanya kila kitu kiganjani mwako
Mimi kadi yangu iliisha muda wake lakini hata sijajisumbua kwenda kuchukua nyingine..

Kila kitu namaliza kwenye simu..nikitaka kutoa kwenye ATM nachukua tu pin kupitia simbanking app navuta mpunga ukutani..

Kudeposit,mawakala everywhere.

Yanini kujisumbua na foleni??
 
Back
Top Bottom