Hivi mabasi ya mwendokasi yana mwenyewe? Au yanajifia kama daladala za UDA?

Hivi mabasi ya mwendokasi yana mwenyewe? Au yanajifia kama daladala za UDA?

Ndani ya gari kunanuka jasho na mvundo wa mrundikano wa watu. Mtu ata ukibeba kukuchoma na chips hakuna harufu utakayoisikia
 
Hakuna kitu sisi wabongo tunaweza kukiendesha kikadumu...
 
Huo mradi umeshajifia , watu wanasubiri aina nyingine ya usafiri.
 
Viongozi wa juu wa nchi (raisi, makamu au waziri mkuu) waingilie kati huu mradi kwani waziri husika anaonekana hajui kinachoendelea. Mradi badala ya kuwa komboa wananchi umegeuka na kuwa mateso.
1. Magari yamekuwa machache sasa hivi kiasi unaweza kukaa kituoni zaidi ya saa nzima ukisubiri gari la ruti yako huku mengine yakipita na abiria wachache sana kuelekea ruti nyingine na mbaya zaidi mengine yanapita matupu kurudi yadi kupaki
2. Abiria kujazana sana hasa asubuhi na jioni mpaka kufikia wengine kudhalilishwa na wahuni (dunga dunga)
3. Hakuna wasimamizi kwenye vituo vikubwa ambao wengeweza kupiga simu makao makuu iwapo vituo vimezidiwa na abiria ghafla ili watume mabasi matupu.
4. Hakuna uangalizi kabisa kwenye kituo cha faya ambacho ndio kiunganishi cha kwenda hospitali ya muhimbili na baadhi ya shule hivyo wanafunzi na wagonjwa wanasukumwa. Ajabu vituo vingine wanasimamaia abiria kupanda kwa foleni lakini hapa faya ambapo wagonjwa ndio huunganisha kwenda muhimbili wagonjwa wanaachwawasukumane na watu wazima.

Iwapo serikali imeshindwa kuuendesha basi wamuuzie tu mfanyabiashara kama Bakhresa wao serikali wabakie wapate kodi tu.

Ni mtizamo tu.
 
Nimefika Dar es salaam nikafanikiwa kupanda magari ya mwendokasi nikajiuliza viongozi wenye dhamana wameisha DSM? Mabasi yamechoka, yanajaza abiria hadi milango haifungi, yapo machache na hakuna msimamizi serious unayemwona mwenye lengo la kuyatunza yadumu.

Kwa namna mabasi haya yanavyoendeshwa na kwakuzingatia utaratibu mzima wa ukataji tiketi, ukaguzi wa tiketi na usimamizi wa ulinzi wa abiria niseme fedha za walipa Kodi zinatumika vibaya.

Watu wetu weusi hao hao wanamiliki mabasi ya mikoani na siku zote huduma unaona zinaboreshwa; wamepewa mradi wa serikali hakuna mwenye uchungu nao hadi aletwe Mzungu aje atusaidie kukata tiketi, kupakia abiria, kulinda NK......Nani katuloga?

Kwa huduma hizi mbovu bado unasikia IPO mamlaka ya serikali imepandisha nauli.....unasikia MTU anasema tumepandisha nauli kumvutia mwekezaji huku wananchi wakiteseka.

Kampuni hata chenchi zakuwarejeshea wateja haina kweli? Kwamba mradi wa serikali watu wanaamua kutotafuta chenchi Kwa lengo lakuwadhulumu wananchi kidogo walichonacho! Kwamba abiria asiye na pesa kamili Hana Haki, viongozi mpo wapi? Au mnasubiri waziri mkuu au Mhe. Rais atembelee huu mradi wakaulize kwanini wananchi wanalazimishwa kuja na chenchi kamili? Wakaulize kwanini watu wanajazwa Hadi kuyafanya magari kuaribika mapema?

Watu tunatafuta kazi hatuna then wapo watu wanaunderperfom mnawafumbia macho kisa ajira za undugu...poa
Abiria ni wapumbavu sana.pale mlangoni huwa wanagongwa hadi wanatoka na vilema.Hata ijae vipi ikisimama wanapanda.
 
Kile kichwa kingekuwa kinakubali kushauriwa kingekuwa hai hadi leo.
Alikuwa muoga kukosolewa kiasi cha kupoteza wakosoaji wake kina ben saanane ETC.

Apumzike kwa amani.
mkuu ukianza vita ya kuondoa upumbavu, wa kujitetea ni wengi mno huwezi kuelewa umsikilize nani so, wakati mwingine kwa kuwa wewe unajua ni kitu gani unafanya inakubidi ujisikilize wewe mwenyewe... Excuse ni nyingi sana ukionesha misimamo. Namfeel sana yule mwamba... Lait ungekuwa ww ungeona, wewe imagine unagundua upumbavu unafanyika sehemu fulani unakasirika sana, unaamua kwenda kufukuza wazembe alafu anatokea mtu anakushauri usifanye hivyo kwa sababu katiba hairuhusu.
 
Huu mradi ni Muhimu sana na mipango ya kuuleta hapa Tz ulikiwa na mafanikio makubwa sana ila wasimamizi waliopo washashindwa kujua nn wanataka mfano;

Juzi nimetoka gerezani nakwenda mbezi nikaambiwa tiketi zipo nikapewa tiketi moja yenye kiwango cha fedha mpaka mbezi

Cha kushangaza nafika kimara nashuka naelekea kwenye foleni ya mbezi naambiwa kakate tiketi nyingine

Nimewanyesha tiketi moja yenye kiwango cha 650+ 400 mbezi wamekataa kabisa sasa najiuliza kwani mradi wa dart ni wa watu wawili?

kwamba gerezani kuna mmiliki wake na kimara kuna mmiliki mwingine
Niliona isiwe tabu nikaenda kukata tiketi nyingine japo kwa shingo upande

Narudia mradi ulikuwa na lengo zuri ila usimamizi umekuwa very poor
 
MKITAKA MABADIRIKO YA KWELI, ANZENI NA KULE IKULU.
-BY-
 
Watalam wa IT mnajionaje? mwendokasi wanarudi nyuma kila leo,kivipi?wakati mradi unaanza yale maneno ya basi linaenda wapi yalikuwa digital na kila kituo kinachofuata kinatajwa sasa baada ya kuachiwa tumeanza kubandika vibao vya mbao vimeandikwa kwa mkaa.
 
Back
Top Bottom